Tanzania inarudi nyuma kimaendeleo kwa kasi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania inarudi nyuma kimaendeleo kwa kasi.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The hammer, Mar 17, 2012.

 1. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Wakati nchi hii inapata uhuru haikuwa na vitu vingi vya kujivunia....Ila wakati wa uongozi wa Jk.Nyerere nchi ilijitahidi kujenga huduma nyingi za kijamii kama
  1:hospitali zote za mikoa na wilaya tunazoziona leo hii
  2:Shule za msingi na sekondari na vyuo vya elimu ya juu,veta na vinginevyo...
  3:Ujenzi wa barara mpya,ofisi za serikali sehem mbalimbali
  4:kuanzisha jeshi letu jipya...
  5:Ujenzi wa viwanda
  6:Miradi ya umeme na mawasiliano kama simu
  unaweza endeleza orodha

  Ila pamoja na serikali ya awam ya kwanza kujitahidi kufanya yote hayo,serikali zilizofuata zilishindwa na inaendelea kushindwa kutuletea vitu unique kama;
  1:Miradi mikubwa ya umwagiliaji
  2:Umeme wa uhakika usiotumia maji
  3:Uwekaji wa vifaa vya kisasa kwa hospitali zilizopo ili tuache kupeleka watu India kwa zamu tukiacha wengine wakifa wakisubiri foleni
  5:Uboreshaji wa huduma ya maji safi na taka mijini na vijijni
  6:Upimwaji wa viwanja vya makazi,viwanda,kilimo na mifugo
  7:Elimu bora
  8:Uboreshaji wa ajira kwa vijana kupunguza tatizo la ajira na maslahi kwa wafanyakazi
  9:Kuboresha mazingira ya uwekezaji wa viwanda na mauzo ya bidhaa za viwandani nje ya nchi
  10:Kuboresha usalama wa wananchi wake si viongozi wa nchi tu,wananchi wanajilinda wenyewe mfano wa bidhaa hafifu zinazoongizw nchini si salama km simu,vykula na madawa nk
  11:Utunzaji wa mazingira na mali asili za nchi
  12:
  13:
  Endeleza......


  TOFAUTI NI KUWA
  1:HUDUMA ZA HOSPITALI NI KAMA ZA ZAMANI
  2:HUDUMA YA UMEME SI YA UHAKIKA NA INAONEKANA NI ANASA KWA MWANANCHI WA KAWAIDA NA BAADHI YA MIKOA HAZIJAUNGANISHWA GRID YA TAIFA KM RUVUMA,RUKWA,KAGERA,KIKOMA N.K
  3:BARABARA IMEJITAHIDI ILA SI KWA KIWANGO AMBACHO CHA KURIDHISHA KWANI MIKOA MINGI LAMI ZAKE NI VICHEKESHO
  4:VIWANDA VINGI VILIVYOANZISHWA WAKATI HUO VIMEKUFA KM GENERAL TYRE,PHILIPS,TANELEC,NK
  5:UJENZI HOLELA USIOPANGIKA NA SEHEMU ZA KILIMO,MAKAZI,NA UFUGAJI HAZIPIMWA.KILA MTU AJUE ATAKAPOJENGA
  6:UTUNZAJI WA MAZINGIRA UMETUSHINDA KABISA.....
  7:USALAMA WA MWANANCHI HAUPO KABISA
  8:ELIMU IMESHUKA KWA KIASI KIKUBWA,LEO FORM 4 SI KAMA STD 7 MIAKA YA 80.
  9:KILIMO NI SIFURI.
  10:
  11:Endelea

  SERIKALI ZA AWAMU YA MWINYI-JK IMEJITAHIDI WAPI
  1:KUUA VYOTE VILIVYOTAJWA HAPO JUU HIVYO MATUMAINI YA WATZ KUDIDIMIA KABISA
  2:RUSHWA NA URASIMU VIMEONGEZEKA
  3:MATABAKA TAWALA YANAJULIKANA NA WATWANA WANAJULIKANA
  4:UJENZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEC UNARIDHISHA
  5:endelea(taja mazuri tu yaliyofanyika kwa awamu tatu)


  Je serikali inajivuna kila siku kwa kuwadanganya wananchi wakati hakuna inachofanya rasilimali zetu zinaenda bure na haziboreshi lolote kwa Mtanzania tofauti na wakati wa Nyerere.....Wananchi tunabaki kudanganywa na elfu 30 wakati wa uchaguzi tena wanaofanya hivyo ni watu wazima(mshahara wa elfu 30 kwa miaka 5 hilo nililiona wazi tena wanafurahia kwa kusema ni wakati wao wa mavuno hao wanaojiita kamati kuu za wilaya ccm)

  INAUMA SANA NCHI HII INATAFUNWA NA ITAISHA WANANCHI NDIPO TUTAKAJUTIA NA KUWAZA YASIYOWAZIKA
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tuwekee, awamu ya kwanza walifanya kipi na ya pili na tatu na ya nne.

  Utakuta ya nne imefanya zaidi ya vyote vya awamu zakabla ukijumlisha pamoja.

  Weka jedwali la takwimu hapa, usilete pumba.:
   
 3. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  umesahau vingi vya muhimu kama vile treni,meli,ndege hata viwanja kama kirumba mza na amri abed stadium ar vinazidi kuchakaa pesa zake hazieleweki zinaenda wapi?...angalia michezo ipo ipo tu hata haieleweki
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hakuna lami ndani ya mitaa hata mkoa mmoja hakuna mradi mkubwa wa maji kama ule wa jr arusha ,,soma vibao vyote bara bara hii imejengwa kwa hisani ya watu wa japan na so n so ,wachina walijaribu dar lakini hakuna maji hayatoki

   
 5. c

  collezione JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  kiukweli naweza sema Tanzania inasonga hatua 5 mbele na kurudi nyuma 7... Hapo hakuna cha kujipongeza
   
 6. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  nilishakuwekea mwanzoni kabisa ila kuna mdau kaongeze awamu ya kwanza vilijengwa viwanja vya ndege,viwanja vya mpira,treni,meli nk tena wakati huo madini yalikuwa hayachimbwi kwa kasi kama ilivyo hivi sasa na misaada ilikuwa si mingi kama ilivyo hivi sasa.....
  Sasa kama umeona ktk awamu zote 3 wamefanya jambo la maana litaje hapa tulione usibaki kusema wamefanya,mi nimekutajia we hujataja nani anaongea pumba...
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe unasema vimejengwa husemi wapi? tujuao tunajuwa kiwanja cha ndege cha dar kilikuwepo toka Uhuru, kipya kikajengwa wakati wa Mwinyi, cha Kilimanjaro kilijengwa wakati wa Nyerere.
   
 8. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ukiona mtu anatetea serikali ya awamu ya nne, sifa mojawapo kati hizi anazo.
  1. Ni mwanachama wa ccm amabaye anamaslahi ndani yake.
  2. Ni Muslim utaona mitazamo yake atasema either nyerere alifanya nini au atamtaja Mkapa.
  Kama tungeweka id zetu halisi mngeshuhudia
   
Loading...