Tanzania ina watumiaji milioni tano wa internet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ina watumiaji milioni tano wa internet

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by EMT, Jan 4, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa ripoti ya TCRA iliyotoewa hivi karibuni, kati ya Watanzania milioni 42, watu milioni 5 tuu ndio watumiaji wa internet. Ripoti inaonyesha kuwa mwaka 2005, watu milioni 1.6 walikuwa wanatumia internet, lakini idadi hiyo iliongezeka kuanzia Oktoba 2010 na kufikia watu milioni 4.8. Kati ya hao watumiaji milioni 5, watu 2,663,200 walikuwa wakitumia internet maofisini, 1,932,816 majumbani na 260,280 kwenye internet caf├ęs.

  Kwa upande wa Afrika Mashariki, mpaka Oktoba 2010, Kenya ilikuwa ikiongoza kwa kuwa na watumiaji wa internet milioni 10.2 milioni (zaidi ya mara mbili ya Tanzania). Uganda ilikuwa na watumiaji milioni 4.1. Hizi data ni kwa mujibu wa ripoti za KCC (Kenya) na UCC (Uganda). TCRA inadai kuwa idadi ya Watanzania wanaotumia internet kwa ajili ya mawasiliano imeongezeka hasa kutokana na vifaa vya wireless kuwa rahisi pamoja na kuwepo kwa simu za mikononi zenye teknologia mpya.

  Figures zinaonyesha kuwa kuna watu milioni 19 wenye simu za mkononi. Mobile wireless zinaongoza kwa asilimia 45, zikifuatiwa na wireless za kawaida. Ripoti inasema matumizi ya internet yameanza kuwa maarufu zaidi kuliko simu kama njia ya mawasiliano. Figues zinaonyesha kuwa Tanzania ina watumiaji 2,206,480 wa mobile wireless, 1,514,580 wa wireless za kawaida, 471,524 wa VSAT, 388,176 wa broadband na 269,536 wa cable.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 4. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tofauti inayoonekana ni kubwa sana. Naweza amini data za TCRA zaidi kuliko za Africa Internet Usage. According to facebook themselves, there are over 400,000 Tanzanians. Hii figure ya 600,000 ni ndogo sana.

  TCRA should be closer to accurate data more than Africa Internet Usage. TCRA sources data directly from ISPs and Telcom companies which is far more accurate than just speculating or using data derived from other sources.

  My two cents.

  Ram
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Kusema "wanaotumia internet" bila ya kutoa frequency ya matumizi hakutoi picha halisi.

  Je, mtu ambaye katumia internet mara moja tu, naye unamhesabu? Je anayetumia mara moja kwa mwaka? Mwezi? Wiki?

  Definition ya "wanaotumia" ni nini? Subscribers? Usage per a certain period?
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Nadhani 600,000 ndo inakaribia ukweli zaidi, angalia tulivyokuwa wachache humu Jf. Plus 400,000 Fb ukihesabu na wa TZ wa nje nadhani inamake sense.
   
Loading...