Tanzania imeshakuwa kama jumba la sanaa kwa sasa

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,932
5,560
Heshima kwenu Wana JF,

JPM baada ya kuapishwa alifanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 349 yalikwepa kodi bandarini watumishi wa bandari TPA na TRA wakawajibika .

Waziri mkuu baada ya kuapishwa naye alifanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 2490 yalipitishwa bila kulipa kodi watumishi wa TRA na TRA wakawajibika pia.

Waziri wa uchukuzi baada ya kuapishwa jana amefanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 11,884 pamoja na magari 2019 yalipitishwa bila kulipia kodi kuna watumishi wa bandarini TPA na TRA wamewajibishwa .

Sinema inakuwa pale ambapo wanawajibishwa watumishi wa TPA ,TRA na baadhi ya wafanyabiashara wadogo lakini wale wakubwa hawaguswi.

Mara nyingi sana tumekuwa tukiilalamikia serikali kwa uonevu wakati wa kuwajibisha huwa inadili na vidagaa tu lakini mapapa huwusa hawaguswi.

Hivyo basi tunataka serikali iwafuatilie wamiliki wote wa hayo makontena zaidi elfu 13 walipe kodi na kuchukuliwa hatua kali .

Pia waliokuwa mawaziri katika hiyo uchukuzi walipaswa kuwa chini ya ulinzi kulisaidia jeshi la polisi upelelezi haiwezekani ukwepaji mkubwa kama kufanya bandarini bila waziri husika kujua .

Tumeshachoka kusikia habari za makontena yaliyokwepa tunataka kusikia wamiliki wa hayo makontena wamekamatwa na wanalipa kodi .Hatutaki sifa za ziara za kushtukiza bila mafanikio.

Wenzetu Ethiopia na China ukikamatwa umekwepa kodi unafilisi mali zako zote na hatua zingine zinafuata .
 
Last edited by a moderator:
Heshima kwenu Wana JF.

JPM baada ya kuapishwa alifanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 349 yalikwepa kodi bandarini watumishi wa bandari TPA na TRA wakawajibika .
Waziri baada ya kuapishwa naye alifanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 2490 yalipitishwa bila kulipa kodi watumishi wa TRA na TRA wakawajibika pia.
Waziri wa uchukuzi baada ya kuapishwa jana amefanya ziara ya kushtukiza bandarini akabaini mankotena 11,884 pamoja na magari 2019 yalipitishwa bila kulipia kodi kuna watumishi wa bandarini TPA na TRA wamewajibishwa .
Sinema inakuwa pale ambapo wanawajibishwa watumishi wa TPA ,TRA na baadhi ya wafanyabiashara wadogo lakini wale wakubwa hawaguswi .
Mara nyingi sana tumekuwa tukiilalamikia serikali kwa uonevu wakati wa kuwajibisha huwa inadili na vidagaa tu lakini mapapa huwusa hawaguswi.
Hivyo basi tunataka serikali iwafuatilie wamiliki wote wa hayo makontena zaidi elfu 13 walipe kodi na kuchukuliwa hatua kali .
Pia waliokuwa mawaziri katika hiyo uchukuzi walipaswa kuwa chini ya ulinzi kulisaidia jeshi la polisi upelelezi haiwezekani ukwepaji mkubwa kama kufanya bandarini bila waziri husika kujua .
Tumeshachoka kusikia habari za makontena yaliyokwepa .tunataka kusikia wamiliki wa hayo makontena wamekamatwa na wanalipa kodi .
Hatutaki sifa za ziara za kushtukiza bila mafanikio.
Wenzetu Ethiopia na China ukikamatwa umekwepa kodi unafilisi mali zako zote na hatua zingine zinafuata .
Emma ....Na hapo nipo Makufuli hatakapo anza kushindwa kazi . Huwezi amini mtu kama Bahlesa anakwepa kodi halafu Anapewa muda ili alipe kodi.Muda huu alitakiwa kuwa ndani ili iwe fundisho Kwa wengine
 
Mimi naona kulipa kodi ni lazima alipe, ila kampuni husika (ICD na wakala) lazima zifungiwe na kufilisiwa. Mwenye ICD na Kampuni ya wakala lazima washitakiwe kwa kuhusika na ukwepaji kodi. Kututangazia tu kuwa watumishi wa bandari au TRA wamekamatwa ni upuuzi na ni usanii usiokubalika.

tunataka kusikia wahusika wameshakamatwa wameshalipa kodi hatutaki usanii wa kubaini kila siku huu usanii unafanyika Tanzania tuu.
 
hao watumishi wa TRA na TPA ndo wawataje hao wafanya biashara wakubwa na wenye makontena na watoe ushaidi wa kuweza kuwashika na kuwafungulia kesi za kuwalipisha kodi walizokwepa na faini juu hao wafanyabiashara wakubwa, bila wao kutoa ushirikiano au ushahidi kwa vyombo vya dola hutaweza mkamata mtu mkubwa utamshtaki kwa lipi? hao majama ndo wanajua walimpitishia nani na ndo wao wakwanza kuvunja sheria kwa kupitisha makontena bila kulipiwa kwasabu kazi ya ilikua kuhakikisha yanalipiwa
 
Tanzania yangu na uongozi wake ni jumba la sanaa.Tusubiri tuone mhusika mkuu na wahusika wasaidizi wanamaliza vipi hii Tamthilya.
 
Tunataka kujua mtandao wenye hao wanapitisha makontena bila kulipia kodi ni akina nani?wanabebwa na nani?
 
Nnachokiogopa hawa wahuni watakapoona kua kumbe hawachukuliwi hatua, wataota sugu na hali ya ufisadi itakua mbaya kuliko ilivyokua mwanzoni.
 
Tanzania yangu na uongozi wake ni jumba la sanaa.Tusubiri tuone mhusika mkuu na wahusika wasaidizi wanamaliza vipi hii Tamthilya.
tuliona kasi ya maigizo mwanzoni baada ya kile kikao cha kamati kuu ya wenye nchi hakuna kinaendelea ngoja tuendelee kusubiri
 
Nnachokiogopa hawa wahuni watakapoona kua kumbe hawachukuliwi hatua, wataota sugu na hali ya ufisadi itakua mbaya kuliko ilivyokua mwanzoni.
hakuna chochote mkuu hata Waziri mkuu akifanya ziara leo muda huu utakuta kuna upotevu tena mankotena tatizo ni mfumo wanatakiwa kuufumua na wahusika wachukuliwe hatua hukuona yule mtuhumiwa Masamaki ameweka dhamana kwa bilioni sijui 3 utagemea wenzake wataogopa kuendelea kupitisha mankotena bila kulipa kodi?
 
Last edited:
hakuna chochote mkuu hata Waziri mkuu akifanya ziara leo muda huu utakuta kuna upotevu tena mankotena tatizo ni mfumo wanatakiwa kuufumua na wahusika wachukuliwe hatua hukuona yule mtuhumiwa Masaki ameweka dhamani kwa bilioni sijui 3

Ndio nasisitiza kwamba wao wanafikiri wanatumbua majipu kumbe wanayapapasa yatakua sugu na yasiyopona kabisa.
 
tuliona kasi ya maigizo mwanzoni baada ya kile kikao cha kamati kuu ya wenye nchi hakuna kinaendelea ngoja tuendelee kusubiri
Na hapo ndipo wenye akili walianza kung''amua ni aina gani ya nchi tuliyopo.Waliolala hadi leo wanaamini kuna jipya!Nakuambia ukifuatilia vizuri utagundua dhamira ya mkuu wa kaya ni safi kabisa ila kuna lidubwana limoja ambalo linamfunika na kumhujumu! Ikitokea mkuu wa kaya akaamua kufa na dhamira yake tutegemea mazuri mbeleni ila hata hivyo kwenye uteuzi wa kikosi kazi kimeonyesha dubwana limeshamzidi kipenzi chetu nguvu.Hapa kuna mambo mawili tu mosi, afe na dhamira yake atutumikie kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano pili, akubali kusalimu amri kwa hili dubwana atumikie miaka kumi.Ila ukubwa wa cheo cha mkuu wa kaya ni mtamu nadhani option ya pili itakuwa jibu kwa kuwa hata dalili tumeshaanza kuziona.
 
Ndio nasisitiza kwamba wao wanafikiri wanatumbua majipu kumbe wanayapapasa yatakua sugu na yasiyopona kabisa.
huo ndo ukweli huu usanii unafanyika hakuna nia njema .majipu wanayapapasa tu wanapita
 
Na hapo ndipo wenye akili walianza kung''amua ni aina gani ya nchi tuliyopo.Waliolala hadi leo wanaamini kuna jipya!Nakuambia ukifuatilia vizuri utagundua dhamira ya mkuu wa kaya ni safi kabisa ila kuna lidubwana limoja ambalo linamfunika na kumhujumu! Ikitokea mkuu wa kaya akaamua kufa na dhamira yake tutegemea mazuri mbeleni ila hata hivyo kwenye uteuzi wa kikosi kazi kimeonyesha dubwana limeshamzidi kipenzi chetu nguvu.Hapa kuna mambo mawili tu mosi, afe na dhamira yake atutumikie kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano pili, akubali kusalimu amri kwa hili dubwana atumikie miaka kumi.Ila ukubwa wa cheo cha mkuu wa kaya ni mtamu nadhani option ya pili itakuwa jibu kwa kuwa hata dalili tumeshaanza kuziona.
ugumu hawezi kwenda kinyume na mkuu wa kaya ndo tatizo lipo hapo
unataka kupambana na mafisadi wakubwa lazima uwe dhamira ndani ya moyo siyo kuongea ovyo halafu utekezaji unakuwa ziro tuliambia wataunda mahakama ya mafisadi ambapo hii mahakama itakuwa inashughulikia mafisadi duh nikikumbuka naishia kucheka kila kitu ni kama maigizo kwa sasa .Kagame alipomwambia Mkwere amempa bandari tuu aongoze nchi kwa kasi ya maendeleo wengi waliona ni kauli ya madharau sasa wanaanza kuona uozo unafanyika na yanayoendelea
 
Back
Top Bottom