Wana JF,
Wiki iliyopita nilipata mtihani mgumu baada ya mgeni wangu ambaye namuheshimu sana alipoamua kunitupia suala ambalo sikulitarajia.Sijui yalimjia mawazo gani lakini wakati tunakaribia kuagana ghafla aliniuliza kwa kizungu "Are you proud of your country?"
Nilishusha pumzi na kupepesapepesa macho nikijaribu kutafuta jibu la haraka nikashindwa. Kwa vile ni mtu ninayemuhesimu sana, sikuweza kumtoa njiani au kumdanganya. Nilijaribu kuwaza mambo ambayo naweza kuyaita yakujivunia nikashindwa.Kila kilichokuwa kikija mawazoni mwangu kilikuwa si cha kujivunia bali cha kutia uchungu. Mambo yaliyonijia haraka yalikuwa kama:
- rushwa iliyopindukia mipaka,
- viongozi mafisadi, wezi waliojaa kila sekta na taasisi za serikali ambao hujitajirisha kwa kila nafasi anayoipata mtu,
- miaka karibu 50 ya uhuru hatuna hata umeme wa uhakika,
- watoto wanakaa chini mashuleni na hakuna kinachosomeshwa,
- mahospitali hayana madawa,
- barabara yo yote inayojengwa au kufanyiwa ukarabati basi ni kwa pesa ya msaada,
- tumeshindwa hata kujilisha licha ya kuwa na ardhi ya kutosha ambayo kama ikitumiwa kitaalamu tunaweza kulisha eneo kubwa la Afrika
- hata kuvua samaki tukala sisi wenyewe na kusafirisha tumeshindwa licha ya kua na eneo kubwa la bahari
- hao tunaoambiwa ni wataalamu wetu hawana hata kitu kimoja walichovumbua,
- tumefanya mageuzi ya kutokana na udikteta wa chama kimoja tumeshidwa.Demokrasia imeshindwa kupiga hatua.Vyombo vyote vya dola vinafanya kazi na kutumikia chama tawala na hata uchaguzi ukifanyika ni mizengwe mitupu,
- hata kwenye mambo ya michezo ni aibu tupu. Tunashindwa hata kuingia kwenye mashindano ya kombe la Afrika.
Mwisho ilibidi nimeze mate machungu nimjibu "NO, I'm ashamed".
Dalali