Tanzania imo kwenye OneLaptop program?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,910
6,822
Naiweka hii hapa kwa vile wengi wetu huwa hatuchezi mbali na hapa. Hivi Tanzania imo katika huu mradi wa One Laptop per Child? kama hatumo, kwa nini tunasita?
 
najua waswahili watasema Laptop ni bei mbaya, bei yake ni us$100 tu.
 
..hatumo kwenye hiyo program

...priority yetu ni kupata wawekezaji wengi zaidi.
 
najua waswahili watasema Laptop ni bei mbaya, bei yake ni us$100 tu.

Imepanda, inauzwa dola 200 tu! Nadhani wengi tutalinganisha bei hii na ya mitumba iliyojaa! Hivi kweli hatuwezi kujitahidi tupate angalau moja kwa kila shule?
 
Tukiwa tunaongelea "open source" taarifa kwa watakaofaidika

kuna mbadala wa Microsoft Office hapa http://www.openoffice.org/

Inaweza kufanya kila kitu unachoweza kufanya na Microsoft Office, kwa bure!
 
Pundit thanks...
Mradi wa Laptop hatumo..kuna nchi zishabook hizo tangu kutangazwa kwake..hasa Algeria...sie mitumba inatufaa lkn si kwa watoto, hizo onelaptop zinawafaa watoto..let say std 1 to 7...
HATA KAMA TUMO ktk MRADI tutakwama ktk UMEME kwani hadi sasa hatuna UMEME wa UHAKIKA...
 
ndo ile kesi ya Celtel kupatikana hadi vijijini, JE UMEME nao upo? unakwenda charge simu kwa mjumbe au Kibosile mliemuuzia mazao yenu...
 
Pundit thanks...
Mradi wa Laptop hatumo..kuna nchi zishabook hizo tangu kutangazwa kwake..hasa Algeria...sie mitumba inatufaa lkn si kwa watoto, hizo onelaptop zinawafaa watoto..let say std 1 to 7...
HATA KAMA TUMO ktk MRADI tutakwama ktk UMEME kwani hadi sasa hatuna UMEME wa UHAKIKA...

Hivyo vi-laptop si lazima vitumie umeme unaomaanisha. aidha ni betri au hasa solar energy. Niliandika kuhusu hii project muda mrefu kidogo uliopita katika thread ya high speed internet connection(and wireless) in Tanzania. Seems no one had eyes to see it...or time to look at it.
 
Tatizo letu ndio hilo, tunapenda mno siasa!
 
1. Watanzania jamani- hizi lap top mnamaanisha kwa watoto wanfunzi wa mijini au vivijini?

2. Do we need such laptop wakati watoto wetu hawana uhakika na mlo shuleni na madarasa ni ya tope na kuezekwa kwa nyasi na hakuna hata waalimu?

We need to set our invetment in Education priorities right!
 
Tatizo microsoft hawauzi mojamoja kama DVD za jumanne iddi, wanaingia mkataba na nchi husika, Thailand wamesema zao ziwe na internet connection ili class asignment ziwe online, libya wamesema zao ziwe na solar energy zifae hata vijijini. nasikia UDSM asignment bado wanaprint nakufanya binding, eti nikweli?
 
Ila kwa habari nilizozipata mwishoni mwa mwaka jana 2007 wizara ya Elimu ikipata msaada kutoka kwa Microsoft waliwagawia Ma Afisa Elimu wa Wilaya zote za Tanzania Laptop kila mmoja wao na kuwapa Seminar iliyofanyika Bagamoyo. Nafikiri Mwendo sio mbaya ingawa tupo mbali sana na Dunia inavyokwenda.Sasa sijui hii wakina Kayumba lini itawafikia?
 
Ila kwa habari nilizozipata mwishoni mwa mwaka jana 2007 wizara ya Elimu ikipata msaada kutoka kwa Microsoft waliwagawia Ma Afisa Elimu wa Wilaya zote za Tanzania Laptop na kuwapa Seminar iliyofanyika Bagamoyo. Nafikiri Mwendo sio mbaya ingawa tupo mbali sana na Dunia inavyokwenda.

Kwa bahati mbaya hii imekuwa ndiyo kawaida yetu. Top down economics badala ya kulenga watumiaji. Ukiingia ofisi za serikali mabosi wengi wana laptop na PCs ( wengine mbili mbili!) lakini barua bado wanadictate kwa sekretari, hawana e-mail address na hawajawahi kuingia kwenye internet isipokuwa pengine zile sehemu sehemu! Watoto na vijana ndio wana udadisi na uelewa wa haraka haraka wa teknolojia mpya. Hawa ndio huu mradi wa One Laptop inawalenga. Si kompyuta ya kukaa ofisini kwa mwalimu mkuu itakayotumika siku shule itakapotembelewa na wageni waalikwa. Microsoft na Intel ( Intel wamejitoa sasa hivi kwenye mradi wa OneLaptop)wana mradi wao wa Classmate kompyuta ambayo ni aghali zaidi , US $ 350 na inatumia MS office products. OneLaptop kama ilivyoelezwa kabla inatumia open-source products. Lakini pengine kigugumizi kinatokana na ukweli kuwa hakutakuwa na study tour na semina nyingi kama tutachagua OneLaptop. Sasa hao maafisa elimu watakula wapi?
 
FM, sasa umeanza kuleta point, unafikiri mradi huu kwetu tutaufanikishaje? angalau tuanze na wanafunzi wa university! kwani wengine wa mba bado wanaandika asignment kwenye madaftari. nadhani tunaweza tukamshauri prof.msola tukaanza na university students kama pilot project, waachane na kutumia ruled paper. mambo ya ODM na PNU tuyaache kwanza.
 
Sidhani kama huu mradi umelengwa kwa hao wa university! Ni vigumu child kuwa university.
 
Intel has started to sell it India for $500. YES THATZ TRUE.. 500 dollars..It was all marketing to get the Government and schools to buy INTEL products. Shame on you INTEL
 
Imepanda, inauzwa dola 200 tu! Nadhani wengi tutalinganisha bei hii na ya mitumba iliyojaa! Hivi kweli hatuwezi kujitahidi tupate angalau moja kwa kila shule?

..halafu itatumiwa na nani?mwalimu mkuu au?

..ni bora kuwa nazo katika baadhi ya shule,zitakazostahili,kuliko kuzisambaza moja kwa kila shule.haitaleta maana.
 
FM, sasa umeanza kuleta point, unafikiri mradi huu kwetu tutaufanikishaje? angalau tuanze na wanafunzi wa university! kwani wengine wa mba bado wanaandika asignment kwenye madaftari. nadhani tunaweza tukamshauri prof.msola tukaanza na university students kama pilot project, waachane na kutumia ruled paper. mambo ya ODM na PNU tuyaache kwanza.

..hao wa mba hawahitaji hizi,kwani ni za watoto wa shule!

..hiyo mibaba na mimama ina hela za kununua hata pc za usd 1000.

..ukitaka kujua,fanya iwe lazima kwa mba kuwa na pc,utaona!

..mradi kama huu unatakiwa uwe kwa shule za msingi na labda o'level!
 
Hizo laptop ziko za betri za kujaza kwa kusokota kwa mkono. Nielewavyo Rwanda na Burundi wamo kwenye mradi lakini sisi hapana. Kuna kuwawekea internet connection.

Kwenye nchi isiyo na maktaba za mikoa na wilaya kama ya kwetu, basi huu mradi ni muhimu sana. Maktaba ya jumla ni internet.

Kwa sasa, itabidi serikali iwe na sera zitakazosukuma upatikanaji wa internet cafes nyingi, na kila wilaya, ili ziwe ndiyo maktaba za shule zinazoanzishwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom