Tanzania inachungulia kaburini, wananchi amkeni

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Kwa hapa Tanzania ilipofikia hivi sasa inahitaji mapinduzi ya haraka, yaani yawe ya kijeshi au ya kiraia. utawala uliopo umeshindwa kabisa kwenye kila idara, sasa hivi imefika mahala ambapo hatujui hatma ya kesho yetu.

leo ktk historia ya taifa hili dola moja ya marekani ni tsh, 1620, sasa kwale walioweka pesa zao benk ktk fix acount ni hasara ya kiasi gani watakayopata!

tangu jumatano ya wiki iliyopita umeme unakatika kwa zaidi ya masaa 18 kwa siku. sasa kwa hapa tulipofika ni nini cha ziada tunahitaji kutoka serikali zaidi ya kushikana mashati,?. yaani ni kwamba serikali imefilisika hata pesa ya kununua mafuta ya kuwasha umeme hakuna.

Hizi kodi zetu zimeenda wapi? ni nani wanagawana pesa zetu, sasa ni fedheha gani zaidi ya hii tunayosubiri? kila kukicha ni heri ya jana.

Sasa tuache siasa ni lazima tuitwae nchi yetu sasa hivi.
 
Kwa mtu mwenye uzalendo wa kweli sio wa kuigiza hali ya nchi lazima ikuumize kichwa hali ya umaskin inazidi kuwa juu kama umeme ni kati ya mahitaji muhimu ya mtu na umeme unakatika masaa 18 mpk20 uzalishaji unafanyika saa ngap 2taweza kujikwamua na umaskini kwel hii itakua na itaendelea kuwa ndoto rais anaongea majukwaan uchumi wa nchi nchi umekua anaanglia nini hasa ilihali maisha ya watu yanaendaelea kuwa duni kwanini tisiwe kama Kenya nchi jiran kabisa watanzania 2amke jaman tatizo ni nini? woga,au kuridhika na umaskin 2lionao?
 
JK mambo yanamshinda kwanin asiresign nahis atapata heshima zaid mpk miaka 5 iishe tutakuje jaman?
 
mkuu ningependa kuchangia hoja yako kwamba nchi hii kuna matabaka ya aina mbili, wenye nacho na wasio nacho (hakuna mtu wa wastani leo) watu wa tabaka la chini ni karibu 80% na wanaumia mno lakini hawana nguvu ya kuwaunganisha na kuchukua jukumu la pamoja, resources na media zote zimeshikiliwa na hawa watu wachache wa tabaka la juu, wanazitumia kugawanya watu hasa kwa kutumia sera ya amani tuliyonayo, wanapandikiza mbegu ya woga mioyoni mwetu kila kukicha ili tu tusiweze kuchukua hatua yoyote, hii itatugawanya sana tutazidi kuumia na kunung'unika kila siku na mwisho wa siku wao wataendelea kuneemeka. Hata siku moja usitegemee kundi la watu elfu moja au laki ndio waanze mapinduzi, nia huanza na mtu mmoja kisha hufuatiwa kwa kuungwa mkono, ila kwa Tanzania ikifikia hapa watu huanza kuulizana 'nani wa kumfunga paka kengele', kwa swali hili watu huamua kulala majumbani mwao huku wakishindia nusu mlo kwa siku. MI nadhani tuvumilie tu hadi tutakapoanza kufa mmoja mmoja kwa njaa majumbani mwetu bila hata maandamano hadi kufikia idadi ya watu kama milioni nne hivi labda serikali ndio tutachukua hatua na pengine haya ndio yatakuwa mapinduzi ya kwanza ya aina yake kutokea katika historia ya dunia hii.
 
janga kama hili linalo endelea rahisi hata kueleza jitihada za makusudi ameshindwa,naona sasa wamefanikiwa kuweka mkurugenzi mwanasiasa kewnye hii kampuni nyeti nchini kila leo anahubiri siasa za umeme kwenye tv.alafu wanasema wanayaangaza maisha yetu??????
 
Huyu bwana mkubwa aliingia na siaisa za visasi kwa wenzie ndio kinapelekea kukomolewa manake wanataka awe rais wa kwanza failure Tanzania! naye ameshindwa ku side na wa vyama vingine wapenda haki na maendeleo ya kweli kwa Tanzania hii ndio maana anakufa na tai shingoni!

Mimi nadhani awe shujaa tu avunje baraza la mawaziri na kisha yeye naye ajiuzuru ili uitishwe uchaguzi mwnigine ambao tunajua wanaostahili kushinda ni akina nani. Kama anataka kulinda heshima na kukumbukwa kama shujaa wa nchi hii afanye hivyo tu.
 
mimi najiuliza kwa wafanyakazi wenye kimshahara mambo magumu hivi je kwa wale wasio na kipato inakuwaje, hii serikali ya miaka hii kweli pasua kichwa nashindwa kuielewa
 
Back
Top Bottom