Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Kwa mujibu wa comparitech Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa sera mbovu za usajili ambazo zinafanya mtumiaji wa simu akose faragha ya simu yake, kwa kukosa sharia zinazohusu faragha ya mtu kutumia simu,
Usajili wa kutumia alama za vidole unaofanywa pia unaongeza hatari kwa kuwa taarifa za mteja hupelekwa kwenye mamlaka husika mwezi mmoja baada ya kujisajili.
Nchi zinazofuata baada ya Tanzania ni Saudi Arabia imeshika namba mbili, north korea na Uganda zipo nafasi ya tatu
Japo mambo haya huonekana kuwa yanaleta usalama kwa watumiaji wa mitandao, lakini bado Tanzania haiku vizuri kwenye usalama wa mtandao CyberSecurity, kwa tafiti za Comparitech walizopanga kutoka kwa mtiririko wa wanaofanya vibaya hadi wanaofanya vizuri, Tanzania ni ya nne ukianzia kwa walio na ubovu wa ulinzi wa mtandao, asilimia 28.3 ya simu zake zikiwa na malwares, huku computer zake asilimia 14.7 zikiwa na wadudu waiba taarifa, nchi ya kwanza kwa ulinzi mbovu wa mtandao ni Algeria, ya pili ni Indonesia, ya tatu Vietnam na Tanzania ikiwa ya nne
Hali hii inaonekana kuwa serikali inawekeza muda mwingi kutaka taarifa kwa wananchi wake kiasi cha kuwa na sera mbovu huku wakiwa na ulinzi mbovu wa mtandao unafanya taarifa zake kama nchi na wananchi wake wazi Zaidi kwa watu wan je au computer geeks
Taarifa za wananchi sio vibaya kuwa nazo lakini kama tunangalia ndani Zaidi na kuacha usalama wan chi ukawa vulnerable kiasi kikubwa kwa computer geeks ni hatari Zaidi
Tujitambue
Signed
Oedipus
Hongera Magufuli; viva awamu ya 5. Watanzania tunapaswa kujipongeza kwa mafanikio haya ya kujivunia.