Tanzania: Hatukupiga kura sababu tulichotaka kati ya Urusi vs Ukraine hakikutokea!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine

Imesisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo hilo ndilo walilotaka lakini halikutokea.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema: “Katika sera yetu ya mambo ya nje ni kutafuta muafaka, kutumia njia ya diplomasia, lakini hilo halikuwezekana ndiyo maana katika kupiga kura tukaamua kutofungamana na upande wowote.

“Lengo ni kutoa meseji kuwa sisi hatufungamani na upande wowote, hivyo kutopiga kura ni kuonyesha msimamo wa Tanzania.”

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja tangu Umoja wa Ulaya (EU) utoe tamko kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi hadharani.

Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

Source: TBC
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi.

Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga.

Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
 
Naamini huu utaendelea kuwa msimamo wetu daima. Afterall its a "family matter" hatupaswi kuingilia.

Syria, Iraq na Libya hatukulazimishwa na sasa tusilazimishwe tuunge mkono ajenda yao, tuwaachie wenyewe "its a familly matter".

Tanzania tuna maslahi na Urusi na Ukraine na hatupendi kuharibu uhusiano lakini pia hatufurahishwi na yatokanayo na tupo tayari kusaidia suluhu kwenye mgogoro huo
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Wakati Israel anavamia Palestina mlipiga kura?
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Unataka tuchezeshwe ngoma..?
 
Ni lini tutakuwa na viongozi wawazi?
Kwa nini tusiwaambie ukweli NATO/ AMERICA kwamba mmekosea.?

Hawa North Atlantic Terrorists Organization ndio wanachochea vita.

Wanapeleka silaha kuua watu.

Katiba mpya ili tupate viongozi wenye maono.
 
Sasa mnapotoa msimamo uliothabiti wa kutofunganana na upande wowote kwenye migogoro ya kimataifa kama huu unaoendelea, msiwe wepesi wa kupokea misaada inayolenga kulainisha na hatimae kupindisha maamuzi au kutoa kauli kuhusu mgogoro wa Ukraine.

Jana tu, mmepokea msaada kutoka EU ambao masharti yake Labda mnayajua ninyi tu, lakini Tangu wiki ianze tunashinikizwa tuonyeshe tuko upande gani kwenye mgogoro walioutengeneza wao kwa makusudi ya kuuza silaha.
 
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu- Mungu hapendi kauli kama hizi, hata ktk vita ya malaika Gabriel na Lucifer - wale malaika wote walio kaa kando kuangalia mshindi ni nani ili wajiunge naye - waliswekelewa mbali pamoja na kundi la Lucifer...

Yaani Ukraine inavamiwa na inajitetea kutetea sovereignty yake na bado sisi kama nchi tunasema tuko neutral...je ikitokea sisi tukavamiwa na majirani na kupewa kauli kama hii, tutaona ni Sawa?
 
Kutokupiga kura kuunga mkono upande wowote kidiplomasia maana yake ni kuwa na upande lakini tunaogopa kuunyosha wazi wazi. Na katika hili la sasa maana yake Tanzania tumechagua upande wa Vita, tunawaunga mkono Urusi kwa 100%, hivyo huyo waziri wa mambo ya nje wa Tz aache kutufanya sote wajinga. Na katika hili tujiandae kulipa gharama.
Mimi ni mtanzania ambaye namsapoti mrusi kwa kuwapa mkwara nato.

Lakini wakati huo huo simsapoti mrusi kuingia ukraine.

Na wakati huo huo simsapoti marekani kuzuia mafuta ya urusi.

Na wakati huo huo simsapoti ukraine kwa kutokukubali kuwa bwege kwa mrusi.

Hivyo hata mimi ningekuwepo kwenye kura nisingefungamana na upande wowote ule kwa sbabu mambo ni magumu sana.
.kuchagua upande fulani ni ufinyu wa akili
 
Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.
Hakuna nchi zilizopoteza 'credibility' kama hawa mabeberu wa Ulaya. Iraq ilipovamiwa walisemaje, uliwasikia?

Wamerikoroga, acha walinywe wenyewe, wasitake kutuingiza sisi kwenye mambo yao ya kinafiki.
 
Na wakati huo huo simsapoti ukraine kwa kutokukubali kuwa bwege kwa mrusi.
Huu mstari, sikuelewi mkuu, ingawaje hayo mengine kidogo yamenyooka.

Ukraine amekuwa bwege kwa hao wanafiki waliomtumia kama chambo, na bado wanamtumia kwa kumpelekea visilaha ili aendelee kupata maumivu nzaidi huku wao wakipigia kelele pembeni.

Kama ni vidume si waingie uringoni?

Urusi ingekuwa kama ki-inchi fulani hivi, wakati huu ungekuwa unasikia hawa wakiwika kwa kupeleka majeshi yao kukimaliza ka-nchi hako. Hapa wanabweka wakiwa nje.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu- Mungu hapendi kauli kama hizi, hata ktk vita ya malaika Gabriel na Lucifer - wale malaika wote walio kaa kando kuangalia mshindi ni nani ili wajiunge naye - waliswekelewa mbali pamoja na kundi la Lucifer...

Yaani Ukraine inavamiwa na inajitetea kutetea sovereignty yake na bado sisi kama nchi tunasema tuko neutral...je ikitokea sisi tukavamiwa na majirani na kupewa kauli kama hii, tutaona ni Sawa?
Kwani hatujawahi kuvamiwa mkuu?

Mbona historia unaisahau, hata kama wakati huo hukuwepo! Nduli alivamiaga hapa.

Baadhi ya hao hao wanaotuhimiza leo kuwaunga mkono sasa hivi, wakati huo hawakuwa na habari nasi kabisa.
 
Tamko hilo lilitolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, jana Machi 22, 2022, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.
Marekani ilipoivamia Iraq hao mabalozi walitoa tamko gani?

Marekani ilipoivamia Syria hao mabalozi walitoa tamko gani?

Marekani walipomuua Muammar Gaddafi hao mabalozi walitoa tamko gani?

Marekani wanaongoza duniani kwa kuua watu wasio na hatia kutokana na tamaa yao ya kishetani ya kutaka kutawala dunia, lakini hatusikii hao mabalozi wakitoa matamko yoyote. Kwa nini watulazimishe sisi kufuata matakwa yao kipindi hiki?

Haya ndiyo Imran Khan ameyakataa na kuwaambia sisi siyo watumwa hao. Wangekuwa na akili wangeelewa.
 
Huu mstari, sikuelewi mkuu, ingawaje hayo mengine kidogo yamenyooka.
Nimekusudia kwamba ùkraine ilikuwa ajishushe kwa mrusi,ajifanye lofa kwa mrusi ili waelewane hilo lingeepusha hii vita kutokea.
Akini ukraine akamkazia msuli mrusi matokeo yake ndio haya.

Hivyo ukraine naye amechangia kupigwa kwa sababu aliona jau kujifanya bwege kwa mrusi huku akifai kwamba yeye ni nchi huru.
 
SAWA.
Ukraine alitumika na akadhani kutumika kwake kutamlinda.

Unapoishi karibu na papa kama Urusi, ni lazima uwe mwangalifu sana katika mambo unayofanya.

Isingekuwa kukubali kwake kutumika, yote haya yasingekuwepo.

Utahatarishaje uhai wa li-papa, halafu ukadhani utabaki salama.

Sasa hawa mabalozi na wao wanatutishia, eti wanasema, "pamoja na kuheshimu uamzi wetu, eti wanaamini maslahi ya Tanzania yanafana kwa kuilaani Urusi"
Miaka na miaka tumekuwepo nao, mbona maslahi yetu hayajabadilika chochote.
 
Back
Top Bottom