Tanzania Imetawaliwa na Siasa za Uwoga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Imetawaliwa na Siasa za Uwoga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njoka Ereguu, Apr 22, 2012.

 1. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Huu ndio ukweli kinachoendelea Tanzania ni wanasiasa wetu kutawaliwa na siaza za uwoga kwa kujua au bila kujua kuwa siasa za namna hiyo ni sumu kubwa katika kusukuma maenedeleo ya nchi nyuma. Uwoga huu umetawaliwa na umaskini wa wanasiasa na njaa zilizowasukuma kuingia katika siasa bila kuwa na weledi na utashi wa kusimamia kile wanachokisema kwa maslahi ya wananchi waliowachagua.

  Katika vuguvugu linaendelea sasa utabaini kuwa wabunge wote walioonekana kuwa msatari wa mbele kukemea madudu na wizi wa mchana wa viongozi wajuu wa serikali watatishwa kwa maana ya kuwa endapo wataendelea kuwa hivyo watafukuzwa kwenye chama au hawatapata uwakilishi huo 2015. Kwa kuwa wengi wametawaliwa na siasa za uwoga watakubali kukaa kimya ili waendelee kunufaika na jasho la wananchi.

  Endapo siasa za uwoga hazitapatiwa ufumbuzi, Tanzania kuendelea ni ndoto, tutaendelea kuimba tuna madini, mafuta, gesi, ardhi n.k ili kuendelea kuwaneemesha wachache kwa ujinga wetu kwa kuwa tunawapa kura wenyewe.

  I submit
   
Loading...