Tanzania ili kupaisha uchumi wa nchi tunapaswa kuboresha nyanja zifuatazo

Frankmapuga

New Member
Jul 14, 2021
1
20
Tanzania ili kupaisha uchumi wa inchi tunapaswa kuboresha nyanja zifuatazo .Utawala Bora ,Afya,Kilimo,ukusanyaji wa kondi,Uhuru wa vyombo vya habari,bunge nk,Siasa safi,Amani. nk.

1. UTAWALA BORA; kuwa na uongozi unaozingatia sheria na misingi ya maadili,kukemea ubadhirifu,rushwa,unyanyasaji na kushirikisha wananchi katika maamuzi.

2. AFYA; Kila mtanzania anahaki yakupata huduma bora za afya bila kubagu jinsia kabila,umri,rangi,itikadi ya kisiasa au dini,uremavu hivyo serekali iweke jitihada za maksudi kuimalisha upatikanaji wa dawa,vifaa tiba,miundombinu kwenye zahanati,vituo vya afya hospitali,kuongeza wafanyakazi pamoja na motisha,mishahara kwa wafanyakazi Ili kusaidia kutoa huduma nzuri na bora pamoja na kusimamia na kushawishi kila mtanzania apate bima ya afya Ili kuweza kupata matibabu kwa urahisi na kwa haraka bila upendeleo.

3. KILIMO; kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa hivyo serikali haina budi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kilimo bora chenye tija,kama vile kilimo cha umwagiliaji ambacho hakitegemei msimu wa mvua,zana bora za kilimo,mbegu bora na mazao yenye kuinua uchumi wa mwananchi,kuweka usawa kwenye bei ya mazao ili kumpa mkulima hali na nguvu ya kuendelea kuzalisha mazao bora yenye ushindani kwenye soko la dunia.

4. TEKNOLOJIA; watanzania wote kuishi kwa kutumia techologia ikiwa ni pamoja na kutumia vyuo kutoa wataalamu wa kila nyanja ya technology na kuwaajiri kwenye viwanda vyetu Ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa bora zenye ushindani kimataifa.

5. ELIMU;swala la elimu ni mtambuka,mitaala ya elimu iboreshwe ili iweze kuzalisha wanafunzi na wataalamu watakao weza kujiajiri na hivyo kupunguza changamoto ya ajira nchini, hivyo nchi itasonga mbele kiuchumi.

6. UHURU WA HABARI; kimsingi kila mwananchi anayo haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati,wandishi wa habari wawe na Uhuru wa kukusanya habari kwa kuzingatia taaluma,weredi na ufanisi,asanifu wa habari kabla haijamfikia mwananchi,kuwepo na Uhuru wa kupata habari bungeni mubashara.

7. UKUSANYAJI KODI; ukusanyaji kodi ni nguzo muhimu katika kujenga uchumi imara wa taifa letu,hivyo elimu itolewe kwa mwananchi mlipa kodi,mfanyabiashara na watumishi wa umma,kuwepo kwa usawa katika ulipaji kodi, kuepuka matumizi ya mabavu na vitisho kwenye ukusanyaji wa kodi.

8. SIASA SAFI; taifa linapaswa kuwa na siasa safi inayohudumia haki,msingi,amani usawa kuheshimiana,ukweli na uwazi hizi ni tunu za siasa safi,hivyo mwanasiasa safi ni yule anaetambua dhamana na wajibu wake kwa jamii,kujenga na kudumisha umoja na mshikamano kwa jamii.

9. AMANI; amani ni tunu kubwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda kwa nguvu zote amani tuliyonayo kwa kuepuka kuchochea vurugu,kutii sheria bila shuruti,dini na majukwaa yote ya kisiasa zi/ya hamasishe amani na upendo.

#frankmapuga +255625045696
All right received.#jamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom