Tanzania Human Rights Commission wamefulia??

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,517
1,367
JF,

Najiuliza- Tanzania Human Rights Commission mbona hatuwasikii? Vipi wamefulia au wanakula tu posho na pesa yetu bure? Ukiangalia Kenya Human Rights Commission they are so active na every day or two utawasikia wanatoa statemets kuwatetee wananchi!

Mimi hawa jamaa Tz sikuwahi kuwasikia hata kutoa statemets over;

1. Watanzania walikufa ktk mgodi wa Buhemba

2. Watanzania wanaopoteza maisha Tarime ktk mapigano ya koo!

3. Watanzania waliopoteza mali na mifugo yao kule Mbarali!

4. Wananchi waliopoteza masisha na na mali zao kwa mabomu kule Mbagala!

Sasa mimi najiuliza nini kazi ya Tanzania Human Rights Commission???

Nini viongozi wake wanafanya?

Au ndo kufulia huko taratibu??

Je huna haja kuendelea kulipwa pesa yetu ya kodi??
 
kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) japo shirika binafsi kinachapa kazi kuliko hawa jamaa
 
kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) japo shirika binafsi kinachapa kazi kuliko hawa jamaa

Ochu,

sasa hawa jamaa wanahitaji kuwepo??

LHRC ni NGO..wanasikika kweli!

Je hawa wanakula kodi zetu bure?

Nini wamefanya tangu waanze kufanya kazi Bara na Visiwani miaka zadi ya 5 sasa??

Je kuna haja wawepo kama hatuoni matokeo ya wanachofanya??

Je haya matumizi mazuri ya kodi zetu??
 
Toka mwanzo nilihisi hii institution itakuwa ya kisanii na sasa naona kumbe dreams zangu zilikuwa real.
Taasisi hii ni usanii na hata isipokuwepo haina maana. Kwani inawajibika kwa nani?
 
Na cha kushangaza zaidi hata kufanya kazi ya uhamasishaji ili watu wawajue kama wapo hawafanyi. Sijui ni dereva ndio mwenye matatizo au wasaidizi wake wakiwamo makamishna. Au ni kwa sababu wanateuliwa na rais kwahiyo basi wanaogopa kuisema serikali ya rais yule yule. Kwa sababu sehemu kubwa ya uvunjaji wa haki za binadamu unafanywa na serikali, ingawa vile vile makampuni binafsi na yenyewe wakati mwingine huhusika na uvunjifu huo wa haki za binadamu. Lakini binafsi nafikiri kuna tatizo la mfumo. Nitajitahidi kutafuta chanzo chao cha mapato pamoja na uwajibikaji wao baada ya kuteuliwa. Kwa sababu kama mapato yao yanatoka serikalini, na wanaweza kuwajibishwa na rais, basi hapo kuna tatizo kidogo. Wanaweza kuwa too subservient to the president and his government and they may be waiting for instructions from the government in order to attend any human right violation. Lakini nawalaumu hata mimi kwa kukaa sana kimya. Hawajulikani. Hatuwaoni. Hatuwasikii. Haki Elimu wana nafasi kubwa sana katika jamii yetu sasa kuliko hata hao makamishna wanaoteuliwa na rais. Hata Tawla wanajitahidi na sasa hivi 'sidanganyiki' imekuwa maarufu
 
Toka mwanzo nilihisi hii institution itakuwa ya kisanii na sasa naona kumbe dreams zangu zilikuwa real.
Taasisi hii ni usanii na hata ispokuwepo haina maana. Kwani inawajibika kwa nani?

Mchukia Fisadi,

tatizo taasisi za serikali ambapo watu wanakula pesa bure zipo tu kibao Tz!!

Tunahitaji tija!

Kama hakuna tija basi zipigwe chini ..ili hii pesa ijenge zahanati au shule!
 
Toka mwanzo nilihisi hii institution itakuwa ya kisanii na sasa naona kumbe dreams zangu zilikuwa real.
Taasisi hii ni usanii na hata ispokuwepo haina maana. Kwani inawajibika kwa nani?

Hii institution haikuanzishwa kwa matakwa yetu bali kwa shinikizo la AU kwa kila nchi iwe na National Human Rights Institution. na hii ili-replace ile tume ya uchunguzi ya kudumu ambayo nayo ilikuwa use less. serikali yenyewe imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya tume kuhusu kesi ya wananchi walichomewa nyumba na mkuu wa wilaya huko serengeti.
 
Hii institution haikuanzishwa kwa matakwa yetu bali kwa shinikizo la AU kwa kila nchi iwe na National Human Rights Institution. na hii ili-replace ile tume ya uchunguzi ya kudumu ambayo nayo ilikuwa use less. serikali yenyewe imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya tume kuhusu kesi ya wananchi walichomewa nyumba na mkuu wa wilaya huko serengeti.[/QUOTE]
Nahisi walitaka kufanya same thing kwa bunge kuhusu maazimio ya bunge kwa serikali kuhusu Richmonduli.
Unfortunately hapa wamekuta kizingiti ambacho wasipoangalia kinakwenda na mtu.
Pinda upo hapoooooooooo??
 
Back
Top Bottom