Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa sugu wa figo kati ya 4,800 hadi 5,200 ambao wanahitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikizwa figo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
1615446416708.png

Serikali imelenga kuziwezesha Hospitali zote za Rufaa za Mikoa (26) nchini ili kuweza kuanzisha huduma za matibabu ya ugonjwa sugu wa figo ikiwemo usafishaji damu ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea Kitengo cha usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo (hemodialysis) katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Nyanda za Juu Kusini (MZRH), kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yanayofanyika hapo kesho ulimwenguni kote.

“Wizara tumeongeza huduma za Kibingwa katika Hospitali zetu ambapo kwa sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali zote za Rufaa za Kanda na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga – Bombo, zinatoa huduma ya usafishaji damu.

“Serikali imelenga kuziwezesha Hospitali zote za Rufaa za Mikoa (26) nchini ili ziweze kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa sugu wa figo ikiwemo usafishaji damu ifikapo mwaka 2025,” amebainisha Waziri

Dk. Gwajima amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa, asilimia 10 ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa sugu wa figo.

Amesema hapa nchini takwimu zinaonyesha kuwa, Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa sugu wa figo kati ya 4,800 hadi 5,200 ambao wanahitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikizwa figo.

“Kati ya hao wagonjwa 1000 wanapata huduma ya usafishaji wa damu kwa sasa na hadi kufikia Novemba, 2020 jumla ya wagonjwa 316 wamepandikizwa figo katika hospitali mbalimbali.

“Mathalani, hapa nchini jumla ya wagojwa 78 wamepandikizwa Figo na Madaktari wazawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (62) na Hospital ya Benjamin Mkapa (16) na waliobaki wamepandikizwa nchini India,”

Amebainisha kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Ishi Salama, na Ugonjwa wa Figo”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha ushirikishwaji wa mgonjwa wa figo, familia, jamii na marafiki wanaowahudumia waathirika wa ugonjwa sugu wa Figo kuhusu tiba na afya yake ili aweze kuishi salama na ugonjwa wa Figo.

Amesema viashiria vikuu vya ugonjwa wa Figo ni pamoja na, Shinikizo la juu la damu au ‘Hypertension’, Kisukari au ‘Diabetes’ na Maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa mkojo au ‘recurrent UTI’.

Chanzo: TBC
 
“Wizara tumeongeza huduma za Kibingwa katika Hospitali zetu ambapo kwa sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali zote za Rufaa za Kanda na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga – Bombo, zinatoa huduma ya usafishaji damu.

“Serikali imelenga kuziwezesha Hospitali zote za Rufaa za Mikoa (26) nchini ili ziweze kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa sugu wa figo ikiwemo usafishaji damu ifikapo mwaka 2025,” amebainisha Waziri

Dk. Gwajima amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa, asilimia 10 ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa sugu wa figo.

Nini chanzo cha haya maradhi, je ni zipi njia sahihi za kuyaepuka
 
Nini chanzo cha haya maradhi, je ni zipi njia sahihi za kuyaepuka
Dk Linda pia ni mratibu wa magonjwa ya figo wa Wizara ya Afya.
Alisema chanzo kikubwa cha magonjwa ya figo ni kisukari, shinikizo la juu la damu, homa ya ini, maambukizi ya Ukimwi na maambukizi ya magonjwa mengine ya bakteria hususani UTI.
 
Mitungi vp
Maana sisi wengine hatujuwi hatma yetu itakuwaje

Ova
 
Back
Top Bottom