Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Watanzania kwa umoja wetu tukatae viongozi wetu wanapotaka kutupeleka.
Madhara ya ubaguzi,chuki na hasira kali vinavyooteshwa na kupaliliwa na viongozi wetu ni hatari mno kwetu na hatari pia kwa mustakabali wetu kama taifa.
Bahati mbaya sana Rais Magufuli anaamini vitendo vya kibabe na vya kukomoa wapinzani ndivyo vitakavyoiunganisha CCM.
Amejenga spirit na kujiamini kwa viongozi wake waandamizi kukanyaga shingo za wapinzani kila nafasi inapojitokeza.
There is a sadistic heart and spirit that fight so much to establish itself.
Bahati nzuri ni kuwa, Watanzania hatuko hivyo.
Nenda popote duniani na ukisema wewe ni mtanzania, mwenyeji wako atatabasamu, atafurahi. Atafurahi kwasababu tunasifika kwa upendo, ukarimu na mshikamano.
Angalia wageni wanaotutembelea wanavyopenda kucheza na wenetu. Ona tu jinsi wanavyotusalimia kwa bashasha!
Kule Kilimanjaro wakija kupanda mlima wanafurahi sana kuimba na kuweka kumbukumbu ya ile nyimbo yetu nzuri ni- HAKUNA MATATA
Yes! Watanzania hatuna matata.
1. Ukila pesa za tetemeko tutaguna kichinichini, mh! Hii roho ya wapi hii?
2. Ukikataza watu kuchangia wapendwa wao rambirambi, tutaambiana, ' huyu ana laana huyu'.
3. Ukiwatukana wanafunzi kwaajili ya cheo chako, ukawaita vilaz.a, ukawanyanyasa na kuwafukuza shule, tutasema 'labda huyu sio mzazi au labda kiuno chake hakina uzazi'.
4. Ukiteka watu na kuwapoteza, tunashangaa! Ni mageni mno kwetu.
Orodha ni ndefu ndugu zangu, kuanzia Lema kung'ang'aniwa jela kinyume cha sheria mpaka Halima Mdee na Ester Bulaya kufukuzwa bungeni kwa mwaka mzima.
Sadistic heart!
Sadist ni mtu anaefurahi akiona mwingine anaumia.
Ndugu zangu tusiilee hii roho inayomea kwa kasi katika taifa letu.
Kama tulikosea kumpa mchawi mwenetu 2015 ili atulelee alafu ameamua kumfundisha uchawi basi tujirekebishe 2020.
Ila leo tuzuie hii roho chafu na tuipinge kwa uhai wetu ikibidi.
Kama Hitler angezuiwa pale Munich ambako alikamatwa basi vita kuu ya pili ya dunia, vifo, uharibifu wa mali na mateso yaliyofuata vingeweza kuepukwa kirahisi.
Kwenye moja ya picha za Hitler wanasema, sababu pekee kwa uovu kutamalaki ni mtu mwema kukaa kimya!
Watanzania tusikae kimya, sisi ni wema na hii roho si yetu!
Watu wanaweza kwenda mahakamani na wakapigwa danadana ila chuki itakuwepo na hasira itazidi.
Watu wanaweza kuuliza na wakadhihakiwa na chuki ikazidi.
Wachache tutaonyesha hasira zetu na tutadhibitiwa kwa kuwekwa jela ila chuki haitaondoka.
Ila siku kikombe cha chuki, kikombe cha hasira ,kikombe cha ubaguzi kikijaa, tutaipoteza Tanzania tunayoijua na kuipenda.