Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,096
Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na 32 zilizoridhia mkataba huo Duniani.

Utiaji saini wa mkataba huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo, Profesa Kabudi amesema kuwa, kwa kusaini mkataba huo Tanzania inaunga mkono jitihada zote za kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, ikiwa ni sehemu ya kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama pa kuishi.

Hata hivyo Profesa Kabudi amesema kuwa, Tanzania inaunga mkono matumizi ya amani ya nyuklia.
 
Nilimshuhudia Prof. Kabudi akipiga picha na BEBERU. Bila shaka walikunywa juisi na BEBERU. Wakiwa huku kwetu wanawaita mabeberu, wakienda kwa hao wanaoitwa mabeberu wanawaita wadau wa maendeleo. Natamani siku moja nimwone Dr. Bashiru Ally akiwa Marekani akipiga picha na hao mabeberu kama Kabudi alivyofanya.

Maswali kwa Dr. Bashiru. Je, unaunga mkono Kabudi kupiga picha na yule beberu? Je, upo tayari kupokea misaada toka kwa mabeberu?
 
Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na 32 zilizoridhia mkataba huo Duniani.

Utiaji saini wa mkataba huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo, Profesa Kabudi amesema kuwa, kwa kusaini mkataba huo Tanzania inaunga mkono jitihada zote za kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, ikiwa ni sehemu ya kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama pa kuishi.

Hata hivyo Profesa Kabudi amesema kuwa, Tanzania inaunga mkono matumizi ya amani ya nyuklia.
kwanini wasi saini wakati hata vi toothspick tunatengenezewa toka China
 
Juzi nilikuwa naangalia namna wenzetu wanavyojiandaa na endapo kutatokea jabali(kimondo) likaja upande wa dunia ilipo na kutishia usalama wa sayari yetu.

Wametengeneza mashine maalumu ya kuhakikisha binadamu tupo salama. Nikawaza sana, sana nikajisemea, watu weusi huku Africa kweli tuna safari ndefu.
 
kabudi umesaini lakin nchi yako.haina mashiko yoyote. labda ungesain mkataba wa kupinga matumizi silaha zinazotumiwa na ccm aina ya POLISI hapo tungekuelewa. watanzania wa ccm wanachojua ni emama nyukilia weee ruka mbali kutafuta uwa zuri

Duh! Umeua mkuu.
 
daaah
 
Afu huu wimbo huwa naimbia wanangu kila siku. Pumbavu sana!
 
Tanzania imesaini mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 60 zilizosaini na 32 zilizoridhia mkataba huo Duniani.

Utiaji saini wa mkataba huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York nchini Marekani.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo, Profesa Kabudi amesema kuwa, kwa kusaini mkataba huo Tanzania inaunga mkono jitihada zote za kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia, ikiwa ni sehemu ya kuufanya ulimwengu kuwa mahali salama pa kuishi.

Hata hivyo Profesa Kabudi amesema kuwa, Tanzania inaunga mkono matumizi ya amani ya nyuklia.
Ila na ss Tanzania tungetengeneza hata kinu ki1 cha nyuklia kwa matumiz ya umeme maana source of energy zpo vry low.
 
Yaani Marekani, China, Russia, Israel, India, Pakistan wasisaini sisi kwa nini tusaini?

Ilipaswa nchi nyingine zigome kusaini ili iwe ni pressure kwa wengine nao kuziachia hizo silaha
 
Tatizo ni kwamba watanzania hatufundishwi Historia. Mwalimu alikaa Ikulu miaka zaidi ya 23 na yeye alikuwa ni miongoni mwa watu waliopinga kwa nguvu zote huko mkataba wa kuzuia matumizi ya silaha za Nyukilia.

Cha ajabu wanaodai wanamuenzi Mwalimu ndio wao wamesaini mkataba ambao Mwalimu alikuwa anaukata kwa miaka yake yote akiwa Rais.
 
Utazani ana hata mshale wa nuclear nchini kwake ,assign uchaguzi wa huru na haki bila kusahau Uhuru wa kujieleza
Asisahau kuwaomba ushirikiano wa upelelezi wa kesi nzito kama lisu asasination, azary nk
 
Tatizo ni kwamba watanzania hatufundishwi Historia. Mwalimu alikaa Ikulu miaka zaidi ya 23 na yeye alikuwa ni miongoni mwa watu waliopinga kwa nguvu zote huko mkataba wa kuzuia matumizi ya silaha za Nyukilia.

Cha ajabu wanaodai wanamuenzi Mwalimu ndio wao wamesaini mkataba ambao Mwalimu alikuwa anaukata kwa miaka yake yote akiwa Rais.
Embu tushushie Nondo mbili tatu juu ya mwalimu na mkataba huo
 
Back
Top Bottom