kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Tulipopata Uhuru Kazi yetu kubwa tuliyojipa ni kuwapatia wengine pia uhuru. Kazi hii haikuwa lelemama, ilikula mtaji wote tulioachiwa na mkoloni pamoja na rasilimali zetu nyingine kama vile muda na watu. Tulisahau kuwa watu wetu wataongezeka na kuhitaji huduma, nafasi, chakula, malazi na mavazi zaidi ambayo mkoloni hajatuachia. Matokeo yake watu sasa wanahitaji chakula, hospitali, malazi, mavazi, shule, ardhi, barabara, kulindwa, maji na viwanja vya michezo zaidi kuliko wakati tulipopata Uhuru na ambavyo sasa hatuna na Kazi ngumu kuvipata. Kwakuwa hatukuwaza wala kupanga kuhusu hilo Leo ni chanzo cha njaa, maradhi, foleni barabarani, ujenzi holela, mizozo ya ardhi, ukataji misitu, elimu duni, NK.
Yaliyopita si ndwele, tusilaumiane, je sasa tuanzie wapi kurekebisha kule tulikokosea au ndio basi tena?
Yaliyopita si ndwele, tusilaumiane, je sasa tuanzie wapi kurekebisha kule tulikokosea au ndio basi tena?