Tanzania Inakwenda Wapi???????

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
59
Jamani nchi yetu inakwenda wapi??????? Mahospitalini karibia mwezi wa sita sasa huduma ya chanjo kwa watoto hakuna, mimi nina mtoto mchanga tumeshazunguka hospitali karibia zote hapa jijini na chanjo hakuna nadhani na watanzania wenzangu mmeshakutana na tatizo hili..... je hawa watoto wa awamu ya KIKWETE wataishi vipi bila ya hizo chanjo?????? je Serikali hela za walipa kodi inazipeleka wapi hadi huduma muhimu kama chanjo kwa watoto wachanga inakosekana tena kwa muda mrefu kama hivi??? au hela zote ndio zinagalamia safari za bwana mkubwa nnje (Ulaya)????? tujiulize jamani Watanzania Je tutafika kweli???
 
Hilo Mafisadi hawalioni kwa sababu watoto wao hata wakijikwaa dressing ya Donda inafanyiwa nje ya nchi.
Kwahiyo hawawezi kuliona hilo kama ni tatizo maana haliwagusi moja kwa moja.
 
sure hata mimi nina tatizo kama ilo,nimezunguka Hospitali zote hakuna chanjo,watanzania tumekuwa wapole mno.Nadhani umefika wakati mwafaka wa watanzania kuingia mtaani kama walivyofanya wenzetu wa Burma ili tuung`oe utawara wa kifisadi,vinginevyo tunakoelekea na Hospital zitaishiwa hata Aspirini.
 
Poleni sana jamani.
Hii ndo hali tuliyoijenga watanzania.Watu wakishapiga kura tunaiacha serikali ifanye itakavyo.Wakiboronga tunakaa kimya tukisubiri vyama vya upinzani viseme ili mambo yarekebishwe huku sisi tukiwa kimya.
Kuikemea na kuichukulia hatua ya hata kuwaondoa ni jukumu letu sisi watanzania wote. Kuigomea na kuipinga serikali si lazima mtu kuwa na chama.Chama chetu ni Tanzania.
 
Kuna member mmoja anajiita MTU alidai kuwa hatuzungumzii mazuri ya serikali, Mazuri ya kuzungumzia labda yangekuwa ndio hayo ya chanjo, lakini hata chanjo kwa watoto hakuna, sasa sijui ni lipi la kuzungumzia. Kama chanjo haipo Dar, Tunduru je? Wanging'ombe je?
 
Sasa ni wakati wa kuamka, watanzania tukatae upuuzi huu njia ni kuungana pamoja na kuiondoa hali hii kwa kuwaoondoa madarakani.Napendekeza kwa kuanza tuwe na maandamano ya amani kuwaoomba wang'atuke !!
 
Haya ni maneno magumu sana haswa unapoambiwa kuwa ndugu zako wanakufa kwa sababu ya kukosa tuu chanjo,
Eee mola linusuru taifa lako hili maana wanakufa watoto wachanaga ambao hawana hata hatia wala hajapiga kura kwa kupewa rushwa wala hawajawahi kuishabikia ccm .

Mola turehemu sisi waja wako maana hali hii inakuwa mbaya kila kukicha,

Rias wetu haoni kama kuna matatizo kila kukicha yeye ni kwenda kula kuku ulaya na marekani kila uchao,

Nawalilia watoto haw wasiokuwa na hatia ,
 
Ingekuwa ni swala la mpira Taifa star imeifunga msumbiji wangechangisha hela kuwapa, sasa jamani si wachangishe hela za kununua chanjo za watoto pia, mbona nchi yetu inatukuza mambo yasiyokuwa na maana ya maana inayapa mgongo, mpk siku JESHI LA WANANCHI watakapo amua kuchukua nnchi yao ndio mambo yatakaa sawa.
 
Haya ya kweli kuwa hakuna chanzo.. maana tunaweza tukazama kuzungumzia ufisadi tukaacha mambo yanayogusa maisha ya watu wa kawaida kama haya. Naomba taarifa wa ndugu ili tumtafute Waziri anayehusika na Afya. kina Domokaya naomba mniandikie kwenye PM ni vituo gani hivyo mlivyoenda na kama kuna mtu ana contacts za waganga wakuu wake... haitoshi kulalamika tu ni lazima tufanye kitu.
 
Domo Kaya pole sana Mtanzania mwenzangu.. tuna kazi kubwa sana ya kuwaelimisha wanachi kuwa wao ndio wana nguvu kuliko mawaziri. Nashidwa kuamini kuwa hospitali hazina chanjo.. sitaki kukubali kabisa... kwa nini?
 
Haya ya kweli kuwa hakuna chanzo.. maana tunaweza tukazama kuzungumzia ufisadi tukaacha mambo yanayogusa maisha ya watu wa kawaida kama haya. Naomba taarifa wa ndugu ili tumtafute Waziri anayehusika na Afya. kina Domokaya naomba mniandikie kwenye PM ni vituo gani hivyo mlivyoenda na kama kuna mtu ana contacts za waganga wakuu wake... haitoshi kulalamika tu ni lazima tufanye kitu.

ndugu yangu Mwanakijiji asante kwa kuonyesha kuguswa ha hii topic, mwanangu anapataga chanjo kwenye clinic moja ninaitwa FURAHA KWA PR. MASAWE na number yao ya simu ni hii +255 222 667 693, wewe piga na ulizia tu kama chanjo zimeshafika na utapata jibu zuri kuwa chanjo hakuna hata kwenye bohari kuu hawana kabisa..... leo hii nimetoka kupiga simu kuulizia na jibu nililopewa ni kwamba bado hazijaja na hawajui lini zitakuja,

Baadhi ya Hospital nilizotembelea kutafuta chanjo ni kama ifuatavyo:

1. Furaha clinic
2. Lugalo hosp. ya Jeshi.
3. Muhimbili.
4. Mnazi mmoja pale wanapotoa chanjo za kitaifa.
5. Gerezani hosp ya wilaya.
6. Kifuma.
na zingine nyingi nasikia hata huko mikoani chanjo zimekwisha kabisa, mimi nashangaa sana kikwete na wizara ya Afya wanafanya nini.
 
Bado wako kwenye kutalii nje ya nchi.
 
Poleni sana watanzania wenzangu hata mimi tatizo kama hilo nimesha kutana nalo na mtoto wangu hajapata chanjo ya miezi mitatu mpk sasa anafikisha miezi minne. Hii kweli ni hatari sijui tanzania inaelekea wapi.
 
Pesa za chanjo zipo, sema hazijapelekwa kwa wahitaji, kuna mahali zinavujia.
 
Sasa ni wakati wa kuamka, watanzania tukatae upuuzi huu njia ni kuungana pamoja na kuiondoa hali hii kwa kuwaoondoa madarakani.Napendekeza kwa kuanza tuwe na maandamano ya amani kuwaoomba wang'atuke !!
ukishakuwaondoa hawa utamuweka nani? ni vyema ukafikiria kabla ya kuwaondoa.washaondoka watatu kabla yake na hali haijawahi kubadilika. inabidi watanzania tutafute mbinu mpya sasa. tukaeni tufikiri.
 
Sasa hebu fikiria haya mambo yanafanyika Dar.Je kule kijijini kwetu chole samvula si ndiyo mauaji kabisa! Hebu viongozi wetu muwe na huruma jamani.Tunajua kuwa mnapenda hela na kutalii nchi za nje lakini..muoneeni huruma hawa watoto wachanga ambao ni malaika wa mungu wapate haki zao za kupatiwa chanjo.Magonjwa hutesa,huuma na huua hivyo mtu au kiongozi yeyote anazembea kupeleka madawa kwa wakati muafaka huyo naye anahesabiwa kama muuaji tu.
Wembe.
 
Hivi karibuni nimetokea kwenye safari ya kikazi from remote area ya Tanzania (Rukwa) na nimekuta hamna umeme, solar panel wameiba na chanjo zinahifadhiwa kwenye friji inayoendeshwa na mafuta ya taa. Wahudumu wamekubali kwamba haifanyi kazi nzuri wakati mwingine haifanyi kazi kabisa. kama kuexpire ni tayari! Sasa hata kama chanjo ipo itakuwa salama kweli?
Sekta ya Afya is in a crisis!
 
Nchi imewakaribisha ma NGO chungu nzima, wengi ambao walikwisha ahidi kutoa huduma ya chanjo vijijini.

Kila ninapoenda Bar usiku kunywa, huwa nakutana nao wengi tu wakijiachia, full bwax. Hawa watu wamekuja kuchanua na kustarehe huku wakilipiwa gharama za kila aina na nchi walizotoka na Serikali yetu yenyewe.

Hapa, sio serikali yetu peke yake inayokosea, bali ni kuzubaa kwetu sote kilicho sababisha hali hii iote tangia miaka iliopita.

JK, bila wasiwasi..ataiuza nchi yetu. Jamani ziwa la Natron inakuaje? Mwandosya ameikubali ombi la TATA kukinunua?
 
Philosopher,
Ukifika Wilayani utachoka NGOs zinaonekana to replace role of govt- maafisa wa wailaya hutumia up to 40% ya mda wau kuandiaka ripoti kwa hawa watu..na zipo tu kibao ni vurugu tupu! hakuna co-ordnation yaani kila NGO inajua zaidi!
Je tutafika?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom