Salaam Wakuu,
Kupitia WhatsApp yangu nimetumiwa ujumbe wa tahadhari kuhusu kuwepo kwa Mvua katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Ujumbe huo unaeleza:
Shinyanga, Dar, Pwani, Mafia,Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma na Kagera tujiandae, kutakuwepo na Pacific El nino na Atlantic El nino, mvua zitakuwa kubwa na hatari sana, Mungu atunusuru. Hali ya hewa tayari imebadilika kuanzia juzi, upepo umeanza katika bahari za Atlantic, Pacific na Hindi, Wavuvi wameanza kuzuiwa kwenda kuvua na Meli za tafiti zimeanza kukumbana na dhoruba kali sana Baharini, picha za satellite sio nzuri kabisa. Tunatarajia magonjwa ya Kuharisha, Dengue, Malaria na Homa kuongezeka, tuchukue tahadhari mapema.
Tuangalie nyumba zetu kama zinavuja, turekebishe, tununue Neti za Mbu, tuangalie miundombinu ya maji taka kwenye nyumba zetu. Tununue Jik na water guard kwa ajili ya kuweka kwenye maji ya kunywa, kumbuka kipindi hicho umeme utakatika sana kwa hiyo tununue taa za kuchaji. Sehemu za nyumba ambazo sio imara turekebishe. Tuweke akiba ya chakula na dawa.
Tununue dawa za Mafua, dawa za Watoto za Mafua na Kuharisha, na dawa za Malaria. Tuhifadhi vyakula vikavu kwa mfano nafaka kwa wingi na tununue vitu vya kuhifadhia vyakula. Shinyanga, Dar, Pwani, Tanga zitapata mvua za kiwango cha juu zaidi (above normal to normal).
Upi uhalisia wa ujumbe huu?

- Tunachokijua
- Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaeleza kuwa Taarifa hii siyo sahihi, na kusisitiza kuwa ipuuzwe.
Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kusisitiza umma kufuatilia na kuzingatia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA pamoja na ushauri wa kisekta unaotolewa na Taasisi zenye Mamlaka kulingana na sheria na taratibu za nchi.
Ikumbukwe kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria Na.2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa mtu yeyote kutoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kinyume na taratibu na bila idhini ya Mamlaka.