Hivi mikataba ya ndege, SGR, Stifler's , Chato airport ilipitia bunge lipi?Dalili ya mvua ni mawingu, hali hii inatokana na matamshi na vision ya kiongozi aliyeko Madarakani.
Si kweli kwamba utaratibu wa uwekezaji nchini ni mbaya, nakataa hili kwa ushahidi kwa kupitia kauli ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini Rostom Aziz aliyoitoa akiwa ziarani Kenya aliyeambatana na Rais Samia.
Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania,hebu lingania makampuni ya Tanzania nchini Kenya ,ambayo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini kwetu ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.
Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.
Niseme tu hayati Magufuli alikuwa ni mtu ambaye Mara nyingi alifanya tafiti na kupata takwimu kabla ya Maamuzi magumu kutolewa, hii ilimfanya aheshimike sana duniani licha ya mahasimu wake kumshusha thamani.
Hayati Magufuli enzi ya utawala wake hakupenda kabisa ubabaishaji na hili lilimgharimu sana .ndicho kilichopelekea baadhi ya makampuni na wafanyabiashara matapeli kukimbia nchini, ambao Mama Samia kaenda kuwapigia Magoti.
Sasa naiona Tanzania inarudi ilipotoka, Tanzania inaenda kuwa nchi ya wachuuzi tena ,pamoja na raslimali lukuki ilizonazo,hii inaendana pia na kushuka kwa morali ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu na kujiingiza kwenye rushwa.
Maneno aliyosema Rais Samia alipokutana na wafanyabiashara nchini Kenya ya kwamba anaenda kuifungua nchi. Je, ni lini nchi hii ilifunga mipaka yake?
Nafikiri angesema hakusanyi kodi tena wawekezaji ruksa kufanyabiashara nchini bila masharti tungrmuelewa na jambo hilo halipo duniani, kodi ndio msingi wa maendeleo, serikali kama haikusanyi kodi haina uhalali wa kutawala.
Mwisho kataja bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda, tusikubali uharaka haraka wake kusaini hii mikataba bila ya kujiridhisha, bunge lihakikishe mikataba hii haisainiwi gizani kama alivyofanya kwenye hili bomba la kuuza gasi nchini Kenya.
Mambo haya yalifanyika sana enzi za awamu ya nne, na yameligharimu sana taifa baada ya hayati Magufuli kutaka kuinasua nchi kwenye ujinga huu, naona Mama Samia anataka kupita kulekule kulipotugharimu. Vinginevyo nchi hii tunaenda kugawana mbao, Magufuli kaondoka kawatoa watanzania tongotongo machoni.