Tanzania inahitaji tume ya ukweli na maridhiano ya kitaifa

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Watanzania tunahitaji kama taifa au nchi kuwa na tume ya ukweli na maridhiano ya kitaifa na siyo CCM na CHADEMA.

Tume ya Ukweli na Maridhiano ya kitaifa itahusisha wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, dini, rangi na jinsia tofauti na haya maridiano ya CCM na CHADEMA.

Kuna makundi, taasisi na watu mbalimbali waliumizwa na serikali kwa sasa wanaugulia maumivu na wengine wamepoteza ndugu na jamaa zao.

Kinachotakiwa kwa sasa Rais Samia kwa dhati ya moyo wake kuunda jopo la watu mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa dini zote, wanasheria n.k, ili kusimamia Tume ya Ukweli na Maridhiano ya taifa kwa Watanzania wote na wote waliyoumizwa wapite mbele ya hiyo Tume ya Ukweli na Maridhiano kujieleza ili mwisho wa siku Watanzania turidhiane na kuanza upya na kurekebisha mifumo yetu iliyopelekea wananchi kuumizwa na kuteswa au kupotezwa na kuuawa.

Ncgi ya Afrika ya Kusini kupitia aliyekuwa Rais wake Hayati Nelson Mandela alimteua Hayati Askofu Desmond Tutu Kuongoza jopo la watu mbalimbali kusimamia Tume ya Ukweli na Maridhiano na mwisho wa siku wote walisameheana.

Maridhiano yanayoendelea ya CCM na CHADEMA ni ya sehemu ndogo sana lakini Tume ya Ukweli na Maridhiano itahusisha Watanzania wote na taifa zima na mambo mengi yatafichuka na kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
 
Watanzania Tunahitaji kama TAIFA au NCHI kuwa na TUME ya UKWELI na MARIDHIANO ya KITAIFA na SIO CCM na CHADEMA.

TUME ya UKWELI na MARIDHIANO ya KITAIFA itahusisha Wananchi Wote bila Kujali ITIKADI zao za KISIASA DINI RANGI na JINSIA tofauti na haya MARIDIANO ya CCM na CHADEMA.

Kuna MAKUNDI TAASISI na Watu mbalimbali WALIUMIZWA na SERIKALI kwa Sasa Wanaugulia MAUMIVU na Wengine WAMEWAPOTEZA NDUGU na JAMAA zao.

Kinachotakiwa kwa Sasa MH.RAIS SAMIA kwa DHATI ya MOYO wake KUUNDA JOPO la Watu mbalimbali Wakiongozwa na VIONGOZI wa DINI ZOTE WANASHERIA n.k ili KUSIMAMIA TUME ya UKWELI na MARIDHIANO ya TAIFA kwa WATANZANIA wote na Wote WALIOUMIZWA wapite mbele ya hiyo TUME ya UKWELI na MARIDHIANO kujieleza ili Mwisho wa Siku Watanzania TURIDHIANE na Kuanza Upya na Kurekebisha MIFUMO yetu iliyopelekea WANANCHI kuumizwa na KUTESWA au KUPOTEZWA na KUUAWA.

NCHI ya AFRIKA ya KUSINI kupitia Aliyekuwa RAIS wake Hayati NELSON MANDELA alimteua Hayati ASKOFU Desmond TUTU Kuongoza JOPO la Watu mbalimbali Kusimamia TUME ya UKWELI na MARIDHIANO na Mwisho wa SIKU WOTE walisameheana.

MARIDHIANO yanayoendelea ya CCM na CHADEMA ni ya sehemu ndogo sana lakini TUME ya UKWELI na MARIDHIANO itahusisha WATANZANIA WOTE na TAIFA ZIMA na Mambo Mengi Yatafichuka na Kutafutiwa UFUMBUZI wa KUDUMU.

Ushapata barabara za kutosha, Hospital za kutosha

Mishahara na Ajira za kutosha ?
 
Back
Top Bottom