Ndugu wana JF, kwa maoni yangu na kwa kuangalia upepo wa kisiasa unavyoenda hapa tanzania, ni kama chama shindani dhidi ya chama kinachoongoza serikali (CCM) kimebaki kimoja tu, yaani, Chadema.
1. CUF waliamua kujiunga na ccm kuanzia zanzibar na kuelekea tanzania bara.
2. Baadhi ya vyama shindani vlivyoamua kujitoa kwenye mchakato wa uchaguzi viliwahamasisha wanachama kukiunga mkono chama tawala kwenye mchakato wa kampeni mwaka jana. Hivi vyama vilipoteza sifa ya kuwa vyama shindani.
3. Baadhi ya vyama (wabunge wa vyama hivyo) walishirikiana na wabunge wa CCM kubadilisha vifungu vya kanuni za kudumu za bunge ili wakidhibiti chadema. Chama shindani kinaposhirikiana na chama kinachoongoza serikali kwa sababu ya kukidhoofisha chama shindani kingine, chama hicho pia kinakuwa kimepoteza sifa muhimu ya kuwa chama shindani.
4. Katika yale, ambayo chadema wanaona ni maslahi ya wananchi na wana wajibu wa kuikosoa serikali kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kufanya mikutano na maandamano, vyama kadhaa vimeungana na serikali kukikosoa chadema hata kuomba kifutwe. Vyama hivi navyo vimepoteza sifa ya kuwa vyama shindani.
5. Vyama shindani ni vile vinavyotoa changamoto kwa serikali ili iweze kuwajibika zaidi na kuleta maendeleo ya watu na vitu na siyo vile vinavyoi'fan' serikali ili izidi kulala usingizi.
kuna msemo unaosema kwamba utawala uliogawanyika hauwezi kuwa na nguvu - kwa maana kwamba kama vile ilivyo 'military strategy' kukabliana na 'common enemy', ndivyo pia ilivyo kwa siasa. Kama vyama shindani vinaungana na chama tawala haviwi tena na mlengwa mmoja (CCM) bali pia Chadema au zaidi sana mlengwa wao amekuwa Chadema. kwa namna nyingine (kwa kufanya hivi) CCM na vyama vingine vinakilenga chadema na kwa jinsi hiyo kukipa chadema nafasi kubwa ya kuwa na sifa ya chama (potential) kuongoza serikali.
q: Mna maoni gani?