Tanzania hatuna Viongozi tuna Wanasiasa; Maisha ya Kujitakia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hatuna Viongozi tuna Wanasiasa; Maisha ya Kujitakia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Mar 3, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Nchi yetu tunayosema tunaipenda sana (sina uhakika tena) haina viongozi. Hakuna kiongozi hata mmoja wa kujivunia.

  Ila Mungu ametubariki pamoja na maliasili na madini tuliyonayo tuna wanasiasa wengi sana na wazuri. Wanafanya siasa zao vizuri na kiustadi mkubwa wa kisiasa.

  Kila kona ya nchi yetu ina wanasiasa wa kutosha. Ni bahati ilioje tuna wanasiasa wengi kuliko madaktari, wakandarasi, walimu, wanasheria etc.

  Viongozi hatuna. Katika hili msemo kwamba Mungu hakupi kila kitu unapata maana zaidi. Kutokana na uhaba wa viongozi wanasiasa wetu wameitumia hiyo nafasi kutuongoza. Wanajaribu kutuongoza kisiasa.

  Na sisi tunawafuata tukiamini wanatuongoza. Mara zote wanatuingiza kwenye mashimo mbaya zaidi njia wanayotuongoza ni mduara. Tunarudi pale pale.

  Tumekuwa vipofu, hatuoni tunavyodanganywa kwamba tunakaribia kufika. Hatujui tulipo wala tunapokwenda. Kazi nzuri ya siasa.

  Wanasiasa tulionao wote wamefeli katika maisha. Hawana cha kujivunia zaidi ya machache ambayo ni ya kutengeneza. Kwao siasa ndio maisha kwa hiyo wanachojivunia ni siasa!

  Maisha ya mtanzania sio siasa ingawaje wanasiasa wetu wameyageuza siasa!

  Ni hali inayoumiza sana. Mamilioni wanateseka, wanaishi maisha ya dhiki na kudhalilishwa wakati sisi wanasiasa tunafurahi na kushukuru kwa yale Mungu aliyotujalia.

  Watanzania tafuteni viongozi. Achaneni na sisi wanasiasa. Tunawapoteza. Tumewaongoza kisiasa kuanzia 1961. Angalia hali zenu, angalieni za kwetu! Ni nini msichokiona? Ni muda wa kutafuta viongozi na sio wanasiasa.

  Mwenye masikio na asikie. Mwenye macho na aone.
   
 2. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It seems like Viongozi wapo! Labda mimi ndio siwajui. Ngoja niendelee kusubiri!
   
 3. H

  Haika JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni kweli na inasikitisha,
  tutafute mfumo wa kuweka viongozi bora katika nafasi za kuongoza,
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe Haika. Mfumo tulionao unatupatia wanasiasa kutuongoza huku wao wakituaminisha ni viongozi. Hapo ndipo chimbuko la uozo wote kwenye nchi hii.
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Viongozi walikuwepo na wanasiasa pia kwa mfano sokoine, dr. Kleruu na wengineo lkn sasa hivi no viongozi ila ni wanasi hasa ndo waliobaki kwa hiyo ndugu yangu msando we anza kuonesha kuwa wewe ni mwanasiasa na kiongozi pia.
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MsandoAlbeto:

  Umeona eh!! Tofauti ni kubwa kati yetu -wananchi na nyie wenyenchi. Na bado juzi spika wenu kaahidi kuboresha posho zenu mnapokuwa kwenye kazi zenu za kamati ili msichukue bahasha kutoka taasisi / kampuni / mashirika husika. Sijui kama inawezekana, sana mtaongeza usiri ili tusijue.

  Hivi kweli wabunge wetu mnaosema mna uchungu na maisha ya sisi mnaotuita "wapiga kura wenu" mnakubali mkopo wa sh mil 90 kwa ajili ya kununulia magari: Mil 90 (90,000,000/-) kila mtu. Nilitegemea waheshimiwa muwasilishe hoja binafsi kupinga hilo. lakini mmekaa kimya. Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

  Kwa wenye akili watanunua gari za kawaida za mil 30 hadi 40, na pesa zingine watazitumia kwa manufaa ya wapiga kura wao. Mfano tunao: G. Lema. Lakini kwa walio wengi wanaopenda sifa (masharobaro) utawaona wanasukuma VX za ukweli. Sawa bwana wakati ni wenu kuleni nchi yenu.
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Msando toeni kwanza boriti kwenye hayo macho yenu ndo muwe viongozi ka kina sokoine
   
 8. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Our country has too many politicians and too few statesmen. While the statesmen are concerned with the next generation, the politicians are terribly concerned with the next elections.
   
 9. M

  Martin Mollel Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli mkuu
   
 10. S

  SIMPLE X Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ujinga kwa mtanzania kutegemea kuwa maisha bora yataletwa na mwanasiasa, watanzania wengi wanaamini CDM ikichukua nchi kutakuwa na maisha bora hata wakiwa wanakaa kijiweni, hayo ni mawazo ya mgando yasiyo na maana. Kama CCM walivyo hata CDM ndivyo walivyo hata mkipinga kwakuwa mna mapenzi na chama lakn huo ndo ukweli, kwani hao CDM wamezaliwa mbinguni.?

  Kwamuujibu wa John Locke ''man is selfish and greedy'' ni binadamu yupi asiye na tamaa?? Ni binadamu yupi atakaye kufikiria wewe kabla ya kujifikiria yeye na familia yake??. Kitu kingine... wote tunafahamu tabia ya wazungu, mzungu si mpuuzi hawezi akakupa kitu bila kuwa na maslahi na wewe, sasa kwakutumia akili ya kawaida unategemea CDM watawalipa nini OCD wa ujerumani kama si madini kama walivyofanya CCM. We unadhani nchi ikichuliwa na CDM nafasi za kazi hazitatolewa kwa undugu??

  Yani wewe uombe kazi ofisi ya raisi na mtoto wa Mbowe aombe kazi ofisi ya raisi unategemea watamuacha mtoto wa Mbowe wakuchukuwe wewe?? Labda kikubwa ni mabadiliko kwamba labda CDM watakuwa sio wezi sana kama hawa wenzetu wa CCM ila kitu ambacho nataka kuwakumbusha wenzangu matumaini yako ya kimaisha usiyaweke kwa wanasiasa, wanasiasa wengi hawana maana, wamejawa na tamaa pamoja na ubinafsi.
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkubwa kwa hiyo wewe unatoa ushauri gani kwa watanzania wafanye nini ili wajikomboe.
   
 12. P

  Penguine JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Penguine says thank u simple x for this useful remind.
   
 13. d

  dada jane JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mahali umeongea point sana. Only kuwajibika mtu mmoja ni muhimu sana.
   
 14. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe unataka kutuaminisha tuendelee kuwapa kura majambazi wa ccm? au unataka tufanyeje? kikubwa unachotakiwa kuelewa ni kuwa kitumike kihalali wala si kikundi cha watu wachache. ndio maana CDM inapigania huu usawa hatusemi tutakaa vijiweni tu bali maendeleo yatakuja kwa kufanya kazi tukisaidiana na serikali kupitia raslimali tulizonazo
   
 15. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  kweli mkuu...wanasiasa wanatofautiana kauli....malengo yao hushabihiana
   
 16. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  wewe ni miongoni mwa watanzania wengi waliokata tamaaa" hawathubutu kujaribu, hawapigi kura, ukweli ni kwamba wanafanana na aliye jeruiwa na nyoka, wakiona hata mjusi wanaogopa. thread yako haitufundishi chochote!
   
 17. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,120
  Likes Received: 10,471
  Trophy Points: 280
  Ahasnte kwa ushauri......Ila penda usipende T2015CDM....
   
 18. S

  SIMPLE X Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si vibaya kutoa support kwa vyama vya siasa lakini usiweke tumaini lako kubwa huko, mafanikio yatakuja kwakufanya kazi kwa bidii
   
 19. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  kumbe cdm inapigania usawa na si kuchukua madaraka...hata hivyo bado sijajua usawa upi unaoongelea...kama ni mgawanyo wa rasilimali basi tuanzie ndani ya cdm.....chama mapato ni kiasi gani kwa mwezi??.mwenyekiti anapata ngapi?? muhudumu wa ofisi anapata ngapi?..kuna usawa gani??......ni usawa huu mnaopigania??
   
 20. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  ushakata tamaa wewe.
   
Loading...