Tanzania inahitaji UKAWA sasa kuliko miaka ile ya nyuma

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,672
2,539
Huenda CCM ikadhani kuwa mchezo walioufanya mwaka huu katika uchaguzi ni kwa manufaa kwao tuu. Laa mimi sioni hivyo,bali ni wa manufaa kwa vyama vya upinzani vyote nchini.

CCM imejipambanua kuwa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu, ni nani alitarajia kuwa Mdee ange bebwa na CCM kutumika katika usaliti huu wa karibuni?

Ni nani aliye dhani kuwa Mrema ,Hamad Rashid, Lipumba na Mbatia watapigwa chini na vyama vyao kubakia vinalia lia kama chadema na ACT?

Hivi ndivyo CCM walivyo na sura za kinyonga. Hukutumia tuu wakati wa haja yao na kukutupa pipani wakisha kutumia. Kuna wakati hata Chadema wali ituhumu CUF ya wakati ule wa maridhiano na serikali ya Umoja wa kitaifa kuwa imekuwa CCM B. Aidha kulikuwa na wakati CUF imeituhumu Chadema kuwa CCM B lakini mwaka huu alituhumiwa Mbatia na Mrema Kuwa CCM B ,alimuradi mwisho wake wote tumetiwa kwenye tenga moja tuko sokoni tunanadishwa kama kuku wa kienyeji.

Hali ya mwaka huu imetukutanisha wapinzani wote tukiwa hali sawa tumepigika kwa kichapo cha CCM.
H
apa ndipo ninapoanzia maudhui yangu.
Kwa vile sasa tumejifunza vya kutosha mwenendo wa CCM nchini na mtindo wake
Kwa vile hakuna aliyefanikiwa kwa kushirikiana na CCM kwa namna yoyote ile,
Kwa vile hakuna chama kilichosalimika na maafa ya mwaka huu ya uchaguzi na engua engua na piga piga na kamata kamata .
Kwa vile Jumuia ya Kimataifa inaonesha kutuunga mkono katika suala la kudai demokrasia nchinikwetu iliyo sawa.
kwa vile CCM imepora hata maeneo ambayo yakuwa ngome za CUF, ACT, Chadema na Nccr -Mageuzi bila huruma,
Inaonesha vyama vyote vya upinzani hakuna kilicho salama mbele ya Haramia CCM, hata ukijipendekeza CCM inakutosa.
Hivyo basi ndipo nilipoona nije na mada hii

TANZANIA INAHITAJIA UKAWA SASA KULIKO MIAKA ILE YA NYUMA.​

Yafaa sana sana sasa VYAMA VYA UPINZANI MAKINI tuache kuhasimiana kwetu, tushikane mikono kwa umoja wetu ili kuli ngurumisha suala la katiba mpya na Tume iliyo huru ncini kwa sauti kuu na kinywa kipana.Yafa tuanze mapema tuu by January 2021 tuanze kuimba wimbo huu,sio kungoja hadi 2024.

Tukumbuke Usemi wa Mzee Mtikila enzi zake alisema kuviambia vyama vya upinzani

''TUSIKIMBILIA KUSHIRIKI CHAGUZI KWA KATIBA HII,
BORA TUCHELEWE NA TUDAINI KATIBA MPYA KWANZA NA TUME HURU
KULIKO KUSHIRIKI CHAGUZI LAGHAI''

Tutakuja kujuta huko mbele ,kwani kataiba hii inaipa chama Tawala mamlaka ya kufanya wapendavyo bila ya kulaumiwa.
Mwaka huu tumeona ukweli wa maneno ya hayati Mzee Mtikila.​

KARIBUNI KWA MICHANGO YENU NA WAPI PA KUANZIA.
 
Hatutaki vyama vingi,

Upinzani unachelewesha maendeleo!

Tunewapiga chini wabunge wote wa upinzani,

Ndani ya mwezi mmoja Toka awamu ya tano imeapishwa ,tumeanza kuona juona maendeleo kwa Kasi, maisha yetu wanyonge tameboreshwa,huduma zote za msingi na mzunguko wa fedha umerejea kuliko hata enzi za JK.
 
Siyo vyama vya upinzani vya aina hii tulivyonavyo vinavyopinga kila kitu! Unakwenda Benki ya Dunia kusema Tanzania isipewe msaada kwa kuwa inataka waliopata mimba wasirudi shule za Serikali badala yake watafute shule mbadala, kuchongea kwa mabeberu na kuomba Nchi ipate matatizo ili kupata agenda, kunyanyasa wanawake hapana!
 
True Hadi wanafunzi wanakaa hostel 5 star hotel.
 
Siyo vyama vya upinzani vya aina hii tulivyonavyo vinavyopinga kila kitu! Unakwenda Benki ya Dunia kusema Tanzania isipewe msaada kwa kuwa inataka waliopata mimba wasirudi shule za Serikali badala yake watafute shule mbadala, kuchongea kwa mabeberu na kuomba Nchi ipate matatizo ili kupata agenda, kunyanyasa wanawake hapana!
Dona kantri haitaji misaada
 
Kwa hiyo Tanzania tumeshakuwa 'Doner country', tunajitegemea wenyewe?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom