MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,472
- 8,692
Nimesoma mahali Watanzania wanashangilia sana Raia wa Kenya aliyekuwa awe Mkurugenzi wa Cocacola Kwanza kuzuiwa na uhamiaji. Watu wanashangilia sana kana kwamba sasa maisha yao yanaenda kubadilika.
Ila kinachonishangaza ni kwamba Kwenye Makampuni mengi ya hawa wafanya biashara wenye asili ya Asia wamejaza Watu wa nje kibao.MO na watu wa Asia kibao kwenya nafasi za juu. Arusha nenda kule A to Z kuna Wa Asia kibao hata kiswahili hawajui na cha ajabu sio Expert.
Arusha ukienda pale Culture Heritage Arusha, kuna walinzi wametolewa Nepali na uhamiaji ikatoa kabisa kibali, Kampuni nyingi za kitalii Arusha zina wazungu unakuta mzungu ni Mhasibu au ndo Meneja. Kuna Wazungu wengi mno Arusha wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya ila cha ajabu hata sisi hatulalamiki bali tunalalamikia Waafrika wenzetu Wakenya au Waganda.
Sasa kwa nini Uhamiaji inadili na hawa wanaotokea Kenya tu na kuwaacha hao wa Asia na Ulaya? Logic ni ipi hapa? au ndo sheria inavyosema kwamba wadili na wakenya pekee?
Huu ni ubaguzi sawa na ule unaofanywa na Waafrika Kusini, badala wapambane na Wazungu wao wanapambana na Waafrika wenzao, kwamba maisha yao magumu yanasababishwa na Waafrika wenzao na wala sio Makaburu.
Wabongo tunashangilia sana Uhamiaji kudili na Wakenya ila wale Wa Asia na Wazungu waliojazana huku tunaona ni sawa kabisa.
Fikiria Walinzi wanatolewa sijui Nepal then tunaona ni sawa kabisa.
Chuki zitatumaliza tusome tutafute Exposure