Tanzania inafuata mfumo upi wa uchumi?

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
Wananchi Tunaendelea Kupotoshwa na Mwelekeo wa Tanzania. Huu Uchumi wa Tanzania Unafuata Principles Zipi? Kama Kweli Ninavyofikiria Naona Wanataka "Free Market" Iwe Direction ya Inchi at the same time Hakuna Jitihada za Kuimarisha Private Sectors na Kujenga Middle Class at All. Leo Tukiangalia Infrastructures za Tanzania Katika Kila Maaneo Hakuna Efforts za Kuziimarisha na Hizi Priorities za Kujenga Infrastructures Zinatakiwa Ziwe Kipaumbele Sana Kuinua Uchumi wa Inchi. Mfano Security kwa Investors ni Kitu Muhimu Sana na Kinaonekana Kimemshinda Kabisa Kikwete. Ujambazi Katika Mabank na Wizi wa Fedha Kila Sectors za Inchi Umeenea na Pia Swala la Political Instability Linaonekana Wazi Kabisa Sasa. Kitu Gani Mtanzania Anachotaka Kukifanya Inchini Kitasaidia Kukuwa Kibiashara na Kutengeneza Profit? Philosophy na Vision ya Inchi Imepotea Siku Nyingi na Hatujui Kama CCM Wanaona Haya?

"Kukuwa kwa Biashara na Uinuaji wa Maisha ya Wananchi Utatokea Tu Endapo Inchi Inajali Haki za Wananchi na Kukua kwa Demokrasia. Kikwazo cha Tanzania ni CCM na Mafisadi Wengi Wakubwa"
 
Ni mfumo wa UJAPERI ndio tunaoufuata Tanzania.

Mfumo wa ujaperi bado ni dhana mpia sana na wengi hawajaufahamu vema. Hata Katibu Mkuu wa zamani hayati Horace Kolimba (apumzike kwa amani) ilimuwiia vigumu sana kulitambua bayana mfumo huu. Tena pale alipopatwa na maswali juu ya mfumo wetu huenda ndio kipindi ambapo mfumo wa UFISADI ulipochukua mimba na leo kutuzalia sisi wajukuu majuto yasioisha.

Kwa kifupi ni mchanganyiko wa Ujamaa kidogo kama kachumbari + Ubepari kutajwa tajwa tu kama kilainisha koo kwa Wahisani kuleta msaada + lakini Mloo Rasmi Mfumo wa UFISADI kwa kwenda mbele.
 
Mimi nadhani Tanzania bado hatujawa na uchumi wenye sura inayoonekana. Wakati wa ukoloni tulikuwa na mfumo wa uchumi wa kibepari japo wananchi wa chini walifanya kazi katika mfumo wa ubepari na wakapata chakula chao katika mfumo wa ujima wa kati. Baada ya Uhuru tuliazimia kuingia katika Ujamaa na Kujitegemea. Tukaanzisha mashirika chungu nzima ya umma. Tukaanzisha vijiji vya ujamaa na kuwahamisha wananchi kwa nguvu toka kwenye mahame kwenda kwenye vijiji vya ujamaa nk. Wakati tunafanya mabadiliko makubwa kama hayo, sheria zetu nyingi zikabaki zile zile za mkoloni. Tukaendelea kuwatumia nchi za kibepari kuinua uchumi wetu na wakati huo huo tukizitumia nchi za kikoministi. Ili kujiweka katika nafasi ya kupata kote, na kwakuwa wakati huo dunia iligawanyika katika matapo makuu mawili kutokana na vita baridi, tukaamua kuchukua sera za kutofungamana na upande wowote. Maana yake Marekani tupo na Urusi tupo.

Kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri ya kisera na kisheria, mashirika yetu ya umma yakaonekana kama mashimo ya kumeza fedha za umma. Mashirika ya umma yakawa yanaendeshwa kwa ruzuku. Shirika moja lenye mashine moja likaweza kuajiri mamia ya wafanyakazi ili mradi kila mtu ana ajira. Matokeo yake ni kwamba kiwanda kinachozalisha shilingi 10,000,000/= kwa mwezi kiliweza kutumia 100,000,000 kwa mwezi kwaajili ya mishahara. Kwa upande mwingine, sekta ya kilimo ikabaki namna ile ile ilivyoachwa na mkoloni na pengine duni zaidi. Kilimo kikabaki cha jembe la mkono kikitegemea vyua. Miundo mbinu ikabaki duni sana kiasi kwamba mahindi yangeweza kuoza Sumbawanga wakati Shinyanga watu wanakufa na njaa na fedha wanayo. Safari ya kutoka Morogoro hadi Dodoma ikawa ya siku mbili wakati Mwanza Dar Es Salaam safari ya wiki nzima. Kwa mazingira kama haya pamoja na matatizo mengine mengi yaliyoendana nayo yakatulazimisha kujaribu ubepari.

Tukarudia matatizo yale yale katika kwenda ubepari. Sera ikawa ya kibepari lakini sheria za kijamaa. Tukabinafsisha mashirika ya umma bila kuweka mazingira mazuri ya kisheria na liuchumi. Matokeo yake mashirika ya umma yakauzwa kwa "bei poa" kama anavyosema Prof Lipumba. Rasilimali kama dhahabu na almasi zikauzwa kwa bei za kugawa. Japo pamekuwepo na mabadiliko makubwa katika miundo mbinu bado maandalizi ya kuingia free market economy bado sio mazuri. Tutumie mtaji wa katiba mpya kuweka mufaka mpya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom