NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Haya ni majanga, sina uhakika ila ikibidi mnisahishe ila niliwahi kuona nchi kama Kenya hapo hizo shule zipo, Huko Rwanda wapo next levels wala si wa kucompare nao.
Hivi katika ulimwengu huu ambao tunazidi kujionea jinsi mifumo ya computers inavyozidi kuwa sehemu kubwa ya uchumi, biashara, government administration, private life, n.k. inaingia akilini kweli kwamba tunakosa hata shule maalum hata moja tu ya kuwaandaa watoto wenye vipaji vya hivi vitu ama interest na bidii ya kujifunza ?
Kama sio kutengeneza utegemezi mpya kwa maksudi kabisa ni nini hiki ?
Huwa hatuoni aibu watu kuanza kujifunza haya mambo mpaka wafike vyuoni tayari washaanza kunyoa ndevu ?
Nimeona kuna kombi ya computer ya PMC lakini niliwahi kuifatilia nikaaona bado sana, ni mara kumi tu hata mtu aende chuoni aanzie certificate maana huko shuleni hampo huru kutumia laptops, somo la computer ni moja tu, waakim wanaofundisha nao ni stress tu, n.k. na hapo bado wanaoenda kusoma ni wale ammbao wapo kwenye kingo za late teenage ages (17 - 19)
Ingependeza kuwe na shule ya kuanzia form 1 iwe maalum kwajili ya mambo ya computer zaidi.... masomo kama biology na history yanawekwa pembeni huko yanafidiwa na masomo mengine ya computer, kuwe na computer labs ambazo mda wote zipo wazi, kuwe na unlimited internet yenye speed kali, watoto wawe wanakwenda kwenye mashindano yoyte kama yapo, n.k.
Rais Samia nae nilisikia anapita pita humu ila nae sijui kama anagusa hili jukwaa, Mama unaupiga mwingi sana ila jaribu pia kuupiga kwenye ulimwengu huu ambao mambo ya Tehama yamekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu, piga na huku nasi tusiwe wategemezi kupita kiasi kwenye vitu hivi vinavyoibadili dunia,