Tanzania imekutana na Umoja wa Ulaya (EU) kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Serikali ya Tanzania imekutana na Umoja wa Ulaya (EU) kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya Umoja huo na Tanzania.

Akiongea wakati wa kikao cha wataalamu kutoka Tanzania na EU kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema kikao hicho kinalenga kujadili makubaliano yaliyokwama awali kutokana na Tanzania kutokuwa tayari kuridhia baadhi vipengele vilivyomo kwenye mkataba huo.

Prof. Kahyarara amesema Tanzania haikukubaliana na baadhi ya vipengele vya mkabata wa EPA na kuona kuwa ni vigumu kuingia katika makubaliano ya mkataba huo kabla ya kurekebisha vipengele hivyo.

“Tumekaa na wataalamu wetu na wenyewe wamekuja na wataalamu wao, tutapitia kipengele kimoja baada ya kingine na tunaamini tutafika mwisho na kama tulivyo waambia wenzetu wa EU tunaona faida ya kufanya biashara na wao kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Prof. Kahyarara

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti amesema majadiliano hayo yanalenga kuangalia vipengele vya mkataba ambavyo Tanzania ilionesha mashaka katika kikao kilichopita ili kuvipatia ufumbuzi na kusonga mbele kwa pamoja hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania sasa inatoa kipaumbele katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

“Itakumbukwa kuwa Tanzania inatekeleza diplomasia ya uchumi na wawekezaji kutoka Umoja wa Ulaya wanania ya kuja kuwekeza Tanzania na Afrika Mashariki, hivyo tukikamilisha majadiliano haya itakuwa ni jambo lenye maslahi kwa pande zote,” Amesema Balozi Fanti.

Kikao cha leo kinatokana na mazungumzo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyafanya alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Ubelgiji ambapo alikutana na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya, Bw. Charles Michael mwezi Februari 2022.

Pia, soma;

1). ACT-Wazalendo: Mkataba wa Mashirikiano ya kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA), unaruhusu upotevu mkubwa wa Mapato

2). Umakini na njia mbadala unahitajika, mkataba wa EPA huwenda ukaivunja jumuiya ya Afrika Mashariki

3). Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

2 (1).jpg

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti akiongea na washiriki wa kikao (hawapo pichani), kulia ni Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

4 (1).jpg
Washiriki kutoka Tanzania na Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja
 
 
Nikisikia neno wataalam au prof basi naanza kupata mashaka sijui kwanini??
 
Ujue ukitaja neno profesa nachukia sana.

Ona tafiti zao zinavyoumiza watu.
1. Mkandala na kikosi kazi chake
2. Manyele kachezea wananchi kama Mayele


Uprofesa umenajisiwa
 
Back
Top Bottom