Tanzania inahitaji viongozi wanaofanya mabadiliko sio wanaofuata mabadiliko

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
Tanzania ni Nchi ambayo ina rasilimali nyingi za kutosha kabisa kuendesha watu wake ambao ni karibu milioni Arobaini na na Nne hivi na ikawa na maendeleo ya kutosha na kila kitu kikakaa katika mstari ambao uan mwelekeo wa kisasa kabisa.Tatizo kubwa la Tanzania ni kuwa na viongozi ambao wanajifikiria wao kwanza badala ya kuangalia Taifa zima kwa ujumla.Hapa tunaviongozi ambao wanaweza kula dili na Makampuni ya Nje yatuuzie kitu fulani madhalani Rada iliyoleta kashfa kubwa na kusababisha Nchi ya Tanzania kurudishiwa Tsh 29bilioni baada ya Serikali ya David Cameroon na aliyekua Waziri wa Misaada ya Maendeleo ya Africa Mama Clere Short alisema kuwa siku zote itabaki kuwa mradi huu wa ununuzi wa Rada ambao haukua na tija kwa Tanzania ni ufisadi na ni kufisidi Nchi.
Viongozi wa aina hii si viongozi bali ni madalali wanaweza kuuza hata nchi na wananchi tuliomo humu kwa maslahi yao bianafsi na bila hata kuona aibu.Zamani wakina Chifu Mangungo wa Msovero walisaini mikataba feki lakini hawa hatuwezi kuwalaumu kwani walikua hawajui kusoma wala kuandika kwa hiyo walilaghaiwa lakini hawa viongozi wa sasa huwezi kumshawishi mtu kwamba hawajui kusoma ns kuandika eti na hawajui kuwa wanachokifanya ni kitu kibaya la hasha wanajua fika ila ni watua ambao nia madalali tu hili ndilo jina lao kazi ambayo wanaifanya na kwa maana nzuri zaidi ni Mafisadi.
Tatizo kama la umeme la Tanzania sio kubwa kama linavyochukuliwa bali ni kwa kuwa hatuna viongozi bali watu wa misheni tauni na wao wanachangamkia fursa ya kuleta majenerata badala ya kuatatua tayizo kwa watanzania wote .Suala la umeme limekua tatizo kubwa toka enzi za kina Msabaha walipojiuzulu kwa kashfa iliyolihusisha shirika hilo lakini hakuna kilichaobadilika watu ndio walewale waliokuja kusababisha kina Lowasa kujiuzulu pia kwa kashfa nyingine ya Richmond.Ukiangalia mtiririko huu kwa makini utaona kwamba taifa hili halina mwelekeo dhabiti ni sawa na kusema tunaelekea kusini ilihali tunaelekea kaskazini.
Angalia jinsi ambavyo tunajua kucheza na maneno tujiulize Kilimo kwanza kinatofauti gani na Siasa ni kilimo hapa nataka tuangalie wakati akiwepo muasisi wa Taifa hili Mwalimu J.k.Nyerere na baada ya miaka hamsini tumeweza kutumia nyenzo gani za msingi .Angalia tena kilimo cha kufa na kupona nah iii ya sasa kilimo kwanza tofauti hapa ni maneno tu hawa watunga sera sijui kama nao huwa wanakua hawaendi pamoja na kiongozi mkuu yaania Rais.Lzima tufikie sehemu tujiulize kwamba ni nini ambacho kilifanya urudiaji wa kauli zenye maana ileile kwa miaka hamsini nab ado soko la mahindi likipatikana tunalinda mipaka ili mahindi yasiuzwe nje ya Nchi. Je hii sio nchi ya watu ambao wanapishana na sera zao wenyewe?au labda hatujui tunachokimaanisha?
Twende taratibu hapa Tanzania ni mtu basi angekua ni mtu wa makamo lakini kwa kuwa Tanzania ni Nchi basi utakuta kuwa tunazunguzua kitu kidogo tu na hapa ndipo pa kujiuliza kwamba tatizo ni nini ?je ni mazingira yetu tumeshindwa kuyatumia au ni kitu gani?Wanasema mtaka cha uvunguni sharti ainame na Nchi yetu inasemekana kwamba ikitoa Nchi kama Iraq na afganistani kwa kupenda vya uvunguni ni ya Tatu je hili ni tatizo la kisera au kiuongozi ?kama ni sera hatuna viongozi ambao wanaweza kutumia wataalamu hawa na kutunga sera makini ambazo zitabadilisha maisha ya mtanzania? Na kama ni tatizo ni viongozi je hatuoni kwamba umefika wakati viongozi waliopo wakalitafakari hili na kujivua gamba kabla ya umma haujatumia nguvu yake na kulivua gamba hilo ambalo ni mzigo mkubwa kwa serikaali?
Hawa viongozi tulionao je wanamawazo endelevu au huwa wao ni genge la watu ambao ni madalali wanaotaka kutumia dhamana tuliyowapa kwa kujinufaisha wenyewe na kutuacha sisi tukiwa maskini kam ilivyo kwa makampuni ya uchimabaji madini ambao watatuachia mashimo muda si mrefu.Hapa nimepata swali je madini yanayochimbwa sasa hivi yanatusaidia nini na sisi tunastahili nini kwenye hili?Haya ni mambo ya msingi ya kujiuliza .Kuna kisa kimoja cha Dalali ambaye aliitwa kwenye uuzaji wa kiwanja wakati kiwanja mwenyewe alikua anauza kwa shilingi milioni mbili dalali alikua anachukua milioni nane mara tatu zaidi sasa balozi akajiuliza kwamba ni nani alikua mmiliki wa kiwanja kile alipojibiwa akamwambia yule jamaa aliekuwa mmiliki usikubali na yule dalali akampigia simu mteja wake kwamba hawa watu wameghairisha kuuza kwani kuna tatizo lakifamilia hivyo kiwanja kile kikabaki.lakini hapa nataka tujifunze na sisi tusije kuwa tunafanyiwa kama mwenye kiwanja kile .
 
Mipango na wakaitekeleza kwa maslahi ya umma na sio matumbo yao na wenzao. Watumie rasilimali kwa uangalifu na sio kwa ubadhirifu. Na akijiona hamudu basi aachie nafasi mwenyewe bila ya kulazimishwa. Thats what we need for progress.
 
Hoja nzuri doctors..sorry doctorz..
Tatizo ninaloliona mimi ni utashi.. Ama uthubutu.. We lack that.. Wengi wa viongozi ni wachumia tumbo eidha kwa asili yao ndiyo maana wakakimbilia siasa au wamefanywa hivyo na mfumo wa siasa zetu za sasa..
Wanasiasa watendaji wapo,kwa bahati mbaya wanchangamanishwa na mfumo uliopo..wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa kadri ya uwezo walio nao,wanafungwa speed governor bila kupenda..Mpaka hapo tutakapoweza kuubadili mfumo,hakuna mabadiliko yoyote ya maana +ve kwa nchi yetu
Hilo ndiyo tatizo!
 
Back
Top Bottom