Tanzania hatuna wanunuzi wala wafanyabiashara wa korosho bali tuna Madalali wa zao la korosho!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Huo ndio ukweli, wale wanaojiita wafanyabiashara wa korosho pamoja na kile chama chao ni kakikundi tu ka madalali.
Nawahakikishia madalali hawa wanaenda kuaibika soon kwani hii hatua aliyochukua Rais Magufuli inaenda kuleta tija kwa Wakulima na taifa kwa ujumla. Korosho inapelekwa sokoni moja kwa moja na mkulima mwenyewe ( via serikali) itakosaje profit margin nzuri?!
Hao madalali kwa kutikisa kibiriti walijisahau kuwa njiti zimejaa.
Kila la kheri serikali yetu!
 
Heee kumbe serikali hainunui tena inawapelekea wakulima sokoni...!!!
 
Jamaa zamani walikuwa wanapata profit kubwa phuku wakulima wakiteketea..sasa wanataka wapate faida kama zamani ambapo korosho walinunua 1700 hadi 2000 kwa kilo..sidhani kama mwakani watatest tena kugomea.maana wengine korosho ndio biashara yao kwa miaka nenda rudi..unadhani mwakani atakubali
 
tapatalk_1541959324648.jpeg
 
Usiangalie issue ya Korosho Kwa kutazama 600 billion Za kununua hizo Korosho Au magari ya Kijeshi kwenda kusomba

Tazama athari yake Kwa Picha pana

Ni Sawa Na tunavyopiga Kelele Kuwa
Athari Za Azimio la Arusha zitaishi Kwa zaid ya Karne Moja Na haya aliongea Hayati Oscar Kambona 1967 akasingiziwa Uhaini ili anyongwe

Nyerere alipora mali Za watu 1967 mpaka Leo Tanzania Investment center wakienda nje kuvutia Wawekezaji swali wanaloulizwa nmeacha lini kupora mali Za watu Kwa njia ya utaifishaji?

Jk aliwahi kuulizwa katika Safari zake zote Za nje ya Nchi kuna swali gani common kaulizwa zaid Na Wawekezaji wa nje alijibu Ni wasiwasi wao kuhusu Azimio la Arusha Kama litarudi Tena

Sasa hivi tutaulizwa nmeacha lini kupanga Bei Za Mazao yenu Na kulazimisha tununue bila ya kujali bei ya Soko la Kimataifa ? Na ukibisha unfutiwa leseni?

Kwenye Masuala ya Uchumi Rais anakosea mambo Mengi Kama alivyokuwa anaboronga Nyerere japo nia zao wote ni njema

Uchumi unaendeshwa Kwa mbinu sahihi sio nia Sahihi - Pohamba
 
Serikali ingeweka mazingira rafikimakampuni makubwa yangekuja kununua Korosho moja kwa moja. Ugumu wa kufanya biashara ndiyo unafanya madalali watokee.
Karibisha makampuni yote makubwa ya kununua korosho na weka mazingira rafiki uone kama hao madalali watasurvive.
 
" Korosho inapelekwa sokoni moja kwa moja na mkulima mwenyewe ( via serikali)".........neno kuntu!
 
Back
Top Bottom