Tanzania ikipata viongozi wazarendo ndani ya miaka 20 yaweza kuwa sawa na nchi za ulaya na amerika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ikipata viongozi wazarendo ndani ya miaka 20 yaweza kuwa sawa na nchi za ulaya na amerika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nkundwanabhake, Oct 23, 2012.

 1. N

  Nkundwanabhake New Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote napenda kuwapongeza wana Jf kwa kuendeleza kile kinachoitwa "uhuru wa fikra",nimekuwa mfuatiliaji wa maoni katika jukwaa hili. Kwa mara ya kwanza najiunga na forum hii kama Mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu na mada hiyo hapo juu baada ya kutafiti na kugundua kuwa nchi yetu inapungukiwa na uongozi bora na ndiyo maana hatuendelei kwa spidi inayotakiwa tangu tuwe huru kuanzia mwaka 1961.

  Tuna Raslimali za kutosha kuijenga nchi hii iwe sawa na nchi nyingine zilizoendelea, Mungu ametupatia mali asili hizi ili nchi yetu iwe mahali bora pa kuishi, kwa sababu ya kuwa na viongozi Wabinafsi wengi, hawa wachache wasio wabinafsi wanapojaribu kusukuma ili mambo yafanyike wanashindwa kwa sababu ya mfumo ama "System".

  Hapa kinachotakiwa kwa Watanzania Wazarendo, wanaoumia kwa madudu yanayoendelea katika nchi hii ni kubadili Mfumo uliopo ama utawala uliokwishakita mizizi kwa muda mrefu na kujisahau.Tuna Madini ya vito, tuna dhahabu, tuna almasi tuna mbuga za wanyama kibao na sasa mafuta ya Gesi, Mungu atupe nini zaidi?

  Lazima Watanzania tufanye maamuzi magumu ya kuondoa mfumo uliozoeleka tangu uhuru, tuondoe hofu ya kuvunjika amani, hatuwezi kuendelea hivi ati kwa kuogopa kusababisha vita, nani atakayeleta vita?

  Lengo langu hapa ni kwamba tuondoe Mafisadi kwenye mfumo wa utawala halafu bila kujali vyama tuweke watu waadilifu kwenye mfumo wa Utawala, utaona matokeo yake ndani ya miaka 20 ijayo, Tanzania itakuwa nchi bora ya kuishi.
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  ni kweli endapo hata hao watakaopewa haya madaraka hawatakuwa vigeugeu maana afrikan politicians wanajijua wenyewe.yes we can if we dare!
   
 3. J

  Jalem JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkubwa karibu sana uwanja wa mawazo na fikra pevu za kujenga nchi na watu wake, uzi wako ni kweli lkn wadanganyika wako wengi na wanadanganywa na wana system ili kulinda maslahi ya wachache, lkn one day yes, tutapata mtu atakae tutoa kimasomaso,

  Tutakuwa si nchi maskini kama wanavyo imba ambao ni matajiri katika biashara kuu ya siasa za kimitandao, nilifika Uganda hivi karibuni, nikaona jinsi nchi ilivyo na amani, ujambazi hakuna, rushwa hakuna au kidogo sana kilinganisha na kwetu, wanajeshi na polisi wako barabarani wakifanya kazi wa ulinzi na usalama kwa pamoja,

  Lkn kwetu nani atawaonea huruma wa TZ kama nchi za wenzetu? Rwanda imetoka vitani lkn leo wako mbali, sisi tupo tumelala tu.
   
 4. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wazo lako ni zuri sana, lakini utakelezaji wake ndiyo mgumu...hasa ni kiwa na maana njia ya kuwaondoa hawa mabwana. ambao kwa mfumu tulio nao ni kwa njia ya kura, lakni njia hii imekuwa si muafaka sana kutoka na mambo mengi tu kama uchakchuaji na rushwa ambayo imeota mizizi mpaka mkuu wa kaya naye kabai kulalamika bila kujua nini cha kufanya...hivyo tuna kazi kubwa sana kufika kwenye ukweli huu
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Naona kama utakuwa umeenda mbali saana! Miaka 20 sio mchezo, tukipata viongozi serious ni miaka minne tuu ndugu!
   
 6. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Without vission people perish! Viongozi wetu wengi hawana vission, kufupi ni kuwa taifa letu kwa sasa linaangamia!
   
 7. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  aisee viytu ni vingi vya kutufanya sie tuwe juuuuu angalia tu bandari jamaa wanavyoichezea imefika mpaka police kuiba mizigo ya wazambia ....
  kenya wanalima mirungi wanauza somalia na uarabuni eti kwetu ni dawa za kulevya....angalia bangi kuna mashamba yameteketezwa tanga lakini wenzeti uk na nchi nyingine wametenga sehemu ya kuvuta ....angalia mkaa wanazuia njiani lakini msituni wanachoma ikishikwa wanauza wao waserikali

   
 8. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,391
  Likes Received: 1,360
  Trophy Points: 280
  Hapo juu utakuwa umekosea sana. Tangu uhuru mwaka 1961 nchi yetu inapungukiwa na viongozi bora? Yaani hata Nyeyere na Mkapa si viongozi bora??? Mh! Labda sijakuelewa sawasawa. Juzi juzi kwenye kumbukumbu ya kifo cha Nyerere ITV waliendesha mdahalo mkubwa sana wa kumkumbuka kama kiongozi bora aliyewahi kuwapo katika nchi hii... Leo unasema hatuna viongozi bora? Imeniuma sana......
   
 9. Super H

  Super H JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 1,004
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu unamawazo poa sana ila kuna vijana wa tanzania ambao wameapa kuitetea ccm na mafusadi kwa garama yeyote na humu wamo wanalambishwa vijipesa kidogo tu wanashinda hapa jf kutetea mafisadi,na nilivyokuwa si muoga naweza kukutajia wachache.
  1 :ritz
  2 .rejeo
  3.ngoromiko
  4.tume ya katiba
  5.
  6.
   
 10. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,391
  Likes Received: 1,360
  Trophy Points: 280
  Weweeeeeee! Acha kulinganisha Tanzania na Rwanda. Kanuni zinazotumika Rwanda haziwezi kutumika Tanzania. Mtaziita ni u-dikteta! Rwanda amri ni moja.... Hakuna kubembelezana na wala hakuna longolongo. Watu wanafanya kazi usiku na mchana (wanatoka jasho), lakin Tanzania watu wanapenda maisha mazuri bila ya kuyafanyia kazi. Sasa hapo utalinganishaje na Rwanda?
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  nimeamua nikugongee 'like' ya kwanza kabisa kukukaribisha jamvini, karibu.
  Unasema ni mtz mwenye uchungu, kama ni kweli je hii ID yako ndio jina lako halisi? Nakuwa na wasiwasi na observations zako kwamba inweza kuwa kama nchi za Ulaya, hiyo unabase kwenye rasilimali tu lakini unasahau kuwa rasilimali vitu na rasilimali watu(akili) ni vitu viwili tofauti. Unadhani miaka 20 inatosha kubadilisha akili ya Watz kuwa sawa na Ulaya?
  Kumbuka kuna nchi zingine Afrika zina rasilimali lakini matatizo ni kama yetu. Nakushauri utoe mfano mdogo tu kwamba "tunasweza kuwa kama Angola, Ghana, Kenye nk"

   
 12. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,391
  Likes Received: 1,360
  Trophy Points: 280
  Jadili hoja iliyoko mezani wewe na si kujadili watu!!! Watu wanaitetea CCM ni watu wanaoona mbali sana. Mfano mwaka 1995 kama CUF ingeingia ikulu leo hii waarabu wangekuwa wamesharudi kututawala.

  Vivyo hivyo kama CHADEMa WANGEINGIA MADARAKANI MWAKA 2005 AU 2010 ukabila ungekuwa umeshatawala nchi hii. Watu tunaotoka makabila mengine ambayo si kaskazini tungetafuta pa kukuimbilia maana ni ukabila kwa kwenda mbele.

  Mfano, angalia majina ya wabunge wa kuteuliwa wa CHADEMA halafu jiulize, ina maana kaskazini tu ndo kunatakiwa wapatikane wabunge wa kuteuliwa wa CHADEMA?
   
 13. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bila kuwekeza kwenye rasilimali watu hakika hatutatoka katika hili tope zito tulilokwama madini na vitu vingine hakika haviwezi kuwa suluhisho la mkwamo wetu tumeona mikataba ikitiwa sahihi na watu husika pengine bila kuisoma na kutanguliza maslahibinafsi
   
 14. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Ukweli unabaki pale pale kwamba nchi hii ya Tanganyika inahitaji madiliko makubwa sana ya kimfumo ili tuweze wote kuifaidi keki ya taifa letu. Tatizo ni je, ni nani wa kubadilisha huu mfumo? Tunawahitaji watu wenye sifa adhimu za kizalendo kama Mwl Nyerere, Sokoine, Kawawa. Je, Tanganyika ya sasa watu wa aina hiyo wapo? Tujadili
   
Loading...