Tanzania imefika pabaya sana, nchi za magharibi zikimwaga silaha nchini na kuweka vikundi vya waasi, vijana wataunga mkono kwa wingi dhidi ya serikali

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Wenye mamlaka wanalo la kujifunza japo ngozi nyeusi ni vigumu sana kutokujimwambafy pale wanapopata madaraka.
Hakika huku mtaani kila ninapopita vijana wanashangilia na wanaona kama USA na washirika wake hawajachukua hatua stahiki inabidi aongoze vikwazo au kama walivofanya Libya, kuna baadhi ya vijana kati ya ambao tulikuwa tunapiga nao stori kijiweni wao wanasema wamepitia JKT na wanasema kama ikitokea kama Libya hapa nchini wao wako tayari Kushika SMG na AK47 kupigana dhidi ya serikali yao. nanukuu baadhi ya maneno yao "Tatizo ni serikali hapa acheni kujiuma uma!, Kwanini nimchukie beberu anaye muhimiza kiongozi wangu asiniteke wala kuniuwa???, Nikiwa mtekwaji/muuliwaji mtarajiwa, beberu huyo kwangu ni mkombozi tutaungana nao porini kama ikitokea"
Ni habari ya kusikitisha kabisa lakini ndiko tulikofikia.

Viongozi angalieni namna mnavyotawala hata kama si leo iko siku mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi, watu wanaonekana kuwa na manung'uniko mengi wanasubiri litokee la kutokea waoneshe hasira zao. Acheni kuwasikiliza hao wanaowapaka mafuta kwa mgongo wa chupa eti kila anaelalamika ni MPIGA DILI, Nyumbu, mara vyeti feki, mhujumu, katumwa na mabeberu, si mzalendo na majina mengine yasiyofaa huku wao lengo lao ni kujineemesha.


Serikali zetu nyingi za kiafrica kiukweli kabisa kama wazungu wasingekuepo kuingilia Kati basi raia tungepata tabu sana.Waafrica wengi hatuna roho ya utu hasa tukishika makali. Afadhari wazungu wanatufanya tuwe watu kidogo Kwanza wasingekubali kuondoka madarakan asilani.Mfano, Seseko Moboto,Charles Taylor, Kagame, Museveni, Nkurunzinza na Raisi wa zamani wa Chad, Hawa ni mifano tu. na hapa nashawishika kusema kwamba kama Western world isingekuepo Hali ya siasa zetu zingekua zakinyama sana!! kuna wakat mwingne hatustahili kuwachukia ni wasulihishi wetu mambo yanapokua Mrama!!


Mimi ni mlalahoi tu ila kwa ninayoyaona na kuyasikia huku mtaani serikali ijenge umoja wa kitaifa na kuwarudisha watu wake pamoja bila migawanyiko iliyoko sasa ni mibaya adui akituingilia ni rahisi kutumaliza.
Asubuhi njema
 
Mmh watanzania hawa ninao wajua eti wakapigani subutu acha uwongo wewe kijana


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mbona kuna wanaokamatwa wakienda kujiunga na shababi iweje uwe uwongo.Mbona kuna wengi wanasumbua na masilaha mitaani kila kukicha.
 
U-Z-A-L-E-N-D-O na sio ule wa kuvaa mibendera kwenye shati bali ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Mzalendo wa kweli daima anaweka maslahi ya nchi mbele na ya kwake binafsi nyuma.

Kwa maana hiyo hapo juu, mzalendo ni mtu yeyote mzawa na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unabeba dhana nyingi sana ikianzia asili, utamaduni, lugha, siasa, historia, nk.

Dhana zote zikifungwa kwenye dhana kuu ya utaifa. NADHAN HAPA KAMA TAIFA INABIDI TUJIANGALIE UPYA TOKA HUKU CHINI
 
cmoney,
Shida sasa hivi neno uzalendo linatumika vibaya, kwamba usipokuwa mfuasi wa chama tawala basi wewe si mzalendo! Ukitoa maoni mbadala kwa utawala basi wewe si mzalendo!

Mbaya zaidi vijana tumeshalishwa sana hili neno kisiasa na tumelishiba haswaaa!
 
Hata wewe mleta mada unavyoongea ni kama vile ukipewa Silaha utaingia vitani kama muasi!
Any way hata hizo Nchi unazozitaja wanatamani kuondokana na vita lakini wanashindwa!

Jambo la pili ufahamu kushika mtutu wa bunduki kama muasi hakutakukutatulia changamoto zako zaidi ya kuishia kuishi porini maisha yako yote! Ingawa nakubaliana na na wewe kwamba watawala waangalie namna yao ya kutawala lakini hilo la vijana kushika mtutu bado kutawafanya waendelee na shida zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uongo hakuna kijana anaweza kushika silaha apambane na serikali.

Hawa wanaotawanywa kwa maji na mabomu ya machozi?!

Wanaanzaje sasa?!
 
Nimezaliwa bongo nimekulia bongo..
Wabongo nawajua vizuri.. hakuna wa kupigana na mtu wala kushika mtutu...
Na hiki ndicho kinafanya walevi wa madaraka wazidi kutoa kauli tata wakiamini kuwa hakuna wa kuthubut hili. Yamkini na Gadaffi aliamini hvhv kuwa hakuna mlibya anayeweza kushika silaha dhidi yake.
 
Na hiki ndicho kinafanya walevi wa madaraka wazidi kutoa kauli tata wakiamini kuwa hakuna wa kuthubut hili. Yamkini na Gadaffi aliamini hivihivi kuwa hakuna Mlibya anayeweza kushika silaha dhidi yake.
kabisa
 
Kwahiyo mawazo yako yameona ivyo pia unakubaliana na icho kitu usikubali kupata asara Mara mbili siku zote Kwani itakugharim kama now unaona hufaidiki na chochote muombe mungu akusaidie kaka ila sio hayo mnayo yafuraia pakiwa na kikund cha uas watao faidikia ni waasi serekal na Hao wazamin walio zamin waasi ila wewe na mm matatizo yetu yatazid Mara Mia ya apa yalipo Sasa tusifanye vitu kama vile hatujui kinin kitatokea ikiwa kama tunavyo taka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaio mawazo yako yameona ivyo pia unakubaliana na icho kitu usikubali kupata asara Mara mbili siku zote Kwan itakugharim kama now unaona hufaidiki na chochote muombe mungu akusaidie kaka ila sio hayo mnayo yafuraia pakiwa na kikund cha uas watao faidikia ni waasi serekal na Hao wazamin walio zamin waasi ila wewe na mm matatizo yetu yatazid Mara Mia ya apa yalipo Sasa tusifanye vitu kama vile hatujui kinin kitatokea ikiwa kama tunavyo taka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wapi nimefurahia hebu soma vizuri
 
Wenye mamlaka wanalo la kujifunza japo ngozi nyeusi ni vigumu sana kutokujimwambafy pale wanapopata madaraka.
Hakika huku mtaani kila ninapopita vijana wanashangilia na wanaona kama USA na washirika wake hawajachukua hatua stahiki inabidi aongoze vikwazo au kama walivofanya Libya, vijana wawili kati ya ambao tulikuwa tunapiga nao stori kijiweni wao wanasema wamepitia JKT na wanasema kama ikitokea kama Libya hapa nchini wao wako tayari Kushika SMG na AK47 kupigana dhidi ya serikali yao. Ni habari ya kusikitisha kabisa lakini ndiko tulikofikia.

Viongozi angalieni namna mnavyotawala hata kama si leo iko siku mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi, watu wanaonekana kuwa na manung'uniko mengi wanasubiri litokee la kutokea waoneshe hasira zao. Acheni kuwasikiliza hao wanaowapaka mafuta kwa mgongo wa chupa eti kila anaelalamika ni MPIGA DILI, Nyumbu, mara vyeti feki, mhujumu, katumwa na mabeberu, si mzalendo na majina mengine yasiyofaa huku wao lengo lao ni kujineemesha.

Mimi ni mlalahoi tu ila kwa ninayoyaona na kuyasikia huku mtaani serikali ijenge umoja wa kitaifa na kuwarudisha watu wake pamoja bila migawanyiko iliyoko sasa ni mibaya adui akituingilia ni rahisi kutumaliza.
Asubuhi njema
Una mawazo ya kisengerema kweli. Hivi watanzania wapumbavu kama wewe unavowaza!
 
Back
Top Bottom