Tanzania inazidi kuwa Jangwa, je hii ni laana kwa Matendo tuyatendayo?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Waziri wa Mazingira January Makamba amepiga hizi picha na kusema

"Nimepiga picha hizi chache za mito toka angani, nikiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam. Mito mingi imekauka, na kujaa udongo na mchanga kwa kiasi kikubwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira katika vyanzo vyake, na mabadiliko ya tabia nchi. Tuna kazi kubwa ya kufanya kuinusuru nchi yetu na tishio la jangwa".

Imenitisha sana. Kumbe hata Serikalini wanayaona haya ila wamekaa nayo moyoni.
28c3d7d6004a965afbaf0585a653668e.jpg
e6d17c85047670234051e59b45021883.jpg
dfb94c9ac952af48f10a9f307869a391.jpg

Mungu tunusuru.
 
Bora makamba katoa sababu za kitaalamu,angekuwa yule mwingine angetafuta jina la adui yake ,akaliundia kamati ili kumuaibisha
 
Duuh balaa hili!! Sasa yeye kama waziri wa ofisi husika angetuambia pia ni malengo gani amepanga afanye ili kunusuru janga hilo lisizidi!? Au ndo hivyo tena mawazir wetu hukosa ubunifu kwenye ofisi zao?

Pilato 007
 
Jamaa ni kiazi, tuletee na picha za miaka mitano Kabla!

JPM hadi 2025, hutaki hama nchi. !
 
Aliyetulea Laana unamjua unachofanya hapa ni kutaka kupindisha ukweli
 
Huwezi kumuwinda mwenzio na smg ukategemea Mungu atakuacha anakupa punishment mdogo mdogo.
 
Yawezekana hizo ni seasonal rivers ambzo zinakuwa na maji yanayotirirka wakati wa msimu wa mvua tu,na kukiwa hakuna mvua inakauka.
 
Huwa nashindwa kuamini macho yangu pale ninapokumbuka miaka 15-20 iliyopita na niliyokuwa nayaona, leo hauwezi kuamini kabisa nikianza kukupitisha kwenye hayo maeneo ama kukusimulia. Kanda ya ziwa ilikuwa ni sehemu yenye mito inayotiririka miezi yote lakini leo huoni miti/mapori na wala si hiyo mito. Serikali na watendaji wameamua kuongea siasa huku nchi yetu ikiteketea. Leo hii hamna tena ule uoto wa asili, kila siku ni mikaa, mbao na kuchoma tofari na nyika. Sijui miaka 30 ijayo mbeleni itakuwaje

Watanzania kutokujari kutatumaliza, hapa hakuna mjanja wala mjinga na msomi wala mbumbumbu. Likija watakaoumia ni watanzania sote
 
Mabadiliko ya Tabia ya Nchi ( climate change ), na hilo si janga la Tanzania pekee kwa kipindi cha karibuni tumekuwa tukiona maeneo mengi duniani yakiathiriwa na tatizo hili haswa kutokana na Shughuli za binadamu
0e9a8bab8c0cba7d2da457d5600b942a.jpg
 
Back
Top Bottom