Tanzania Ina Nini cha Kujivunia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Ina Nini cha Kujivunia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dalali444, Feb 18, 2010.

 1. D

  Dalali444 Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Wiki iliyopita nilipata mtihani mgumu baada ya mgeni wangu ambaye namuheshimu sana alipoamua kunitupia suala ambalo sikulitarajia.Sijui yalimjia mawazo gani lakini wakati tunakaribia kuagana ghafla aliniuliza kwa kizungu "Are you proud of your country?"

  Nilishusha pumzi na kupepesapepesa macho nikijaribu kutafuta jibu la haraka nikashindwa. Kwa vile ni mtu ninayemuhesimu sana, sikuweza kumtoa njiani au kumdanganya. Nilijaribu kuwaza mambo ambayo naweza kuyaita yakujivunia nikashindwa.Kila kilichokuwa kikija mawazoni mwangu kilikuwa si cha kujivunia bali cha kutia uchungu. Mambo yaliyonijia haraka yalikuwa kama:

  - rushwa iliyopindukia mipaka,
  - viongozi mafisadi, wezi waliojaa kila sekta na taasisi za serikali ambao hujitajirisha kwa kila nafasi anayoipata mtu,
  - miaka karibu 50 ya uhuru hatuna hata umeme wa uhakika,
  - watoto wanakaa chini mashuleni na hakuna kinachosomeshwa,
  - mahospitali hayana madawa,
  - barabara yo yote inayojengwa au kufanyiwa ukarabati basi ni kwa pesa ya msaada,
  - tumeshindwa hata kujilisha licha ya kuwa na ardhi ya kutosha ambayo kama ikitumiwa kitaalamu tunaweza kulisha eneo kubwa la Afrika
  - hata kuvua samaki tukala sisi wenyewe na kusafirisha tumeshindwa licha ya kua na eneo kubwa la bahari
  - hao tunaoambiwa ni wataalamu wetu hawana hata kitu kimoja walichovumbua,
  - tumefanya mageuzi ya kutokana na udikteta wa chama kimoja tumeshidwa.Demokrasia imeshindwa kupiga hatua.Vyombo vyote vya dola vinafanya kazi na kutumikia chama tawala na hata uchaguzi ukifanyika ni mizengwe mitupu,
  - hata kwenye mambo ya michezo ni aibu tupu. Tunashindwa hata kuingia kwenye mashindano ya kombe la Afrika.

  Mwisho ilibidi nimeze mate machungu nimjibu "NO, I'm ashamed".

  Dalali
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dalali ungemwambia tunamafisadi wa kufa mtu...
  -Kiongozi akijiuzuru kwa kashfa akirudi kwao anapokelewa kwa mashangwe ya kufa mutu
  -Rais wetu mpenda masifa
  -ni nchi ya wasiopenda makuu na wasiojua rights zao
  -hata wewe ukiwa kiongozi unaiba tuuu...
  -ni nchi ukianzia na mtaji wa dola 100 utakuwa tajiri
  -watoto wa vigogo ndo huandaliwa kuwa vigogo...
   
 3. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Yap.,pamoja na mabaya yetu hayo lakini tunajivunia kuwa Watanzania na Nyerere kuzaliwa kwetu.,hakika kuna watu wengi wanatamani mzee yule angezaliwa kwao ili awe sehemu ya historia ya nchi zao.
   
 4. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 930
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 45
  huyo Nyerere huko alipo sijui anasema nini, maana kazi aliyofanya hakuna kinachoendelea....
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,411
  Likes Received: 2,039
  Trophy Points: 280
  Acha hizo wewe hata kama kazaliwa kwetu viongozi wetu wamefanya nini ili kudumisha his heritage zaidi ya ufisadi?
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  tuna wababaishaji nchi nzima, na mafisadi wa kimataifa bila kusahau chama cha kihuni kuliko vyote africa, CCM
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,187
  Likes Received: 2,712
  Trophy Points: 280
  Ufisadi!!
   
 8. k_u_l_i

  k_u_l_i Senior Member

  #8
  Feb 19, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Tanzania Ina Nini cha Kujivunia? "

  Wananchi watulivu - shida ya maji, umeme, kazi na mengineyo mengi lakini wananchi siku zote wako shwari wanaendeleza maisha yao.
  ┬ČK
   
 9. g

  gudlack Member

  #9
  Feb 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunajivunia kasi yetu ya kutaka utajiri, kila mtu kuanzia huko juuuuuu mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa tunataka kuwa mabilionea kama R al azzz, lowasa, kingunge, mramba, Mkapa nk
   
 10. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Wengi ni mambumbu ,tunajidai tumesoma(idadi ya Phd fake) na uswahili umetuzidi
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,264
  Likes Received: 28,919
  Trophy Points: 280
  mount kilimanjaro,serengeti,ngorongoro crater,lake tanganyika(deepest in the world??),very long coast line with natural sandy beaches bila kusahau ukarimu wa watanzania.
  hata kimoja hapo juu si cha kujivunia???
   
 12. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nikasema cha kujivunia ni yeye tu kuzaliwa Tanzania otherwise hatuna cha kujivunia
   
 13. T

  TANURU Senior Member

  #13
  Feb 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shule za Sekondari za Kata=====
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  tunajivunia uwanja wa kisasa wa mpira.......................................
   
 15. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Naona tulichobaki kujivunia ni ujinga wetu tuu!!
   
 16. M

  Mundu JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tunajivunia mashujaa wetu akina Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Mtemi Munyigumba, Mtemi Milambo.

  Tunajivunia kuwa na lugha moja ya kiswahili inayotuunganisha

  Tunajivunia rangi yetu (usiniulize kwanini)

  Tunajivunia nchi yetu (Kila wakati ninapokuwa nje ya Tanzania, nakumbuka na kutamani kurudi Tz mapema)

  Tunajivunia maliasili zetu (ingawa zinatumika kifisadi)

  Tunajivunia nguvu ya jeshi letu (Vita vya kagera, na operation Ngadzija)

  Tunajivunia jinsi tulivyosaidia ukombozi wa Afrika

  Jamani, chako ni chako, usikionee haya!!!
   
 17. k

  kanyika Member

  #17
  Feb 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo ina vitu vingi vya kujivunia Amani, Mlima mrefu Africa, Serengeti nk
   
 18. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Dalali444

  Nashangaa ulishindwa kumjibu swali rahisi kama hili, kwa nini hukumwambia sisi tunajisifia kuwa ni taifa pekee South of Sahara in Afrika ambalo tunatumia lugha moja. Hali ya hewa nzuri all season, tupo just below equator etc. Next time mwambie jibu linakuja kwenye e-mail just email me.

  Then mualike aje na familia yake Serengeti the seventh wonder of the world hasa mwezi wa Sept-October wakati wa migration ya wanyama pale, halafu aone the tallest free standing mountain etc. Aaaakhg mkuu umetuangusha lakini. Next time ukienda bongo mletee majani ya chai na kahawa aonje.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Sijui nini zaidi cha kujivunia zaidi ya uhuru wa bendera kama nao ni wa kujivunia,unless ujaribu kuwa narrow zaidi,kwa mfano ukawa more specific na uje na listi ili tufanye cross cheking.

  Pia ukumbuke kuwa historia ya nchi yetu nayo bado changa sana,na kwahivyo as a Nation,toka tupate uhuru kuna wenye kuweza kujivunia uzalendo?Amani nayo pia haimaanishi maendeleo,lakini je si quality ambayo tunaweza kujivunia kwa upande mwingine?

  Hivyo natoa changamoto utafakari tena kama kuna cha kujivunia ama la.....Ni kweli mawazo yako yalijikita mara moja kwenye mambo ambayo yamekuwa ni ya kukatisha tamaa hususan kasfha kama Richmond,EPA,Buzwagi,Rada,BOT Towers etc.

  Umasikini unaoongezeka na mambo mengine ya kukatisha tamaa na huku viongozi wakionekana kutokujali...Na kwahivyo ni kweli jibu la papo kwa hapo linaweza kuwa either or depending on you priorities and your memories,na pia in what aspect are you looking at the issue,je unazungumzia kuwa ni nini cha kujivunia on what aspect in relation to the Nation as a whole?

  Kama nilivyokupa mfano hapo awali,tunaweza kujivunia pia uhuru kama tutaweza kuupreserve in all its aspects....Kuweza kuutumia kwa kujiamulia mambo yetu kwa manufaa yetu wenyewe kama Taifa.....Kuweza kuondoa mfumo na tabaka la kinyonyaji lenye kuhujumu uchumi na rasilimali za Taifa letu....

  Ni kweli kadri muda unavyozidi kwenda begining from the time we aquired our independence,mambo ya kujivunia yamekuwa yaki dimish in ana alarming rate,hivyo ni wazi kabisa kuwa direction tuliyoko as a nation ni wrong....Rate ya kuongezeka kwa umasikini ni kubwa kuliko the other way round.
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,411
  Likes Received: 2,039
  Trophy Points: 280
  Nimekumbuka, tuna rais anayecheka muda mwing na pengine muda wote na anawalinda mafisadi!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...