Tanzania ikipata vijana wachochezi wa hoja kama kina Zuberi Zitto wakutosha tutarajie hamasa kubwa ya mabadiliko kama ilivyo kuwa kwa enzi za Mwalimu

Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
468
486
Ndugu wana jamii forum habarini saana.

Nimekuwa nikimsikiliza muheshimiwa kabwe zuberi mara kadhaa wa kadhaa katika kipindi chake chote cha uongozi ntangu akiwa mwana chama hodari wa chama cha cdm enzi hizo.

Kiukweli ni kijana mwenye uwezo wa kujenga hoja na anaye juwa kuzipambanua hoja kindakindaki kitu ambacho kime mjengea heshma kubwa katika duru za siasa nchini tanzania kwa miaka ya hivi karibuni.

Leo nimejaribu kumsikiliza kwenye press aliyo itisha leo tar 26 /3/2019 nime jiridhisha kabisa kwamba kama Tanzania inge pata vija wakutosha wa aina ya zuberiz zito, naamni tanzania ingekuwa ni nchi ambayo haiwezi kuongozwa tu matakwa na fikra za viongozi bali ingeliongozwa pia kwa kiasi kikubwa na matakwa ya wana nchi.

Nasema hivyo kwasababu nimegunduwa kitu kwamba tanzania kwa sasa inahitaji viongozi wenye kuamsha hisia za kijasiri na kujiamini kwa jamii ya kwamba wao wana weza, mawazo yao yana nguvu ya kufanya mageuzi hata wakati wanapo pitia kwenye mazingira yanayo watia hofu kiasi gani, na hii ndiyo sifa pekee aliyo kuwa nayo mwalimu nyerere na kizazi cha wakati ule wamapambano.

Vijana wa aina ya zito wakipewa jukwaa na ulingo sawasawa wa kisiasa basi wanaweza waka amsha ari mpya na hamasa kwa vijana kitu ambacho ama kwa upande mwingine wa watawala kinaweza kikawa na matokeo tofauti kwasababu wao wana amini nchi hii ni yao na hivyo sisi wengine hatuna hisa kwwnye milki ya fahari na ving'ora badala yake sisi ni tabaka la watawaliwa wasio na haki hata ya kutoa hoja zenye mashiko kwa maslahi ya taifa letu.

Kikweli tanzania inahitaji watu kama kina kabwe zito, mh tundulisu na wengine wengi ambao wanaweza waka leta mabadiliko ya kifikra yaliodumu muda mrefu ya kwamba ukiwa na hoja ya msingi alafu uko nje ya serikali basi hauna tija nakwamba wewe ni mpiga debe na zumari tu, hujui unacho kifanya wala kusema kwasababu tu uko nje ya mfumo wao.

Hongera saana muheshimiwa zito lakini na mungu akupe ujasiri wa kuendelea kukisimamia unacho kiamini na mwisho jaribuni kuzipandikiza hisia hizi kwa vijana wengi nchini ili ifikie wakati taifa letu liongozwe kwa mujibu ya sheria nzuri tunzao zitunga sisi wenyewe lakini pia viongozi wetu watao tuongoza hapo baadaye wakae wakijuwa ya kwamba nguvu na dhamana walizo nazo zina toka kwa wana nchi ,

wasijsahau wakadhani nchi hii ni mali yao na familia zao au mali ya taasisi wanazo ziongoza hata kama wamepewa nafasi na taasisis hizo. Hapo ndipo tutakuwa tumejenga taifa lenye nguvu na ustaarabu unao amini katika utu sawa uwezo haki na manufaa ya wote kwa wote, kitu kitacho tufanya tufanye kazi kwa bidii na umoja tukiamini katika nguvu moja yenye kuleta furaha kwa wote bila ya kujali dini au rangi ya ngozi zetu.

Na huo ndio utakuwa mwanzo wa kuendelea kwasababu hakuna jamii inayo weza kuendelea bila kuwa na umoja wa kitaifa katika mambo yote yawa tengayo, bali huunganishwa kwa kuondoa tofauti katika manbo yote yawatofautishayo ili waijenge nchi yao kwa umoja na nguvu na sivinginevyo.

Mungu akubari sana awabariki na wote wenye maono kama yenu, mnacho kipanda leo hakika kita mea hata kama ni kwa kuchelewa, na daima mbegu ichelewayo kumea hudumu zaidi imeapo.

Chilemba wa mela pamputi .

sent by galax s9
 
Tanzania inawahitaji vìongozi wasio na uoga kama Mh.Zitto.huyu mfugaji anakotupeleka siko .anataka kutuswaga kama ng'ombe wa chattle haiwezekani.Tukatae kama watanzania.
Ukiwazuia watu kufanya shughuri zao halali za kisiasa zipo kwa mujibu wa katiba na sheria unawafanya watufute njia mbadala.
 
Zito ni Jembe na anajua kucheza na siasa .

Siasa imara ni lazima zijengwe kiitikadi kama anavyofanya Zito.

Tumuunge mkono ili Tanzania ipate vyama Mbadala vyenye nguvu na ushawishi kwenye jamii.

Bila Upinzani imara wenye kuweza kuzuia dhulma za kisiasa ,kijamii na kiuchumi CCM watakua wabaya kuliko Wakoloni.
Kutawaliwa kikatili na watoto wetu ,wadogo zetu na ndugu zetu tunaoishi nao kwenye nchi moja huku tukiwa tunawapigia makofi na vigelegele ni kosa kubwa sana na ni hatari kwa vizazi vyetu kuliko wakati wa mkoloni Mweupe ambaye ilikua ni rahisi kumkimbia kwa sababu hakua ndugu yetu.

Ni lazima tuikatae CCM na dhulma zake zote ili tuwe na watawala wenye kujenga usawa na utu kwenye Taifa.

Tuwaombe viongozi wa dini watoe Tamko la kulaani dhulma zinazofanywa wakati wa uchaguzi zinazopelekea watu wema wasio na hata kuuawa kwa ajili ya kuwapa waovu madaraka.
Tukatae watu waovu kupata madaraka kupitia mateso na damu za watu wema.
Tuanze na Nasari 2020 out.
Na wengine kama Mtulya, moleli, Chixa ,waitara, na wengine waliopata ubunge kisanii.Wote out kwa kuwanyima kura. Kila MTU apate nafasi kwa haki ili awatumikie wananchi kwa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanasiasa pekee kutoka upinzani ninaye muamini.ukitakujua jamaa ni bora angali katika awamu hii ya 5 mijadala mingi na mizito ya kuikosoa serikali yeye ndiye anayeianzisha.
 
Ndugu wana jamii forum habarini saana.

Nimekuwa nikimsikiliza muheshimiwa kabwe zuberi mara kadhaa wa kadhaa katika kipindi chake chote cha uongozi ntangu akiwa mwana chama hodari wa chama cha cdm enzi hizo.

Kiukweli ni kijana mwenye uwezo wa kujenga hoja na anaye juwa kuzipambanua hoja kindakindaki kitu ambacho kime mjengea heshma kubwa katika duru za siasa nchini tanzania kwa miaka ya hivi karibuni.

Leo nimejaribu kumsikiliza kwenye press aliyo itisha leo tar 26 /3/2019 nime jiridhisha kabisa kwamba kama Tanzania inge pata vija wakutosha wa aina ya zuberiz zito, naamni tanzania ingekuwa ni nchi ambayo haiwezi kuongozwa tu matakwa na fikra za viongozi bali ingeliongozwa pia kwa kiasi kikubwa na matakwa ya wana nchi.

Nasema hivyo kwasababu nimegunduwa kitu kwamba tanzania kwa sasa inahitaji viongozi wenye kuamsha hisia za kijasiri na kujiamini kwa jamii ya kwamba wao wana weza, mawazo yao yana nguvu ya kufanya mageuzi hata wakati wanapo pitia kwenye mazingira yanayo watia hofu kiasi gani, na hii ndiyo sifa pekee aliyo kuwa nayo mwalimu nyerere na kizazi cha wakati ule wamapambano.

Vijana wa aina ya zito wakipewa jukwaa na ulingo sawasawa wa kisiasa basi wanaweza waka amsha ari mpya na hamasa kwa vijana kitu ambacho ama kwa upande mwingine wa watawala kinaweza kikawa na matokeo tofauti kwasababu wao wana amini nchi hii ni yao na hivyo sisi wengine hatuna hisa kwwnye milki ya fahari na ving'ora badala yake sisi ni tabaka la watawaliwa wasio na haki hata ya kutoa hoja zenye mashiko kwa maslahi ya taifa letu.

Kikweli tanzania inahitaji watu kama kina kabwe zito, mh tundulisu na wengine wengi ambao wanaweza waka leta mabadiliko ya kifikra yaliodumu muda mrefu ya kwamba ukiwa na hoja ya msingi alafu uko nje ya serikali basi hauna tija nakwamba wewe ni mpiga debe na zumari tu, hujui unacho kifanya wala kusema kwasababu tu uko nje ya mfumo wao.

Hongera saana muheshimiwa zito lakini na mungu akupe ujasiri wa kuendelea kukisimamia unacho kiamini na mwisho jaribuni kuzipandikiza hisia hizi kwa vijana wengi nchini ili ifikie wakati taifa letu liongozwe kwa mujibu ya sheria nzuri tunzao zitunga sisi wenyewe lakini pia viongozi wetu watao tuongoza hapo baadaye wakae wakijuwa ya kwamba nguvu na dhamana walizo nazo zina toka kwa wana nchi ,

wasijsahau wakadhani nchi hii ni mali yao na familia zao au mali ya taasisi wanazo ziongoza hata kama wamepewa nafasi na taasisis hizo. Hapo ndipo tutakuwa tumejenga taifa lenye nguvu na ustaarabu unao amini katika utu sawa uwezo haki na manufaa ya wote kwa wote, kitu kitacho tufanya tufanye kazi kwa bidii na umoja tukiamini katika nguvu moja yenye kuleta furaha kwa wote bila ya kujali dini au rangi ya ngozi zetu.

Na huo ndio utakuwa mwanzo wa kuendelea kwasababu hakuna jamii inayo weza kuendelea bila kuwa na umoja wa kitaifa katika mambo yote yawa tengayo, bali huunganishwa kwa kuondoa tofauti katika manbo yote yawatofautishayo ili waijenge nchi yao kwa umoja na nguvu na sivinginevyo.

Mungu akubari sana awabariki na wote wenye maono kama yenu, mnacho kipanda leo hakika kita mea hata kama ni kwa kuchelewa, na daima mbegu ichelewayo kumea hudumu zaidi imeapo.

Chilemba wa mela pamputi .

sent by galax s9

Wote wangekuwa protected na state, kama yeye wala usingemsikia
 
Back
Top Bottom