Tanzania inahitaji political reform

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Tangu mwaka tisini na mbili wakati nyerere akiwa hai aliona siasa ya ujamaa imefeli na aliona sisi sio kisiwa tusalimike akaamuru mfumo wa vyama vingi urusiwe kwa mara ya kwanza baada ya ule wa wakati wa kupigania uhuru kufutwa rasmi baada ya kuwa huru.

Namuona rais wetu john magufuli akijitahidi kujaribu kuvaa kiatu alichoona nyerere hakimuenei tangu miaka ya tisini akaamua kung'atuka madarakani akijua yeye ni mjamaa kweli kweli lakini ujamaa umefeli maeneo mengi duniani ndipo akaona namna nzuri ya kuendana na wakati ni kurusu upepo wa wakati kwa kuwa wakati wa ujamaa umepita na haurudi tena.

Ujamaa una falsafa yake na alama zake moja ni chama dola, mfumo wa chama kimoja ambapo chama ni kubwa kuliko serikali, mifumo ya uzalishaji mali unamilikiwa na serikali mfano ardhi, mabenki na makampuni makubwa kama ya mafuta, umeme, pia biashara inongozwa na era kutoka serikalini na nguvu ya soko. mambo mengi ni amri kutoka juu hairusiwi kukosoa mkuu wa nchi yeye ni mfalme. sasa mimi naona mkulu wetu anataka tumuone kama nyerere lakini mimi nadhani angetengeneza mfumo wake mpya kulingana na wakati huu tungemuona kama nyerere wa pili lakini kujaribu kufuata falasa zilizofeli na kupitwa na wakati matokeo yake ni mashambulizi anakutana nayo kila kona kwa kuwa kwa sasa huwezi kudhibiti watu kwa sababu ya mitandao ya ninternet na dunia invyofanya kazi kwa hiyo anaweza kushangaa kwa nini anashambuliwa hivi wakati anafanya mazuri kumbe anasahau jambo moja kubwa uhuru wa habari na uwazi katika kuongoza serikali badala ya kufanya watu wasiweze kuhoji wawe wametulia tuu wakati wasomi ni wengi sana kwa sasa. Aliyesoma ni vigumu sana kumnyamazisha kwa kuwa anaelewa.

Kama anataka kuwa kama nyerere abuni mfumo mpya wa siasa na si kufuata ujamaa wa nyerere kwenye karne ya ishirini na maoja. Unatakiwa ujamaaa wa kisasa unaokwenda sambamba na ubepari ili watu wawe na uwanja mkubwa wa kufanya uchaguzi wa namna ya kupambana na umaskini(multiple choice nyingi) kuanzia mfumo wa siasa mpaka kwenye mfumo wa biashara na akumbuke kilimuondoa muamar Gadaffi wa Libya wala sio kwamba watu hawatendewi haki na walifanyiwa mambo mengi mazuri lakini jambo moja tu ya uhuru wa habari na kunyamazisha watu ndo ilimgharimu.

Wala asishangae kupata mashambulizi kutoka nje kupitia watanzania wenzetu kuungana na wale wenye nia mbaya na nchi yetu ndo ulimwengu wa kibepari. Ubepari ni uwanja wa wazi wenye kila mazuri ma mbaya mengi kama unakumbuka uwanja wenye mbigiri alafu menchi inatakiwa kuchezwa hapo sharti likiwa ni kucheza peku ndo ubepari hauna huruma huruma wa kubembelezana mbwa mwenye nguvu ndo atabaki na mfupa.

Mimi ushauri wangu ni kwamba rais wetu unafanya mambo mengi mazuri kwa moyo wako wote ila tegemea mashambilizi mengi sana kutoka nje watanzania wakiuungana na watu ambao hawitakii mema nchi yetu. Fanya kila kitu kwa kiasi kwa kuwa ulimwengu wa leo hakuna ujamaa kuna mixture ya mambo mazuri ya ubepari na mazuri ya ujamaa alafu yanakwenda kwa pamoja. Ukitaka kuelewa vizuri usome kwa deng jeaping (samahani kama nimekosea jina lake) rais wa china aliyemfuata mao tse tung alibadili kabisa sura ya china alichonga mfumo mpya wa kiuchumi ambao ulitoa wachina kwenye umaskini wa kutopea mpaka ikawa super power.

Huo ndo ushauri wangu wadau mnaweza kuongeza
 
maganjwa,
Tanzania sasa hivi haifuati ujamaa. Ujamaa ulishakufa. Umeandika kitu ambacho hakipo. Tatizo lililopo sasa hivi Tanzania ni kuwabadilisha watu waliokuwa wanaamini kuwa mafanikio ya maisha yanaletwa kwa njia ya mkato na siyo kufanya kazi sana na kujibana kimatumizi. Ku-change mindset za watu wavivu ni vita kali sana. Ndicho kinachotokea hapa.
 
Tanzania sasa hivi haifuati ujamaa. Ujamaa ulishakufa. Umeandika kitu ambacho hakipo. Tatizo lililopo sasa hivi Tanzania ni kuwabadilisha watu waliokuwa wanaamini kuwa mafanikio ya maisha yanaletwa kwa njia ya mkato na siyo kufanya kazi sana na kujibana kimatumizi. Ku-change mindset za watu wavivu ni vita kali sana. Ndicho kinachotokea hapa.
jiwe lazima akwame kwa sababu anaishi karne iliyopita akidhani yuko karne mpya.akuina zitto wanaposema tunatawaliwa na washamba hawajakosea
 
jiwe lazima akwame kwa sababu anaishi karne iliyopita akidhani yuko karne mpya.akuina zitto wanaposema tunatawaliwa na washamba hawajakosea
Kiujumla rais Magufuli ni rais mzuri japo kuna mambo hayako sawa. Hao kina Zitto ni watu wa ma-deal na wasikudanganye ni viongozi. Kama kuhimiza kufanya kazi na kuacha uvivu ni ''kuishi karne iliyopita'' nakuhurumia! Najua watanzania wengi huwa wanadanganyika na viongozi wasanii...
 
Back
Top Bottom