#COVID19 Tanzania inatarajia kuanza kupokea shehena ya kwanza ya chanjo ya Corona mwanzoni mwa Disemba

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Tanzania inatarajia kuanza kupokea shehena ya kwanza ya chanjo ya korona mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu iwapo mipango itakwenda kama ilivyopangwa.

Taarifa ambazo Moonlight imezipata kutoka Geneva Uswis Makao makuu ya Global Alliance for Vaccine and immunisation kwa kifupi GAVI muungano unaosimamia ununuzi na usambazaji wa chanjo duniani, imesema kuwa Tanzania imewasilisha bajeti ya kiasi cha dola millioni 208.

“Tanzania iliwasilisha ombi lake hapa mfupi sana kabla ya muda kufungwa jana na maombi yao ni kuhusiana na kupewa chanjo itakayojumuisha pamoja na utafiti, elimu kwa wananchi juu ya chanjo na mambo mengine na mpango wao unaanza Julai 2021 mpaka Juni 2022 ni kiasi cha dola milioni 208” kilidokeza chanzo chetu.

Muda wa mwisho kwa nchi zinazotaka msaada kutoka GAVI kwa ajili ya chanjo hiyo dhidi ya korona ulikuwa June 15 saa kumi jioni kwa saa za Uswis.

Wakati huo huo taarifa kutoka wizara ya afya zinasema kamati ya wataalam uliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan juu ya janga la korona inatarajiwa kukutana Morogoro wiki ijayo kupanga jinsi ya kushughulikia msaada huo kutoka GAVI.

Aboubakary Liongo
Moonlight Media

Zaidi, soma; Uzi Maalum: Ujio wa Chanjo za Kupambana na Corona, nini Mtizamo wako juu ya COVID -19?
 
Uganda walipojidunga chanjo, kitu kikalipuka, Malawi wamechoma moto chanjo zote za covid walizopewa msaada baada ya kugundua ni feki, Sasa sisi na huu utaalamu wa ndio mzee, ni neema ya Mungu inahitajika.
 
Hili la uharaka wa kuleta na kupata chanjo pasipo kujiridhisha wenyewe juu ya usalama wake kiafya kwa wananchi wa Tanzania, nakubaliana kwa 100% na msimamo na wasiwasi juu ya uamuzi huu na hayati Dr. JPM.
 
Masharti ya wazungu juu ya kupata misaada yao wakati mwingine yanatulazimu kukubali hivi vitu, masikini hana uhuru kabisa.
 
Mashabiki wa mwendazake, mzee hamnazo watapinga baada ya kumeza ARV za mzungu, sindano za polio za mzungu na watachati kwa techno ya mzungu.

.hamnazo aliwaondoa ubongo wafuasi.

Mimi nitachomwa.
 
Tanzania inatarajia kuanza kupokea shehena ya kwanza ya chanjo ya korona mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu iwapo mipango itakwenda kama ilivyopangwa...
Waanze kuchanja hao wanakamati.Ili waendelee kuwa na afya ya kuishauri serikali. halafu wafuatiwe na mawaziri(wanasiasa).

Mwisho kabisa iwe wale wahudumu wa afya,maana kama kuna side effects zitakuwa tayari zumeshatatuliwa.
 
Kumekuchaaa

Hatuwezi kukaa kilokoloko eti Bhupiji na matunguri mengine
Hatua nzuri sana....Mataga yamenuna

Msoga hoyeee
 
Uzuri wa hii chanjo hulazimishwi.
Kama hutaki kuchanjwa unaacha na hupati visa ya kuingia baadhi ya nchi.
 
Uganda walipojidunga chanjo, kitu kikalipuka, Malawi wamechoma moto chanjo zote za covid walizopewa msaada baada ya kugundua ni feki, Sasa sisi na huu utaalamu wa ndio mzee, ni neema ya Mungu inahitajika.
Ujalazimishwa we mfuasi wa dikteta kichaaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom