The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,294
- 16,983
Tanzania ni moja ya nchi 10 masikini zaidi Duniani, hii ni rekodi ambayo Tanzania tumeishikilia kwa miaka mingi na wala hatuna mpango wa kuachia nafasi yetu hii adhimu kwa sababu kwa miaka yote tumekua tukifabya kila jitihada ili tuendelee kubakia pale pale au angalau kwenye 10 bora.
Kwenye miundombinu tunashika nafasi ya kwanza kua na miundombinu mibovu Afrika hasa kwenye miji mikubwa, ukianza na Dar es salaam, miunndombinu ni mibovu hakuna mfano, hadi unajiuliza hii nchi ina watu walioenda shule kweli? Nenda Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, kila mahali miundombinu ni mibovu, hakuna mpango miji, hii nchi ni kama haina serikali ya kusimamia hilo. Viongozi wetu wametembea sana ulaya, hawajifunzi? Yaani hata kupanga miji kwenye ardhi yetu tunahitaji misaada ya wanaoitwa mabeberu?
Kitu pekee tunaweza kujivunia ni amani kwenye dimbwi la umasikini.