Tanzania inarundo la wazalendo toka kwenye vyama vyote vya siasa, asasi za kidini, serekalini, kwenye majeshi yetu na pia raia wa kawaida

Kolomije wa Dar

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
284
789
Bwana yesu asifiwe, Tumsifu yesu Kristo, Assalam Alekhu...
Wakati nasubiri barua ya kujieleza ni kwanini nisifutwe wacha niyatoe yaliyo moyoni.

Tanzania ni kubwa kuliko ccm, Chadema au Act, ni Kubwa kuliko Magufuli, Mbowe au Zitto.
Tanzania inarundo la wazalendo toka kwenye vyama vyote vya siasa, asasi za kidini, serekalini, kwenye majeshi yetu na pia raia wa kawaida mitaani na hili ndilo linaloifanya Tanzania kusimama pasipo kutetemeka.

Nina imani maraisi wastaafu wote walikuwa ni wazalendo wa kweli na ndio maana hatujawai ona popote wakijitangaza/kujinadi kuwa wao ni wazalendo Bali matendo yao ndio yaliowanadi na kuwatangaza.

Tanzania tumekuwa na utamaduni wa kuzikana, kusalimiana, kuvumiliana, kuoana, kuheshimiana katika siasa. Na hili lililelewa au kujengwa na wazalendo waliopata nafasi katika Tanzania.

Rai yangu kwenu wazalendo wa kweli. Mzalendo hastaafu siku zote huitumikia nchi yake, husimama upande wa Taifa na sio upande wa MTU.
Msikubali kuona itikadi za vyama vikitugawa, msikubali kuona hii hali ya mtu kuwa chama A ni bora kuliko chama B.
Watanzania wote tuna haki sawa.
Kemeeni uovu wowote unaofanywa hapa Tanzania.
Wakemeeni hao wanaojiita wazalendo wakati sio wazalendo.
Semeni kweli ili kweli iiponye Taifa.

Wazalendo mpo, na huu ndio wakati muafa kwenu kusimama kwenye nafasi zenu.

Wazalendoooooooo
 
historia inaonyesha mwanadamu hajawahi kuushinda umma... it's the matter of time. be free be good
 
Back
Top Bottom