Tanzania inavyo uchekesha ulimwengu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,272
Wananchi wamekosa huduma ya umeme wa uhakika, bila aibu Mh. Pinda anatangaza ongezeko la kupanda kwa bei.
Jamani kama sio wizi ni nini? Mtu uongezewe bei ya huduma ambayo huipati.
Kweli dunia inatucheka, yaani tunasukumwasukumwa na sisi tunakubali.
Kuna haja ya kuandamana kupinga ongezeko hili la bei. Wakitaka wazime kabisaaa mitambo yao
 
nchi imajaa mazuzu na mazezeta mkuu,miaka 50 ya uhuru,bado kuna watu(sio binadam) wanaota ccm iendelee kutupeleka gizan zaidi.KIDUMU CHAMA CHA M...
 
nchi imajaa mazuzu na mazezeta mkuu,miaka 50 ya uhuru,bado kuna watu(sio binadam) wanaota ccm iendelee kutupeleka gizan zaidi.KIDUMU CHAMA CHA M...

Wakiongozwa na wote wanaotumia huduma za luku,

Unalipia umeme kabla halafu huupati na bado tunakenua na kwenda kuwasha majenereta ( wenye hela ) wengine wa kati wanaamunua kukaa kwenye container kula laga kuogopa giza.

Wenzangu na mie ni mwendo wa mishumaa na vibatari chemli na karabai majumbani.

Watanzania tuamke, dhuluma hii ikome haraka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jamani Pinda ametumwa. Mwacheni apumzike asije shusha chozi.
 
Uzalishaji una gharama kubwa kwa sasa.
Sio uzalishaji ndo wenye gharama,
Bali mikataba ndio imeipa ugharama huo uzalishaji.
Ufisadi wa kulipana "capacity charge" hata kama hatupati umeme ndio unatupelekea huku.
Dudu liitwalo IPTL litaendelea kutunyonya mpaka mwaka 2015 pale mkataba wa kifisadi aliosaini yule jamaa pale magogoni kipindi hiko akiwa Waziri utakapoisha.
Watanzania tumezidi sana ukarimu kupindukia kuendelea kua na huyu amaa,
Sishangai mtu akimkarimu mgoni wake chai baada ya kumfumania!!
 
Uzalishaji una gharama kubwa kwa sasa.

Gharama zitakosa wapi kuwa kubwa kupita kiasi kutokana na mikataba ya kifisadi ya Dowans, IPTL, Symbion na hao wachimba gesi toka Canada na gharama kubwa za kuwahonga Wabunge ili kuhakikisha bajeti ya Madini na Nishati inapitishwa.
 
hivi,wale wamerekani waliokuja kwa mbwembwe na mrs clinton wameishia wapi na mitambo ya dowans? ama nao wanasubiria muda uende waanze kuvuta kwa ustaarabu? manake sasa hivi mgao hauna ratiba tena,umegeuka mgao wa giza!
 
Hala fu kuna mwingine eti anadai Tanzagiza is like the Germany of Africa! Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
hivi,wale wamerekani waliokuja kwa mbwembwe na mrs clinton wameishia wapi na mitambo ya dowans? ama nao wanasubiria muda uende waanze kuvuta kwa ustaarabu? manake sasa hivi mgao hauna ratiba tena,umegeuka mgao wa giza!
Mazee sio kila kitu chenye lebo ya US kinalipa, hata changa la macho la Richmonduli lilianzia Merekani.
 
Hao ndio viongozi wetu wanaofikiri kwa kutumia masaburi wenyewe hawaguswi kabisa na tatizo hili.
 
haya sasa mm binafsi niko tayari wewe je? chukua hatua. tukiandamana hawa watu utasikia jamani basi tulikuwa tunajaribu tuu, atatoa na machozi huyo jamaa,hebu tazama sukari,ajali,umeme,nk
 
Wananchi wamekosa huduma ya umeme wa uhakika, bila aibu Mh. Pinda anatangaza ongezeko la kupanda kwa bei.<br />
Jamani kama sio wizi ni nini? Mtu uongezewe bei ya huduma ambayo huipati.<br />
Kweli dunia inatucheka, yaani tunasukumwasukumwa na sisi tunakubali.<br />
Kuna haja ya kuandamana kupinga ongezeko hili la bei. Wakitaka wazime kabisaaa mitambo yao
kama wanaona kuwa kupandisha bei kutaleta uboreshaji wa sekta ya umeme, mimi naona hamna haja ya kubishana nao. Kama watashindwa kuboresha huduma hiyo huku tunalipa pesa kubwa hapo ndipo nitawapinga. Tujue kuwa kama tunataka huduma nzuri, tukubali gharama. Ngoja nione mwezi wa 12 itakuwake kulingana na ahadi zake.
 
Kidumu Chama cha Masaburi!!!!! kuwe na umeme kusiwe na umeme bill haipungui afu mbona Mkuu huyu anaingilia kazi za BADRA MASOUD?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom