Tanzania hatuhitaji demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hatuhitaji demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtweve, Apr 29, 2010.

 1. mtweve

  mtweve Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama vitu kwa mtazamo wangu havihitajiki katika nchi hii ya tanzania ni kuwa na mfumo wa serikali kupatikana kwa njia ya demokrasia.Najua nitapingana na wengi labda wakidhani kama hakuna demokrasia basi mbadala wake ni udikteta! zipo aina nyingi sana za serikali,labda tu kwa kuwa kumbusha kuna MONARCHY, ARISTOCRCY, FEDERATION, TYRANY nk.

  Ngoja niseme hivi,mfumo huu ambao leo karibu Africa nzima tunaushabikia ulianzia Ugiriki.Kwa wao demokrasia ilimaanisha WATU WOTE waruhusiwe kufanya maamuzi yanayohusu jamii husika.Abraham Lincolin anasema demokrasia ni serikili ya watu.iliyotokana na watu, kwaajili ya watu.

  Hapa ndipo penye tatizo lenyewe,watu hawa ni akina nani? Je kila mtu ni mbele ya demokrasia? kama ndiyo, kwa nini mwingine anaruhusiwa kupiga kura na mwingine haruhusiwi? au kwa nini hakuna mgombea binafsi?

  Muda mwingine huwa najiuliza ni watanzania wangapi wanajua maana halisi ya demokrasia? Hivi kweli mtu anaweza kuendesha gari bila hta kufundishwa au kujifunza mwenyewe? Hizi ni ndoto za mchana huku unatembea! Hapa ndipo unaona watu wanachagua chama na si kiongozi bora, kwasababu hawajui wajibu wao. Marekani nchi inayotajwa kuwa juu kidemokrasi ni WATU 534 tu ndio wanopiga kura kuchagua raisi pamoja na kuwa na watu zaidi ya bilioni 1.

  Kama tunataka mendeleo basi tuwaachie wasomi na watu wengine wenye upeo wakachagua badala ya watu ambao hawjua kutuchaglia watu hivyo,la sivyi tuishi kwa mfumo wa kifalme.

  Tukiendlea hivi tutaendelea kuwaweka mafisadi madarakani
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kijana naona unatumia marekani kama dhana kuu ya mfumo wa nchi yetu, sisi hatuna sababu ya kuiga
  kila kitu toka kwao, na mfumo wa demokrasia lazima tufanye maboresho sisi wenyewe na si kuiga
  tanzania tuna nafasi kubwa kufanya hivyo lakini mabadiliko hayo ni lazima yaendane na kiwango cha
  elimu kwani jinsi watu wanavyoelimika ndio nafasi ya kukua kwa demokrasia inavyokuwa, na suala la
  kusema watu wachache wachague rais ni la kibaguzi na si la kuleta katika nchi yetu, napenda watu
  wajue kwamba demokrasia haiji kwa siku moja ni mfumo endelevu, na kikubwa ni wakinanani
  wanaogombea uongozi kwani ata ukiwa na mfumo mzuri kiasi gani wa kuchagua rais kama hakutakuwa
  na watu bora wa kugombea urais basi ni kazi bure
   
 3. mtweve

  mtweve Member

  #3
  May 4, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naona bado hata wewew neno endelevu bado linakupa shida,huwezi kujadili kuwa ipo siku tutakuwa na mfumo bora wakati kila kukicha waliopo madarakani wanafanya juhudi kuhakikisha watu hajui wajibu wao.kwa mfano kwa nini kura nyingi zaCCM ambazo huipa ushindi hutoka vijijni? jibu ni rahisi kwa sababu huko ndiko watu hawajui demokrasia nini!wao wanadhani demokrasia ni kuwa tu huru kuchagua mtu ambaye unadhani anafaa,na kwa wao anayefaa ni yule ambaye atagawa tsshet,kofia,khanga, pombe nk. katka mazingira kama haya hwezi kupata viongozi bora hata siku moja,hap ndipo ninipo jenga hoja kuwa wachache ambao wana sifa za kutambua nini maana ya uchaguzi
   
 4. j

  jingoist Member

  #4
  May 4, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtweve nakuunga mkono. Demokrasia penye rushwa haswa kama ya bongo ni utapeli. Ukipiga kura inaweza ikaibiwa. CCM wanawatishiaga wananchi kuwa wasipoichagua watawatrack kwenye fomu walizopigia kura na kuwashughulikia ipasavyo (nimeshashuhudia hii live). Huwa wanawahonga na kuwalaghai watu masikini wawapigie kura kwa ahadi za uwongo. Kiongozi akishaingia madarakani hawajibishwi kwa kutokutimiza ahadi zake. Moja tu hilo la vitisho ni kubwa sana, mkulima masikini anatishiwaga kunyanganywa mazao na mifugo yake na hili huwa linatokea kweli kwa ajili ya intimidation kwa wanaoshuhudia. So demokrasia iliyopo ni hewa tu!
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  elimu kwa kila mtanzania ndio itayokuza demokrasia, rushwa haiwezi kuondolewa kwa kupunguza wajumbe wa kupiga kura
  bali inaweza kuongezeka kama watu wachache wakiamua kuwa wao ndio wawakilishi wetu,kwani kwa mfano bunge letu
  linatusaidia nini , bora lisingekuwepo kuliko usaliti linalotufanyia,
  elimu ndio pekee itamkomboa mtz na kumletea demokrasia ya kweli kuliko kukimbilia mifumo na majaribio katika taifa letu
   
Loading...