Tanzania inahitaji elimu kwa kweli, yaani mhubiri ambaye humshauri hata Rais, anasema Corona inaletwa na 5G

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,744
48,385
Ukiona kauli ambazo Watanzania huwa nazo humu JF utajua kweli hawa ndugu zetu elimu yao ina mapungufu makubwa sana, hebu waza huyu mchungaji maarufu sana Tanzania yote, anategemewa na maelfu ya Wabongo, na mara moja moja hutinga ikulu kwenda kushauri (kama kwenye hii picha), ndiye anadiriki tena kwa akili zake mwenyewe kusema Corona inaletwa na teknolojia ya 5G.

Huwa sishangai nikiwaona Watz humu na kauli zao, maana hapa ndio elimu yao ilikofikia, hata wataalam wote kimya wanapoambiwa Corona ni 'kaugonjwa'.

michuzijr_60972817_148512542951570_1144757953477379838_n.jpg

Are you sure Ngwajima anamshauri Raisi? Sio kila anayekutana na Raisi ndie mshauri wake.

Rais ni taasisi, hukutani naye kishkaji, labda umfuate wakati amekwenda Chato kwake, lakini appointment za ikulu full ofisi, bendera na misuti uende kupiga soga za vijiweni naye? Kawaida lazima upitie hatua nyingi sana kabla ukalie kwenye hiki kiti naye, ajenda yako ifahamike kwa undani, upana na urefu, tija yake itathminiwe, usalama wa taifa wakukague mpaka historia yako na uwezo wako.

michuzijr_60972817_148512542951570_1144757953477379838_n.jpg
 
Punguza pr zako wewe,
Kaenda ikulu mara ngapi?
Unaulizwa kitu simple unandika vitu ambavyo havipo,
Ni mshahuri wa rais toka lini?
 
Vita na gwajima utaiweza?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Hehehe! Wala siwezi kujaribu hata kumnyooshea kidole, mtu ambaye anaingia mpaka ikulu kushauri yaani hauwezi ukapambana naye.
Hehehe nakumbuka video zake kwenye mitandao anavyojua kukata mauno kwa wanawake.
Huyo saizi yake ni Bashite, nakumbuka walipelekana hadi raha.....wote wanasklizwa na mkulu.
 
Hiyo ya corona kuletwa na 5G mbona ni agenda worldwide... Hata nduguzo wanaiongelea.

Kote inazungumzwa na watu wa vijiweni lakini sio kitu cha kutangazwa kwa umma, kwa maelfu ya watu, tena na mtu ambaye ni maarufu na ana access hadi ikulu. Halafu amekusanya watu kanisani, maelfu akiwaambia pumba kama hizo, hamna tahadhari yoyote, watu bado mnakusanyika.
 
Ona kinacho fanyika kwa mabwana zenu kule,
Si huwa hadi kitu kifanyike kwa mabwana zenu ndio mzinduke,
Utanikwepa ila nitakufata nikudunge huko huko.

Na hao mabwana zetu wanaosema hivyo? Nenda YouTube utawasikia na kuwaona.

Tatizo la ndugu zetu Wakenya ni kujifanya mnaelimu wakati hakuna kitu mnawasujudia sana wazungu kiasi mnajitoa hata ubinadamu wenu.

Miaka ya nyuma nilifanyakazi hapo Nairobi na nilikuwa naishi Westland karibu na Saliti Centre nilikuwa naona jinsi gani wakenya weusi wanavyonyanyaswa na weupe wakishirikiana na wakenya wachache ilikuwa inaniumiza sana.

Kuna uwezekano wewe ni kati ya wakenya wachache unaokula matunda ya Kenya ila waliowengi wanapata shida sana huko mitaani.

Kwahiyo mkuu Watz wengi tunajitambua sana pamoja na kuwa bado tuko nyuma kimaendeleo lakini sisi tunajali UTU kwanza!! Ndiyo maana hata sasa hivi tunapambana na corona kiutu zaidi siyo nyinyi hapo kutandikana kama wanyama na wanaopigwa ni wakenya weusi sioni weupe wakipigwa na nina uhakika ukienda Westland utakuta weupe wanaendelea kula nchi tu ya wakenya.
 
Ona kinacho fanyika kwa mabwana zenu kule,
Si huwa hadi kitu kifanyike kwa mabwana zenu ndio mzinduke,
Utanikwepa ila nitakufata nikudunge huko huko.

Mkuu MPE tu vidonge amevitaka mwenyewe hata mimi ninavyo vidonge kibao vya video clip lakini namsubiria kidogo nimpe ameze ili apone ugonjwa wake wa slavery mentality.
 
Kote inazungumzwa na watu wa vijiweni lakini sio kitu cha kutangazwa kwa umma, kwa maelfu ya watu, tena na mtu ambaye ni maarufu na ana access hadi ikulu. Halafu amekusanya watu kanisani, maelfu akiwaambia pumba kama hizo, hamna tahadhari yoyote, watu bado mnakusanyika.
Huyo ni msemaji wa waumini wake na wala si msemaji wa watz... Ukiamua kumsikiliza poa, ila mimi huwa simtilii maanani.
 
Mkuu MPE tu vidonge amevitaka mwenyewe hats mimi ninavyo vidonge kibao vya video clip lakini namsubiria kidogo nimpe ameze ili apone ugonjwa wake wa slavery mentality.
Atajuta kufungua huu uzi.
 
He might be right,sema labda namna ya kuwasilisha kwa njia rahisi imekua ngumu, tafuta noti ya Euro 20 , uione ikoje, ina nini na nini

Hii symbol ya corona ipo
chini yake ni minara ya 5G

je ni coincidence au kuna ujumbe nyuma ya pazia? una google...uliza huko
 
Na hao mabwana zetu wanaosema hivyo? Nenda YouTube utawasikia na kuwaona. Tatizo la ndugu zetu Wakenya ni kujifanya mnaelimu wakati hakuna kitu mnawasujudia sana wazungu kiasi mnajitoa hata ubinadamu wenu. Miaka ya nyuma nilifanyakazi hapo Nairobi na nilikuwa naishi Westland karibu na Saliti Centre nilikuwa naona jinsi gani wakenya weusi wanavyonyanyaswa na weupe wakishirikiana na wakenya wachache ilikuwa inaniumiza sana. Kuna uwezekano wewe ni kati ya wakenya wachache unaokula matunda ya Kenya ila waliowengi wanapata shida sana huko mitaani. Kwahiyo mkuu Watz wengi tunajitambua sana pamoja na kuwa bado tuko nyuma kimaendeleo lakini sisi tunajari UTU kwanza!! Ndiyo maana hata sasa hivi tunapambana na corona kiutu zaidi siyo nyinyi hapo kutandikana kama wanyama na wanapigwa ni wakenya weusi sioni weupe akipigwa na uhakika ukienda Westland utakuta weusi wanaendelea kula nchi tu ya wakenya.

Hizi insha sijui unaandika za nini, nimesema wengi wanaongea kuhusu 5G ni korona kwenye vijiweni, ila sio kwa mtu anayetegemewa kwenda kushauri ikulu, ndio maana mnaita Corona kaugonjwa.
Halafu nimeona kumbe ni kitu kimewahi kufunguliwa uzi
Upotoshaji uliopo kati ya uhusiano wa teknolojia ya 5G na corona - JamiiForums
 
Ukiona kauli ambazo Watanzania huwa nazo humu JF utajua kweli hawa ndugu zetu elimu yao ina mapungufu makubwa sana, hebu waza huyu mchungaji maarufu sana Tanzania yote, anategemewa na maelfu ya Wabongo, na mara moja moja hutinga ikulu kwenda kushauri (kama kwenye hii picha), ndiye anadiriki tena kwa akili zake mwenyewe kusema Corona inaletwa na teknolojia ya 5G.

Huwa sishangai nikiwaona Watz humu na kauli zao, maana hapa ndio elimu yao ilikofikia, hata wataalam wote kimya wanapoambiwa Corona ni 'kaugonjwa'.

michuzijr_60972817_148512542951570_1144757953477379838_n.jpg

hivi kwa nini kwenye awamu hii occupants wengi wa nyumba muhimu ni psychiatric cases - makanisa na maboma (wilaya, mikoa hadi taifa)???
 
He might be right,sema labda namna ya kuwasilisha kwa njia rahisi imekua ngumu, tafuta noti ya Euro 20 , uione ikoje, ina nini na nini

Hii symbol ya corona ipo
chini yake ni minara ya 5G

je ni coincidence au kuna ujumbe nyuma ya pazia? una google...uliza huko

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna jamaa ametole maelezo vizuri sana bora mkasoma uzi wake mtaelewa, hamna kitu kama hicho na haiwezekani, uliza mtaalam yeyote, hebu fuata uzi wa huyu jamaa huku
Upotoshaji uliopo kati ya uhusiano wa teknolojia ya 5G na corona - JamiiForums

Hivi karibuni kumetokea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ugonjwa wa corona na Teknolojia ya 5G.Miongoni mwa hoja zinazotolewa ni kama zifuatazo:-

1. Kuwa karibu na 5G kuna sababisha corona, ndio maana nchi zilizo athirika zaidi ni zile zilizoanza kutumia teknolojia hii.

2. Teknolojia ya 5G inatoa miaonzi ambayo inasababisha kansa, na kuharibu kabisa vinasaba (DNA) vya binadamu.

3. Kuna dhana kuwa Corona imeanza China kutokana na China kuwa ya kwanza kujenga minara ipatayo 100,000 kwa ajili ya 5G.

4. Ipo dhana kuwa kinga dhidi ya corona itakuwa na kipandikizi cha kielekroniki (micro chip) kitakachopandikizwa kwenye mwili wa binadamu kuzuia athari za 5G. Ndio maana Bill Gate anadhamini utengenezaji wa dawa na kinga ili zisambazwe kwenye nchi maskini kwa malengo ya kiusalama.

Dhana zote hizi ni uongo, na ukweli kuhusu mfumo wa mawasiliano wa 5G ni unapatikana katika sayansi ya mionzi pamoja na ile ya mawasiliano kama ifuatavyo:-

Mfumo wa 5G kama ilivyo mifumo mingine kabla yake, mfano 2G, 3G, na 4G ambao mpaka sasa hivi unatumia/kusafiri kwa njia ya mawimbi ya redio (radio waves) ambayo ni aina moja wapo ya mionzi isiyo ainishi (non ionizing radiation) kama ilivyo katika spectra ya mionzi (electromagnetic spectrum).Mfano wa mionzi iliyo katika kundi hili la mionzi isiyo ainishi ni ile inayotumika katika microwave, ile ya jua (ultraviolet) nk.

Mionzi ainishi ambayo inaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu ni ile ya x-ray, alpha, betta, gamma ray na neutron na ile ya ultra-violet light ambayo ipo mwisho wa spectra ya mionzi (electromagnetic spectrum). Mionzi inayotokana na 5G haipo katika kundi hili.

Kwa kuwa mionzi inayotokana na 5G sio ainishi, ni wazi kuwa mionzi hii haiwezi kusababisha madhara ya cancer, kubadili kinasaba au kusababisha matatizo ya mifumo ya kupumua au yanayofana na hayo ndani ya mwili wa binadamu.

Madhara yanayoweza kupatikana katika teknolojia ya 5G ni kama yale yanayoweza kupatikana katika teknolojia ya 2G, 3G, na 4G, ambayo pia yanaweza kupatikana katika microwaves, ultraviolet ambayo ni kuongeza joto la seli.

Mfano ukiongea na simu kwa muda mrefu unapata maumivu kwani seli za sehemu za sikio ni laini. Vivyo hivyo tunashauriwa kutopakata laptop ili joto linaloongezeka kutokana na kupakata laptop lisiathiri sehemu za uzazi ambazo seli zake ni laini na ni rahisi kuathiriwa na joto.

Binafsi ninaweza kutoa mjumuisho ufuatao katika hili:-

Moja kuna upotoshaji unaofanyika kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu mionzi na corona, upotoshaji huu unaweza kuwa na madhara ya kiafya kwa watu kutokuchukua tahadhari stahiki kwa ugonjwa huu wa corona na kuongeza hofu ambayo haipo.

Pili, upotoshaji huu unalenga pia kujipatia kipato kwa wale wanaotafuta idadi kubwa ya watu wanaosoma makala zao katika mitandao ya kijamii.

Tatu, upotoshaji huu unaweza kuwa unafanywa na mataifa makubwa kama Marekani na washirika wake ambayo yanahofu na China kwenye Teknolojia ya 5G.

Vile vile upotoshaji huu unaweza kuwa na athari za kuhofia Teknolojia ya 5G ambayo ndio dunia inapoelekea na hivyo kuwabakisha watu nyuma.
 
hivi kwa nini kwenye awamu hii occupants wengi wa nyumba muhimu ni psychiatric cases - makanisa na maboma (wilaya, mikoa hadi taifa)???

Inasikitisha sana kwa kweli.....japo yote haya yalitabiriwa.
 
Inasikitisha sana kwa kweli.....japo yote haya yalitabiriwa.
Wewe umezidi kutapatapa, huyu huyu alipokua anapambana na Makonda ulikua unamtetea na kumshambulia Makonda, baadae huyu huyu aliposambaza picha za ngono mitandaoni, POLISI wakamtetea, wewe ukaikadhifu POLISI kwa kumtetea wakati ni kweli ile video inaonyesha ni yeye.

Pamoja na kuamini kwamba huyu jamaa ni mpumbavu, Leo unamuhusisha na watanzania, hii ni dalili ya kwamba unapoteza dira na kuzidi kudhihirisha uwezo wako mdogo wa kujenga hoja.

Sikutegemea tena kama ungemchukulia Gwajima kama ni mtu wa kumtolea mfano baada ya ile picha yake ya ngono kusambaa na yeye kuikataa, kwasababu wewe ni miongoni mwa watu wenye kuamini kwamba ni kweli ni yeye anayeonekana katika ile video.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa ametole maelezo vizuri sana bora mkasoma uzi wake mtaelewa, hamna kitu kama hicho na haiwezekani, uliza mtaalam yeyote, hebu fuata uzi wa huyu jamaa huku
Upotoshaji uliopo kati ya uhusiano wa teknolojia ya 5G na corona - JamiiForums
Mkuu, kwahiyo maelezo/mtazamo wa mtu wewe umechukulia ndio Alpha na Omega ?? kwamba yeye alilosema ndio hilo Hilo? kwa mantiki hiyo tunachoona kwenye Noti ya Euro 20 tukitupilie mbali tubaki na mtazamo wa huyu jamaa?? this is too low from you , ulipoamkia leo sio kabisa

Zana ya 5G Inawezekana ikawa na ukweli au sii kweli, ila series ya Matukio ndio inaleta shida

Mwaka 2015 Bilgate akiwa anahutubia watu (sijui ni wapi) video niliona akasema janga linalokuja kuangamiza dunia sio Atomic bombs kama tunavyodhani , ni pendemic itakayo sababisha na kirusi, kwenye slides zake akaweka mwonekano wa kirusi huyo , huyo kirusi ni huyo huyo baadae akaja wekwa kwenye noti hiyo ya euro 20 , ni huyo huyo tunae mjua kama Covid-19 , noti hiyo ya Euro ni hapo hapo kuna hayo maminara ya 5G .. Dunia tuliyopo saiv ni dunia ya taarifa , huwezi ficha siri zote , lakn pia uelewa wa watu unapanuka kutokanA na upatikanaji wa elimu kua mwepesi

Upatikanaji huo wa elimu ndio umeamsha hili vuguvugu, upatikanaji huo wa elimu ndio unatufanya tujadili haya, na ndio maana leo tumeweza kataa kua specimen wa mzungu kwenye majaribio yake ya chanjo ,

lazima tujiulize , ni kwanini series ya matukio kutoka kwa watu hao hao imetuleta hapa ? kwann tusiamn n wao wanahusika hapa ? kwann 5G na Covid-19 wakaweka kwenye noti moja ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Back
Top Bottom