GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,871
Kama ni Rais huyu huyu Samia Suluhu Hassan alishasema katika moja ya Hotuba yake Kubwa kuwa Watanzania tusiache na wala tusiogope Kumkosoa leo hii Spika Ndugai nae katoa Maoni yake kwanini aandamwe na aonekane Mkosaji Mkuu?
Moja ya Kazi Kuu ya Media inayojitambua ( Siti hii yetu ya Waswahili ) duniani kote ni kuweka Uwiano ( balance ) katika ama Kuwahabarisha Wananchi au katika Kulifafanua Jambo fulani lenye Public Interest katika nchi husika.
GENTAMYCINE hapa sitaki nieleweke kuwa labda namtetea au nimeumia Spika Ndugai jana kuamua 'Kujiuzuru' Kwake vile bali Kilio changu Kikubwa ni kwa Media yetu Kushindwa Kuwajibika Kitaaluma na badala yake imekuwa ni 'Kisemeo' cha Kuunga mkono kila ikisemacho Serikali na Rais wa nchi.
Na vile vile GENTAMYCINE nisieleweke na 'Waswahili' kuwa nina Chuki na Rais Samia Suluhu Hassan tena huenda Mimi ambaye huwa namkosoa na nitaendelea Kumkosoa machoni kwa Mwenyezi Mungu ndiyo nikawa nina Upendo nae mkubwa kuliko Wanafiki na wale Team Kujipendekeza wengi Kwake walivyo.
Hivi ukiwa tu 'Critical Thinker' na ukiweka pembeni Hisia za Siasa ( kutokana na Vyama vyetu ) hii Kauli ya Spika Ndugai kuwa tusikope sana, tuimarishe Tozo zetu za Ndani ili huko mbeleni Madeni yasije Kutuzidi na nchi ikauzwa au ikapigwa Mnada ina Ubaya au hata Ukakasi wowote?
Cha Kushangaza baada ya Kauli hii ya Spika Ndugai 98% ya Vyombo vyote vya Habari nchini Tanzania navyo ama kwa Kushinikizwa au kwa Kujipendekeza au kwa Kukubali Kwao Kumezwa na Mamlaka au ninakokuita kwa Kuoza Kwao vikaanza Kumuandama Spika Ndugai na 'Kushadadia' Maoni ya Wanafiki na 'Waswahili' ndani ya Chama Tawala ( CCM ) mpaka lile walilolitaka au walilosetiwa nalo kama 'Agenda' likatimia.
Na tatizo la Watanzania wengi ( kama 75% ) yale ambayo ama wanayasikia katika Redio na Runinga au Kuyasoma katika Magazeti ya kila Siku ndiyo wanayaamini na Wao wakikaa huko Vijiweni wanakoleza zaidi mpaka Sumu ya Uwongo, Uzushi na Majungu inazidi Kusambaa katika Vichwa vyao wakati huenda wangetulia na Kutafakari zaidi wangekuwa na Uelewa mpana wa Kuchambua Masuala Kiundani.
Na Kirusi kingine kilichoibuka ( kilichojitokeza ) hasa katika Tanzania hii ya Miaka 15 hadi 20 iliyopita ni kwamba Watu ambao ni 'Critical Thinkers' wa Ukweli wakiwa wanajitokeza ama Kukemea, Kukosoa, Kupinga na hata Kushauri kwa Kujenga wanaanza Kuonekana ni Maadui wa Tanzania, Wanatumika na ni Wapinzani huku hata muda mwingine Wakitishwa au Kubambikiziwa Kesi kama sehemu ya Kuwanyamazisha na muda mwingine hata kuwahishwa Udongoni kabla ya Mola / Maulana kukuita.
Sikupenda jinsi Spika Ndugai alivyokuwa akiliongoza na akiliendesha Bunge ila sijapendezwa zaidi na jinsi Media ya Tanzania ilivyolikabili hili Sakata lake kwani imelikabili 'very unprofessional' na kwa Kujipendekeza zaidi kwa Mamlaka kwani Spika Ndugai kama Mtanzania nae alikuwa na Haki ya kutoa Maoni yake.
Tanzania inahitaji mno Critical Thinkers.