Tanzania imeshinda goli 2 kwa mtungi dhidi ya Botswana,

Diksela

JF-Expert Member
Nov 6, 2014
212
208
IMG_20170325_190352.jpg

KIkosi cha Botswana dhidi ya Tanzania ni;

Dambe
Gadibolae
Vanderwesthuizem
Ramoraka
Nato
Galenamotlhale
Ditsele
Kebatho
Gaolaolwe
Sesenyi
Ngele


KIkosi cha Taifa Stars dhidi ya Botswana ni;

Manula
Kapombe
Hussein
Nyoni
Banda
Himid
Msuva
Domayo
Samatta (C)
Ajibu
Kichuya .

Dakika 90 za mchezo kati ya Tanzania na Botswana zimemalizika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunga mabao mawili na kuiwezesha Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Samatta alifunga bao la kwanza katika dakika ya tatu tu katika mechi hiyo ya kirafiki katika kalenda ya Fifa.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Botswana nao walionyesha uhai lakini Stars walikuwa imara.

Mara kadhaa, kipa wa Botswana, alionyesha umahiri na kuokoa mikwaju kadhaa.

Samatta alishindilia bao la mwisho zikiwa zimebaki dakika chache akipiga mkwaju matata wa adhabu.
 
Msuva angefunga goli nyingi lakini mpira ulimkataa.Beki yetu Kapombe hakuwa fiti,hata Banda na mwenzake walikuwa wanajichanganya sana.Kwa ujumla timu imeonyesha uhai mkubwa kama wataendelea hivi tutatoka kwenye tope la Mkwasa.
 
Miye nawapa hongera tumejituma. Na pongezi zaziada kwa Samanta nyota iendelee kun'gaa
 
Samata huyu anayetaka Dar iitwe Koromije?

Mwaikyembe kaanza vizuri Wizara Tunataka na Basketball yetu pia
 
Mambo ya Harrison mwakyembe hayo kwa mwendo wa huyu waziri navyomfahamu tunaweza shiriki world Cup ya 2022 ya Qatar, hongera kwake
 
Mwalim MAYANGA anakazi kubwa ya kuijenga timu! nasema hivi sababu its poor team perfomance! kilichotusaidia ni uwezo wa wachezaji binafsi pamoja na bahati ! kwang binagsi timu haijacheza vizuri kuanzia nyuma,katikati,atleast finishing tena ni sababu we score one moving goal na set piece moja! team haimiliki mpira na inapoteza mpira kirahisi,mabeki wanafanya makosa mengi kana kwamba tungekutana na team yenye aggresive attacking forward tungekula nyingi tu! viungo wanapoteza mipira kirahisi na team haimiliki mpira kabisa na kama tujuavyo kutoboa international ili kuchuana na senegal ya akina mane na diof au morroco ya akina soufiane inakubidi umiliki mpira! hvo kocha inabidi awapike viungo na abadili falsafa ili team imiliki mpira tuweze kupata team ya ushindani
[HASHTAG]#iker[/HASHTAG] moekhitaryan!
 
Msuva angefunga goli nyingi lakini mpira ulimkataa.Beki yetu Kapombe hakuwa fiti,hata Banda na mwenzake walikuwa wanajichanganya sana.Kwa ujumla timu imeonyesha uhai mkubwa kama wataendelea hivi tutatoka kwenye tope la Mkwasa.
Tope la Mkwasa? Kwa kuifunga under 20 ya Botswana? Subiri tukutane na timu za soka!!
 
Aah! Unamtetea mkwasa kwa lipi alilofanya stars.Ngoja kesho uone Sulumu Mayanga nizaidi ya Mkwasa tutakapo wafunga Burundi.
 
Back
Top Bottom