Tanzania inaongoza kwa misaada, lakini wakulima wamepuuzwa

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
uchambuzi_katuni.jpg





Tanzania inaongoza barani Afrika kwa kupokea misaada ikiwamo mikopo mingi kutoka kwa wafadhili wa nje na taasisi za fedha za kimataifa kwa lengo la kuleta maendeleo bila kusahau kuwakwamua wakulima wa jembe la mkono.
Nchi yetu inaongoza ikifuatiwa na Ethiopia, Ghana, Uganda, Kenya, na Nigeria.
Lakini Tanzania kuwa ya kwanza kwa kupokea mikopo, hakulingani na kabisa na hali halisi ya umaskini uliokithiri kwa wakulima wa jembe la mkono na kilimo cha kutegemea mvua.
Duniani, Tanzania ni ya pili baada ya India kwa kupokea misaada mingi kutoka kwa wafadhili ambayo imeelekezwa kwa wakulima wa jembe la mkono, ikifuatiwa na Ethiopia, Ghana, Indonesia, Pakistan, Bangladesh, Vietnam, Uganda, na Kenya.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi moja ya kimataifa (syngenta foundation for sustainable agriculture) kwa kushirikiana na taasisi zingine rafiki wa kilimo, mwaka 2009, na matokeo yake kutolewa Agosti 2010.
Utafiti huo ulilenga wakulima wadogo wapatao 1,767 na hatimaye kubainisha nchi kumi zinazongoza kwa kupata misaada mingi zaidi au ufadhili mkubwa zaidi katika kuwasaidia wakulima wadogo ambao kwa hakika ni wakulima wa jembe la mkono.
Baadhi ya wafadhili waliotoa misaada ni taasisi 9 za fedha za kimataifa, ikiwamo Benki ya Dunia (WB), ambazo zilichangia asilimia 75 ya misaada yote, ikifuatiwa na taasisi za kitaifa (Bilateral Agencies) ambazo zilichangia asilimia 22 ya fedha zote.
Picha iliyojitokeza hapa, Bara la Afrika lilipokea misaada mingi zaidi kutokana na idadi ya miradi yake ikilinganishwa na mabara mengine.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania ni nchi ambayo imependelewa au kufanikiwa kupata mgao mkubwa zaidi kuliko nchi nyingine.
Utafiti huo umebainisha kwamba misaada ya maendeleo (ODA) iliyotolewa mwaka 2009 ilikuwa na thamani ya dola120 bilioni za Marekani, kati ya fedha hizo, dola 6.5 bilioni zilielekezwa katika Kilimo, dola 2.6 bilioni za Marekani zilielekezwa kwa wakulima wadogo.
Ukiangalia kiasi cha fedha ambacho kila nchi kilipata kuanzia mwaka 2009, utafiti huo ulibainisha kwamba kila shamba moja dogo (donor funding per smallholder farm) lilipata au lilipaswa kupata ufadhili wa dola 187 milioni nchini Tanzania, Ethiopia ilipata dola 44 milioni za Marekani, Indonesia dola 20 milioni za Marekani, India dola12 za Marekani, wastani kwa Afrika nzima dola 85 milioni za Marekani na wastani kwa dunia nzima (nje ya China) ni dola 48 milioni za Marekani.
Viwango hivyo vimepatikana kwa kugawanya kiasi cha fedha kilichopokelewa katika nchi husika, kwa idadi ya mashamba madogo yaliyopo.
 
Back
Top Bottom