Hatu huku tunazo Sunday market, garage sales etcetera. Na hayo magulio yapo kwa sababu ililetwa concept ya matumizi ya pesa na kalenda. Kama sio concept hizo hakuna cha maana katika magulio.
Neno "hayo" umelitumia kama "adjective" kwenye hiyo "restrictive clause" "hayo mavitabu yako"....huku maana ikibaki ile ile. Jaribio lako la kunizuga: FAIL!!!!
Companero:
Huyu bonge la mchumba nipe contacts zake nimlete huku. Huko atazeeka mapema.
Liberata MulamulaBaada ya kumbishia sana Zakumi kuhusu dhana ya William E. B. Du Bois kuhusu Moja ya Kumi wenye Talanta sasa nimeongoka. Nimeitafakari sana. Nimeijadili sana. Nimeihoji sana. Sasa nakubali kabisa kuwa ili Tanzania iendelee inahitaji asilimia 10 ya watu wake ambao ndio watakuwa injini ya kuiendeleza na sisi wengine (90%) tutafuatia. Tayari sehemu hii ya 10 imeshaanza kazi hiyo ila kinachohitajika ni kuwatambua na kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili zilete haraka mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kisiasa kijamii, kiutamaduni, kisayansi na kiteknolojia hapa Tanzania.
Nimeamua kuanza jukumu hilo na naamini Zakumi na wadau wengine mtashirikiana nami. Ikumbukwe kuwa Tanzania ina watu takribani milioni 40, yaani 40,000,000. Hivyo kwa mahesabu ya haraka haraka asilimia 10 ya watu hao ni watu 4,000,000 yaani watu milioni 4. Natumai server ya JF inatosha kuhifadhi database ya watu hao. Watu hawa wako katika nyanja mbalimbali ambazo zikiangaliwa kwa pamoja kama sekta mtambuka basi zitatusaidia kuweka vipaumbele vya maendeleo sawa. Kwa kufungua database yetu naanza na watu 10 ambao hakika ni sehemu ya 1 ya 10:
1. Prof. Keto Mshigeni - Scientist/Botanist
2. Hon. Zitto Kabwe(MP) - Economist-cum-Politician
3. Hasheem Thabeet - Basketball Superstar/Philanthropist/Role Model
4. Prof. Benno Ndulu - Economist/Bank Governor
5. Issa Michuzi - Photographer/Journalist/Blogger
6. Dr. Asha-Rose Migiro - Lawyer/Diplomant
7. Erasto Mpemba - Discoverer/Physicist
8. Dr. Thomas Neligwa -Computer Scientist/Mathematician
9. Liberata Mulamula - Administrator/Diplomat
10. Hon. Stella Manyanya (MP) - Electrical Engineer-cum-Politician
Angalizo: Hii sio mada ya Celebrity Forum - ni maada ya 'Siasa-Uchumi' (Political Economy) ya kutumia 'Talented Tenth' yetu kama 'zaka' ya kuleta a 'A Political/Governace, Social/Cultural, Economic/Financial and Scientific/Technological Revolution'.