Tanzania ikifunga mpaka wa Namanga na Taveta-Holili, hakika watakiri kuwa Kilimanjaro ipo Tanzania

Joel Johansen

JF-Expert Member
May 12, 2016
242
319
Hivi majuzi kuna mwandishi huko Ulaya alipotosha dunia kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya, TANAPA walipo mfuata akadai waende kwenye Media aliyoitumia kutolea habari hiyo ili wakanushe na sio kumfuata kienyeji.

Nilisoma uzi ule kwa uchungu mkuu (nadhani ilikuwa ni HuffPost News). Wengi walidai kuwa Tanzania ina viongozi ambao hawajali soko la Utalii.

Mchangiaji mmoja akasema, I quote "Kenyans, Tanzania don't care if you are dragged into our business or not, sisi kwetu #HapaKaziTu).

Mwingine ambaye ndio chanzo cha mimi kufungua uzi huu ni aliyedokeza kwamba kama tukifunga mpaka wa Namanga na ule wa Taveta-holili watalii wasiingie, hakika wakenya, watalii na wengi waliolishwa maneno kuwa Kilimanjaro ipo Kenya wataisoma namba na kujua kuwa kumbe kweli #Kili ni Tanzania na Tanzania ni #kili.
 
Mipaka hiyo ikifungwa tutashtakiwa kwa kosa la kuua wakenya kwa njaa. Mahindi, mbaazi, ngwara, vitunguu n.k vitaendaje Kenya? Na kwa jinsi walivyotufanya solo lao la sabuni, biscuits, maziwa ya brookside, spices za tropical n.k watauza wapi? Ukitaka Kenya iwe maskini na utapiamlo wafungie hiyo mipaka.
 
Kufunga mipaka sio ufumbuzi kwa sababu wananchi wa pande zote mbili wataumia kiuchumi, ishu hapo ni sisi kushirikiana na majirani zetu kuutangaza utalii wa mlima kilimanjaro
 
Nasikia hadi Uingereza KUNA matangazo yanayoelekeza watalii wafike Kenya kuuona Mlima Kilimanjaro. Lakini wakibanwa wanajitetea kuwa hawajasema watalii wafike Kenya Kupanda Mlima Huo Bali wamesema wafike Nchini kwao kuuona Mlima Kilimanjaro. Na kweli unaonekana pia kutokea Kenya!!
 
Hivi majuzi kuna mwandishi huko Ulaya alipotosha dunia kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya, TANAPA walipo mfuata akadai waende kwenye Media aliyoitumia kutolea habari hiyo ili wakanushe na sio kumfuata kienyeji.

Nilisoma uzi ule kwa uchungu mkuu (nadhani ilikuwa ni HuffPost News). Wengi walidai kuwa Tanzania ina viongozi ambao hawajali soko la Utalii.

Mchangiaji mmoja akasema, I quote "Kenyans, Tanzania don't care if you are dragged into our business or not, sisi kwetu #HapaKaziTu).

Mwingine ambaye ndio chanzo cha mimi kufungua uzi huu ni aliyedokeza kwamba kama tukifunga mpaka wa Namanga na ule wa Taveta-holili watalii wasiingie, hakika wakenya, watalii na wengi waliolishwa maneno kuwa Kilimanjaro ipo Kenya wataisoma namba na kujua kuwa kumbe kweli #Kili ni Tanzania na Tanzania ni #kili.

Tukifunga mpaka Tanzania itapelekwa The Hegue kwa kosa la kuua Raia wa Kenya wakati tunajua wazi hawana chakula cha kutosha.
 
me naona bora tuuhamishie dodoma mlima wetu kilimanjaro mana kuna sehemu ukiwa kenya unauona vizuri sana mpaka raha.
 
Tanzania pia inafaidika na huo mpaka, tusiangalie upande mmoja tu.

Na pia uzembe upo kwa viongozi wa Tanzania, wamebweteka wakisubiri watalii waufahamu huo mlima wakiwa ndotoni.

Tusiwalaumu Kenya, tujilaumu sisi pia.
 
KUFUNGA MPAKA ITAKUWA NI LOOSE-LOOSE SITUATION KWA KUWA MADUKA YETU YAMEJAZA BIDHAA ZA KENYA. HAWATAUONA MLIMA KILIMANJARO LAKINI NASI HATUTUTASALIMIKA KWA BAADHI YA MAHITAJI. TUNATEGEMEANA
 
Ule mpaka wa Taveta hauwezi kufungwa, kuna bidhaa ya muhimu kule inahitajika kutoka Kenya (wanaume).
He hee hee maajabu sana. Wamechoshwa na ngumi za wanawake wa kenya. wakenya wanakwenda kupumulia Tanzania kuliko na wapole wenye kubembeleza mme
 
me naona bora tuuhamishie dodoma mlima wetu kilimanjaro mana kuna sehemu ukiwa kenya unauona vizuri sana mpaka raha.
hahaa ttb wapuuzi tu hawajiwezi..huo mpaka mtamu sana kama unajielewa, tunapiga zaidi ya milioni tatu kila wiki
 
Sasa mpaka ufungwe halafu iweje ??kazi ya mpaka ni kupitisha watalii tu ?? Serikali iandae program maalumu ya kuitangazia dunia vivutio vyetu sio kila siku tunawalaumu Wakenya na pia waweke mazingira rafiki kwenye vivutio vyetu ,kuwe na paramedics unit na standby helkopters kwa ajili ya emergency ,huenda kungekuwa na Helkopter basi kifo cha yule dereva bingwa wa magari SA kingehepukika
 
Mnalalamika wakati hamna shirika la ndege la kwetu lakuwatoa huko ulaya kuja hapa wakati Kenya airways mshirika namba moja wa sky team airlines alliance anawatoa huko mpaka Kenya wanawambia njoo muone Mt Kilimanjaro baadae wanapelekwa maasai Mara wakimaliza wanamleta tz kuona mlima kwa siku chache kabla awajawarudisha kwao.Kwa kifupi Kuna uhusiano mkubwa wa uimara wa shirika la ndege na kukua kwa sekta ya utalii.
 
Pale kuna biashara nyingi zinaendelea zaid ya mlima kilimanjaro. Na hata tukifunga yawezekana Tz tukapoteza zaid....cz hao watalii hawaji tu kuutembelea mlima kilimanjaro.....kumbuka kenya nao wanavivutio na wanajua kujitangaza kuliko sisi. Kwahyo tukifunga yawezekana watalii wanaokuja kenya wakaishia kenya hapo then wakageuza. Tatizo lipo kwetu, kwanini mkenya akisema mt kilimanjaro ipo kenya anaaminika kuliko sisi? Kwahyo. Afu kumbuka mt kilimanjaro iko karibu na Nairobi kuliko dar.
 
Nafikiri Marketing na Sales person wetu awajaiva vyakutosha
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom