Tanzania inahitaji 'Kinjekitile Ngwale' wa karne hii

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Habari wanajamvi!

Mambo yanayo endelea Nchini yamewakera watanzania kupita maelezo. Wamekereka na kukereka vibaya mno.Awamu ya tano ndio imetia fora. Nitafafanua na mwishoni nitaeleza ni kwanini Tanzania inahitaji Kinjekitile Ngwale wa kizazi hiki.

Mapema 2016 maelfu ya wakazi walibomolewa nyumba zao bila kufuata taratibu na sheria. Hata zilizo wekewa stop order ya mahakama zilibomolewa. Hakuna kufidiwa kisa inasadikika hawakumchagua KIM JONG UN.

Wafanyakazi hawajawahi kupandishiwa madaraja na mishahara toka 2015! KIM JONG UN anasema watamfanya nini?

Wahitimu wa vyuo vikuu hawajaajiriwa toka 2016 mpaka leo hii pamoja na kuwapunguza wafanyakazi zaidi ya 17,000.Vijana wapo mitaani wanahangaika.

TAKUKURU wanakera Wananchi. Bosi wao ndio kabusaaa! Kila siku amevaa sare za Jeshi la Wananchi.Hivi angekuwa Daktari kila siku angetembea na kipima pressure shingoni? Mbaya zaidi sasa anajifanya yeye ndio CAG, POLICE, in short wanawakera wananchi kupindukia.

Kuna huyu mtumia fedha za umma kuhonga wanasiasa wa upinzani. Anatumia fedha nyingi kununua watu dhaifu sana. Wamediriki hata kuwarudishia ubunge hata watu waliokataa ubunge kwa hiyari zao.

Kuna huyu aliye vunja Katiba mara 15 wakati aliapa kuilinda na kuihifadhi kwa moyo wake wote na akili zake zote!

Teuzi zote za Kim Jong Un zinazingatia vigezo vipya kabisa. Je, wewe ni msukuma? Je, wewe unatoka shinyaga, Geita? Simiyu? Au atleast Mara? Ukikidhi vigezo hivyo basi wewe unateuliwa.

Tume ya uchaguzi imegeuka tume elekezwa. Kifupi watanzania wamekerwa na mengi volumes and volumes!

Wanahitaji Kinjekitile Ngwale awahakikishie kuwa wakilianzisha Polisi wote watapata changamoto ya kupumua na hivyo watashinda pambano. Ustaarabu wa kubadilisha viongozi kupitia sanduku la kura umeshindikana.
 
Hizi porojo muwe mbadanganyana ufipa
Kwanza Mimi siyo wa ufipani ingawa Sera zao zinanikosha sana.
Pili, lipi siyo la kweli kuhusu awamu hii kati ya hayo niliyo bainisha?

Nenda jibu hoja baada ya hoja ndio nitakuelewa.
 
Yote ni porojo na uzushi

Siwezi kujibu uzushi
Kwanza Mimi siyo wa ufipani ingawa Sera zao zinanikosha sana.
Pili, lipi siyo la kweli kuhusu awamu hii kati ya hayo niliyo bainisha?

Nenda jibu hoja baada ya hoja ndio nitakuelewa.
 
Back
Top Bottom