Tanzania ina uhakika wa 98% Bomba la mafuta ya Uganda kupitia Tanga

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
WIZARA ya Nishati na Madini imewahakikishia Watanzania kuwa Tanzania ina uhakika wa asilimia 98 za kupata mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda bandari ya Tanga, ambao unapiganiwa pia na nchi jirani ya Kenya.

Kutokana na hali hiyo, wizara hiyo jana imefanya mkutano na wafanyabiashara wa sekta ya mafuta, kuwaeleza fursa zilizopo kwenye mradi huo, jambo ambalo limewasukuma wafanyabiashara hao kuazimia leo kwenda Uganda kukutana na Serikali ya Uganda, kuwaeleza faida itakazopata nchi hiyo kwa kuleta mradi huo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, alisema kutokana na uhakika wa kupata mradi huo, ndiyo maana wameamua kufanya mkutano na wawekezaji wa sekta ya mafuta nchini waone fursa zilizopo kwenye mradi huo na zabuni ambazo wanaweza kuomba na ajira zinazopatikana katika mradi wenyewe na aina ya kodi itakayolipwa wakati wa mradi.

Kauli ya wafanyabiashara:

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara, Dk Gidion Kaunda alisema mkutano wa jana umehusisha wafanyabiashara wapatao 40 na wote kwa pamoja wameazimia leo kwenda Uganda kuzungumza na Rais Yoweri Museveni kuhakikisha kwamba mradi huo wa bomba unaletwa nchini. “Huu ni ushindani wa kibiashara, sisi tuko tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha tunaupata mradi huu wa bomba, hii ni fursa nzuri kwa nchi yetu.

Tumeamua kujitoa mhanga kesho (leo) tunaenda kuzungumza na Serikali ya Uganda,” alisema. Alisema wanaenda kuieleza Serikali ya Uganda sifa za Tanzania miongoni mwake ikiwa ni uzoefu wa kujenga mabomba hayo, usalama pamoja ujuzi wa teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

Akizungumzia mbinu zinazofanywa na Kenya ikiwa ni pamoja na kuleta wajumbe kukagua bandari ya Tanga wakati ujumbe uliokaribishwa ilikuwa ni kutoka Uganda peke yake, alisema kwamba Tanzania iliwazuia mawaziri kutoka Kenya kuingia bandari ya Tanga kwa kuwa hawakualikwa.

“Ni kweli walikuja maafisa kutoka Kenya, lakini tuliwazuia wasiende Tanga, waliishia uwanja wa ndege. Ila wale Waganda ambao tuliwakaribisha tuliwaruhusu kwenda bandari ya Tanga kukagua na kuchukua taarifa walizotaka,” alifafanua na kuongeza kuwa kwa kuwa suala hilo ni la kidiplomasia na Tanzania itaendelea kuchukua hatua stahiki .

Aliongeza kuwa Tanzania imejipanga na inaendelea kufuatilia kwa karibu ili mradi huo usichukuliwe na Kenya wakati sifa zinazotakiwa ziko Tanzania. Alisema makubaliano ya ujenzi wa bomba hilo yakikamilika ikiwa ni pamoja na njia litakakopita ujenzi wake utachukua miezi 36 pekee.

Kuhusu mradi wenyewe Ujenzi wa bomba hilo utagharimu dola za Marekani bilioni nne na litakuwa na urefu wa kilometa 1,410. Ujenzi wake ukianza Agosti mwaka huu utamalizika mwaka 2020 na utatoa ajira kwa watu zaidi ya 1,500.

Kenya ina nafasi ya kupoteza mradi huo kwa kuwa gharama za ujenzi ni kubwa kwani zinafikia dola za Marekani bilioni 4.5. Kulingana na taarifa ya TPDC, ujenzi wa mradi huo utaanzia katika Bonde la Ziwa Albert ambako ndiko mafuta ya Uganda yatachimbwa na mtambo wa mradi utajengwa katika eneo la Hoima ambako bomba litaanzia na kupitia maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kwenye mikoa ya Kagera na Singida hadi bandari ya Tanga.

TPDC imewahakikishia wanaharakati ambao nao wameingia kwenye mkumbo wa kupinga ujenzi wa bomba hilo kuwa hautapitia katika hifadhi ya taifa ya wanyama na pia ujenzi wake utakwepa milima pamoja na makazi ya watu.

Source: Habari Leo

MY TAKE: Ngoja tupate angalau haka ka mradi, tunaweza kujipoza na machungu ya kukosa hela za MCC
 
Kama kuna mtu ana ramani nzuri jinsi bomba litakapopitia atujuze yani linapoanzia, linapopitia mpaka kufika Tanga.
 
Kama kuna mtu ana ramani nzuri jinsi bomba litakapopitia atujuze yani linapoanzia, linapopitia mpaka kufika Tanga.
market01+pix.jpg
oil+triangle.jpg
 
Ngoja nianze kujiandaa kuwacheka manyang'au...
Waganda ni watu makini huwezi ukapeleka Bomba la mafuta lipite kenya ambako linaweza likawa linalipuliwa kila kukicha na Alshabab, investment kubwa kama hizi zinatakiwa ziende maeneo salama kama Tanzania
 
Kuna tetesi kwamba raisi wakenya anataka kwenda Ufaransa kulifuatia hili dili mwenyewe mimi bado siamini kama hii dili itakaa sawa mpaka pale nitapoona wamesaini mikataba.
 
Tuliosoma "Probability" bado asilimia mbili zinaweza kupata mradi! Swali langu kwa nn hatuna uhakika wa asilimia 100? Au mwandishi hakuiweka vizuri???
 
Back
Top Bottom