Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,968
Tanzania inatarajia kuanza kupokea shehena ya kwanza ya chanjo ya korona mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu iwapo mipango itakwenda kama ilivyopangwa.
Taarifa ambazo Moonlight imezipata kutoka Geneva Uswis Makao makuu ya Global Alliance for Vaccine and immunisation kwa kifupi GAVI muungano unaosimamia ununuzi na usambazaji wa chanjo duniani, imesema kuwa Tanzania imewasilisha bajeti ya kiasi cha dola millioni 208.
“Tanzania iliwasilisha ombi lake hapa mfupi sana kabla ya muda kufungwa jana na maombi yao ni kuhusiana na kupewa chanjo itakayojumuisha pamoja na utafiti, elimu kwa wananchi juu ya chanjo na mambo mengine na mpango wao unaanza Julai 2021 mpaka Juni 2022 ni kiasi cha dola milioni 208” kilidokeza chanzo chetu.
Muda wa mwisho kwa nchi zinazotaka msaada kutoka GAVI kwa ajili ya chanjo hiyo dhidi ya korona ulikuwa June 15 saa kumi jioni kwa saa za Uswis.
Wakati huo huo taarifa kutoka wizara ya afya zinasema kamati ya wataalam uliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan juu ya janga la korona inatarajiwa kukutana Morogoro wiki ijayo kupanga jinsi ya kushughulikia msaada huo kutoka GAVI.
Aboubakary Liongo
Moonlight Media
Zaidi, soma; Uzi Maalum: Ujio wa Chanjo za Kupambana na Corona, nini Mtizamo wako juu ya COVID -19?