#COVID19 Tanzania inajipima mabavu dhidi ya Covid-19; yupi atakuwa wa kwanza kusalimu amri?

Waliobuni hii biashara ya corona lazima watakua wanamuangalia rais wetu John Pombe Magufuli kwa jicho la husda sana.

Au nakosea ndugu yangu Sumu ?
Hapana unakosea sana katika hili, mimi namuunga mkono Rais kuondoa hofu katika jamii ila ni juu yetu kuwa waangalifu ugonjwa upo.

Halafu wanunuzi wa chanjo Tz wala sio walengwa kama tunaongelea biashara, nchi tajiri duniani wameanza au wameshanunua dawa in advance ndio wenye pesa nchi nyingi za Africa tutakuja kupewa bure tu.

Kumbuka chanjo za watoto zote ni bure kutoka UN hatulipi kitu na matokeo chanjo wa watoto sote tunajuwa faida yake. siasa pembeni corona ipo ndio maana unaona siku za karibuni raisi kila mara anaongelea hilo hatuna corona sababu anajuwa hofu iko.

Hawana sababu ya kutulenga sisi maana sio wanunuzi hata tungekubali corona ipo zaidi tungepata misaada na chanjo za bure.
 
Tatizo la Tanzania corona imefanywa kisiasa CCM wanasema corona hamna watu wasichukue tahadhari, chadema wanasema corona ipo watu wachukue tahadhari,

Hamna kitu kibaya Kama jambo serious lifanywe kisiasa.

HII ITATUCOST TANZANIA KIUCHUMI, NA VIFO KUONGEZEKA.

nashangaa mtu anasema corona hamna wakati huko hospital ma Dr wenyewe wanaogopa kukaa karibu na mgonjwa ukiwa kwenye folen mtu akikohoa anatengwa na kuhudumiwa haraka.

Akili za kuambiwa changanya na zako.
Corona ipo kila mtu ajiongeze mwenyewe kama kweli unapenda watu wako basi chukuwa tahadhari.

Siasa ina sehemu zake lakini sio katika mambo ya msingi kama haya, ndio maana mkuu kila mkutano analazimisha watu waamini hakuna hasa katka siku za karibuni ukiona mtu anatumia nguvu sana kukanusha kitu basi ujuwe kuna jambo.

Sawa sawa ukiona mtu anaapa sana miungu wote hajafanya basi tia shaka. Naunga mkono hoja yako.
 
Mimi nafikiri elimu itolewe .
Sio kila anayekufa kwa changamoto za upumuaji basi amekufa na Corona..
Hata nimonia pia usababisha changamoto za upumuaji
 
Nawashangaa sana wanaosubiria chanjo za Mabeberu ambazo hata Wananchi wake wanazitilia mashaka wakati sie tangu Mdudu kaanza tulielekezwa na Serikali na Bungeni jinsi ya kutumia tiba mbadala na zimeonesha mafanikio makubwa sana kwa uwezo wake Maulana
Tuliambiwa tutakufa tuokotwe mitaani kama kuku hadi leo kimya. Watanzania tuamke, COVID ni scam.
 
Muulizeni Diva, kakutana na "flue" mpya, isije ikawa mafua ya popo
t23092094ri04r049.PNG
 
Daktari unafahamu kuwa uko chini ya wizara ?
Madaktari ni frontliners sio waziri na wizara yake. Daktari anaposema Hali ni mbaya waziri ilitakiwa amsikilize , unachomaanisha ni kuwa Madaktari wake kimya hata Kama hali ni mbaya mahospitalini. Kwa kuwa wapo chini ya wizara ambayo kwa sababu za kisiasa imeamua kufunga masikio
Wengine hawakubali kupoteza haki zao kirahisi,
 
inawezekana au isiwezekane.amini tena nakuambia ikiwa mtoa mada wanataka watu wafe ilihali allah subhanatallah hajataka.jua halitakua.mapigo saba ya wana wa isreal yalikuja lakin yaliwasafisha wakibti tu na magonjwa na dhoruba ikiacha milango ya waisrael.
haikatalik kuwa hali ya ugonjwa imetamalak dunia mzima ila kusema watu fulan lazima wafe et kuwa tu hawakubal kuwa upo.sio sahihi.west huko kila precaution inachukuliwa lakin kila uchwao ni iddad inaongezeka.ombea taifa lako kheri
 
Kipimo tosha kuwa elimu tunayopata haiwapi Wasomi maarifa zaidi ya kufahamu jinsi ya kusolve quadratic equations.
 
ucheni unafiki na uongo, hakuna mtu aliyesema virusi vya corona ni kitu ca kufikirika..... nadhani Rais na watanzania tunaamini hii kitu ni real ndio maana tukaamua kumuachia Mungu maana yeye ndio mjuzi wa kila kitu.

Kuhusu chanjo najua serikali ILIWEKA MAMBO CLEAR KABISA KWAMBA HAINA MPANGO WA KUAGIZA HIZO CHANJO INSTEAD INAENDELEA NA UTAFIT WA LOCAL MEDICS,

Ahsante.
na ndio swala ambalo lina mantiki.kitu kipya kimekuja why uzarau dawa zako za asil.hiv unafikir wale jamaa wakizama wakatoka na mchanganyiko mkal zaid ya ule wa kwanza wa mitishamba ambao wakau design vizur unafikir sio dawa.? na dawa ni dawa tu kama pip ila tiba inatoka kwa allah subhanatallah.ila ni lazima utafute dawa ila unaikana dawa sio inayokuponyesha ispokuwa ni allah subhanataala ndio mponyaj.
 
Tuliambiwa tutakufa tuokotwe mitaani kama kuku hadi leo kimya. Watanzania tuamke, COVID ni scam.
Siamini kama kuna mwana JF mwenye level ya ujinga kama ya kwako. Endelea kuamini kwamba hii ni scam
 
Nisicho penda kwa wa-Tanzania wenyewe ni kukuza mambo haya bila hata kuona mgonjwa au vifo vya Corona, ni kweli ipo lakini bada haina nguvu sana kwetu waafrika, Malaria inaua kuliko lakini hatusemi,hapa nchini maneno ya Corona hayapo kwa uhalisia isipokua yapo ya kulenga kumlaumu Rais na serikali,yaani kila anaye sema habari kuhusu Corona anaelekeza lawama kwa uongozi.

Sawa, ugonjwa upo lakini kila anayeongea ukimuuliza alisha fiwa na ndugu au jirani,hakuna na anaanzaa kuongea maneno mengi kweli ili tu ashinde kwenye maongezi.
 
Binafsi nashukuru mataifa mengi ya Afrika kuwa silence japo kwa ukimya huo kuna ambao wanshindwa kukaa kimya wakiwa na hofu ya kukosa misaada.

Tanzania naona hawana wasiwasi, tajiri mwenzao China atawapa msaada wa dawa wenye riba nafuu, 'the day has come'
 
Back
Top Bottom