Tanzania hatuna 5 hotels kwa vigezo vya Kimataifa

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-alaikhoom Wana-JF!

Kuhusu mada iliyopo hapa juu napenda nianze kwa kusema kwamba kama TZ tukiendelea kujidanganya kuhusu mambo mengi ya msingi katika huduma za jamii, dunia itatuacha tu; tukijinasibu kwamba tumeendelea au tunapiga hatua kubwa mbele, kumbe sivyo!

Yafuatayo ni baadhi ya masuala yanayowezesha nchi kukidhi vigezo vikuu vya hotel za Nyota Tano [V HOTELS]:

1. Nyota ya KWANZA inahusu VIGEZO VYA HOTELI ZENYEWE:

USAFI wa watu, mazingira na
UBORA wa HUDUMA za CHAKULA na vinywaji,

MALAZI, huduma za vyumbani (room service), burudani, mazoezi/michezo ya nje na ndani, huduma ya afya ya dharura hotelini, miundombinu ya usafiri na vyombo mbali mbali kwmfn taxi, self drive cars, safe parking and storage facilities nk.

Huduma za mawasiliano ndani na nje ya nchi, kwa simu, fax, email, radio, nk. Huduma za kiofisi, audiovisual meeting rooms na conference facilities etc.

2. Nyota ya PILI inahusu VIGEZO VYA NCHI YENYEWE:

AMANI (political stability) NA TABIA ZA KISTAARABU na UKARIMU kwa kila mtu.

Kusiwe na viashiria vya aina yoyote ya kuvunjika kwa amani kwa muda mrefu nyuma, sasa na wakati ujao.

3. Nyota ya TATU inahusu HUDUMA na INFRASTRUCTURE za NCHI NZIMA:

Uwepo wa usafiri salama na wa haraka ndani na nje ya nchi kwa barabara, anga, maji etc. na kwa mguu, mabasi, texi, treni, ndege, ferry, private car, nk.

4. Nyota ya NNE Inahusu:

Uwepo wa MAJI SAFI na SALAMA YA KUNYWA ya bomba (kwa nchi nzima sio hotelini tu).

Huduma nzuri za kuondosha maji ya mvua na majitaka, kuondosha taka laini na ngumu. Public toilets SAFI za UBORA wa KIMATAIFA nchi nzima.

5. NYOTA YA TANO inahusu Uwepo wa HUDUMA za kibingwa za MATIBABU (consultant level hospital service) na AMBULANCE service za viwango vya KIMATAIFA (reachable within 5 minutes kutoka popote ulipo nchini).

Uwepo wa HUDUMA IMARA na za HARAKA za ZIMAMOTO na HARAKA kama za MATIBABU hapo juu na za viwango vya KIMATAIFA.

Uwepo wa HUDUMA za POLISI wa HARAKA na za UBORA na Usalama kwa watu WOTE wakati WOTE.

Lakini pia haya chini ni baadhi ya mambo yanayofanya nchi isiwe na hoteli zenye UBORA wa KIMATAIFA kwa VIGEZO vya KIMATAIFA kwa nyota 5:

Kwanza kwa nchi kutokidhi vigezo vya mojawapo ya hayo matano hapo juu kunafanya msiwe na 5 hotel YOYOTE inayotambulika KIMATAIFA.

Pili mkiwa na magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kila mara kama kipindupindu, TB nk. corona nk kwa kipindi kirefu. Pamoja na magonjwa ya mifugo kama rabies, anthrax, bovine TB nk. (Hiyo ni dalili za viwango uduni vya mambo mengi katika nchi). Sahauni 5 HOTELS!

Tatu mkiwa na chronic traffic jams ktk njia muhimu kama within 5 minutes to & from airports, from airports to hotels, nk. Iwe kwa taxi, commuter systems, private car, helicopter, subway, tramcar etc.
Five star hotels sahauni!

Nne mkiwa na usafiri aina zote wa mikoani na commuter systems zisizozingatia muda kituo hadi kituo, USAFI wa wahudumu na vyombo husika na Usalama wa abiria, huduma bora za njiani kama chakula, maji, vyoo, nk. Vyote hivyo kwa viwango vya KIMATAIFA;
Hapo hakuna 5 HOTELS!

Tano mkiwa na usafiri usio salama, angani, relini, baharini na barabara mbovu. Na kote huko AJALI za kila leo, au mavumbi NJIA NZIMA, pia ni kikwazo.

Sita mkiwa na sehemu za starehe na chakula chafu, wahudumu wachafu, maji, machafu ya kunywa na kunawa, jiko na vyombo vyake uchafu mtupu; mijini na vijijini, na hii maana yake kuanzia mnavyolima na kuvuna mazao ya chakula, matunda na mbogamboga. Hivyo vyote vinachunguzwa kuhusu USAFI na Usalama na handling, na mnavyosafirisha na kuvifikisha kwa mlaji.
Kama ni business as usual, watu wanshika nyama namatunda kwa mikono, au kubeba nyama begani!
Basi sahauni 5 HOTELS!

Saba mkiwa na msongamano na uchafu wa kila aina ya biashara barabarani, miferejini, kila mahali.
Na hapo basi sahauni 5 HOTELS!

Mwisho nchi isiyozingatia usawa na HAKI kwa WOTE, isiyoheshimu au inayonyanyasa watu wenye misimamo tofauti na wao kidini, kiuchumi, kisiasa; na wenye mahitaji maalum kama walemavu wa kuona, kusikia, kutembea, kusema, ngozi ya mwili, pamoja na masuala ya jinsia, watoto, wazee, nk.
Sahauni 5 HOTELS.

Hayo ni maoni yangu binafsi, lakini ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina na kitaalamu, asiyeyajua haya au asiyeyapenda avumilie tu, hiyo ndiyo hali halisi.

KWA LEO, NA KWA KIPUFI SANA; NAPENDA KUWAWASILISHA!
 
Du weka source ya andiko lako mkuu, Kama ndivyo bado tuna safari ndefu. Dubai Kuna 7 Star hotel Burg Al Arab
 
Ngoja tuendelee kujidanganya maana hata 4G kwa upande wa internet hatuna pia. Tuna 2G na 3G zilizochangamka tu.
Pia Mkapa stadium for international matches ni chini ya kiwango ukilinganisha na viwanja vya vilabu fulani fulani huko mbelembele.
Magari tunayoagiza toka Japan na ulaya na kutamba nayo mtaani kuwa ni mpya huwa ni used tena kwa zaidi ya miaka kumi ila sisi huita mapya- Hii nchi ngumu sana.
Mwisho naunga mkono hoja hatuna 5☀️hapa bongoland
 
Hapa Rubwera Kyerwa Mbona Hotel Ipo Japo Sijajua 🌟Ngapi
 
Hotel nyota tano maanake Ni level ya juu ya huduma za hotel kwa mfano Kuna hotel ambazo hata rais anaweza kulala..mambo ya nchi hayahusiani kbs umetupeleka chaka
 
Back
Top Bottom